Mariam Uswazi: Ikitokea nimekufa kisa albadiri mtajiskiaje?

Mariam Uswazi: Ikitokea nimekufa kisa albadiri mtajiskiaje?

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Story Kubwa Tanzania kwa sasa ni kuhusu@uswazi_food na hela za upatu ambao watu wanalalamika na kuomba misaada ili warudishiwe hela zao yan walipwe. Siku Ya Leo Mariam alipiga simu na akaongea upande wake wa story ya kwamba wengi wamevunja taratibu za mchezo huo , akiongea na Diva kupitia njia ya simu ya mkononi kwa Malalamiko ya story yake kutokuwa balanced Mariam amesema suala hili lina pande mbili zinazopaswa kusikilizwa, akidai kuwa katika michezo ya upatu, wengi wamevunja katiba za mchezo wao wenyewe, akiwemo Nipher Cosmetics ambae hata kabla hajamaliza mchezo na kufikia zamu yake ya kupokea alipiga simu akitaka hela zake ambazo hela hizo ziko ktk mzunguko!.

Aidha, Mariam amezungumzia video inayodaiwa kusomwa Albadil, na kuuliza: “Ikitokea nimekufa, tutajisikiaje? hata wewe Diva unaefanya kazi yako ya uandishi wa habari hautalia?! ameuliza ?! amesisitiza yanayoendelea yanamuumiza sana sababu yeye ni binadamu ana watoto ndugu na wazazi na zaid yeye ni mfanyabiashara na haya mambo hapendezewi nayo , ameuliza Diva Mimi nimetokea Mikononi mwenu ukiwemo wewe ulipambana mimi kuwa hapa mpaka kupata tuzo miaka ya nyuma unajisikiaje ? (Diva - Mimi nafanya kazi yangu Malalamiko ni mengi sana na siwezi kuacha ' Diva anajibu huku akisisitiza kama anahitaji kweli haya mambo yaishe amalizane nayo kwa njia sahihi maana yamefika mbali sana huku Diva akisisitiza lazima kama waandishi kazi yetu kwa jamii ni kuhakikisha tunapaza sauti hasa mambo yanavyofika mezani kwetu.

Mariam amesikitika na kinachoendelea na Amesisitiza umuhimu wa kusikiliza pande zote za mgogoro na kufuata utaratibu unaostahili.

mariam uswazi.png
 
Huyu bint anatafuna hizo za wajinga na mtu, maana kelele nyingi lakini yupo kitaani anadunda.
 
Mm mwnyw nikisikia mariam amekufa ntalia sana 😭

Tutapata wapi mwanamke mwenye akili timamu hv ya kuweza kutumia fursa ya uwepo wa wajinga wajinga kama hao ili kujinufaisha 😂
 
upatu ni kinyume cha sheria ila upatu mkubwa kama huu unahitaji watu walio serious na wanaojielewa imagine wewe ndio kijumbe alafu unachezesha mchezo mil 1 kwa wiki watu 10 kila mtu anapokea mil 10 kila wiki sasa mchezo umeanza jina la kwaza hadi la 3 watu wamechukua hela mil 10 kila mmoja alafu zengwe mmoja anaanza kudema dema kutoa rejesho wiki imefika mwenye zamu anataka mil 10 watu watatu hawatoi hela cash una mil 7 watatu wamedema hapo ndo ugumu wa hio kazi unapoanzia je utaufanya mchezo uwe wa mil 7??

vipi wale wa mwanzo washachukua 10 zao au kijumbe utajazilia hela zako mchezo uendelee ili upokee kwenye majina yao ujilipe?? vipi kama hauna??
hio ndio shida ya upatu ilipo kingine unaweza tumia hela za wengine au ukauza jina mwingine aliendeleze lile jina na ukifanya hivyo it meas zile hela za wale waloshindwa maliza mchezo kupatilana kwake hadi mwisho wa mchezo.

nilisikia anawasainisha mikataba kwamba ukiishia kati hela unaweza usipewe nao wakasaini 😂😂

pili kijumbe ana miradi mingi inayotokana na hela za mchezo huo anafanya kama NSSF hela anazungushia kwingine.
 
Back
Top Bottom