- Source #1
- View Source #1
Habari wakuu,
Kama kweli ni kauli ya Maria Sarungi simuuungi mkono
Naona Maria Sarungi katema cheche huku akidai Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche pmoja na Jonathan Lema kuwa uongozi wao wa Mabavu umeua CHADEMA
ilhali tangu CHADEMA ikumbwe na matatizo ya kisiasa ya kufungiwa kufanya shughuli za kisiasa na Mwenyekiti wao Tundu Lissu kukabiiwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo uhaini, hawa watu wawili wamekuwa wakionekana kusimama imara na kutetea maslahi ya CHADEMA na kuendelea kukemea matukio ya ajabu yanayoendelea nchini

- Tunachokijua
- Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.
Madai
Kupitia mtandao wa Facebook mtu mmoja alichapisha taarifa iliyoambatana na grafiki ya chombo cha habari cha Mwananchi ikiwa na ujumbe unaoleza kuwa Maria Sarungi amesema Heche na Lema wakeiua CHADEMA kwa uongozi wa mabavu.
Grafiki hiyo imeambatana na ujumbe unaonekan kuchapishwa katika ukirasa wa X wa Maria Sarungi akitoa shutuma hizo dhidi ya Heche na Lema.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo haina ukweli.
JamiiCheck kwa kutumia njia za kimtandao na utafutaji wa maneno muhimu imebaini kuwa ujumbe huo unaonekana kuwa ni kutoka katika ukurasa wa X wa Maria Sarungi ni wa kughushi kwani haujachapishwa naye.
Aidha grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi na haijachapishwa na chombo cha habari cha Mwananchi. Grafiki hiyo ina mapungufu kadhaa ikiwemo mpangilio tofauti na ule unaotumiwa katika grafiki halisi za chanzo hicho.