Chadema wakikubali mtego wa CCM kuingia kwenye maridhiano yasiyo na tija watakuwa wamejimaliza wenyewe, madai yao yote yatafunikwa na blanketi la maridhiano.
Chadema itakuwa imejiziba mdomo kwa mikono yake yenyewe kila kitu wataambiwa wasubiri matokeo ya maridhiano.
Maridhiano feki hayana tofati na tume ya Chande ya kupumbaza jumuiya za kimataifa, wananchi na wahisani.
Chadema ikiingia kwenye maridhiano 'feki', means kwa heri mpatanishi huru wa kimataifa, mswada wa bunge la Marekani hautakuwa na nguvu tena itabidi usubiri matokeo ya maridhiano.
Kombo atazunguka dunia nzima kuelezea mafanikio ya CCM kufanikisha maridhiano hata kama hayapo.
CCM watatumia tukio hilo zikiwemo picha kwenda kujitetea kwa wahisani na kuwaambia kuwa wametekeleza madai yote ya wananchi na upinzani.
Maridhiano bila Lissu kutoka itakuwa ni kumsaliti Lissu na CCM itatumia mwanya huo kupandikiza mifarakano ndani ya Chadema.
Maridhiano yatatoa matumaini hewa ya kupatikana kwa katiba mpya, na utakuwa ndio mwanzo wa mwisho wa madai ya katiba mpya.
Maridhiano yatahusisha vyama mamluki ambavyo vitataka haki sawa kwa vyama vyote hata kama vilikuwa havina sababu ya kuridhiana lengo ni kupunguza sauti ya Chadema.
Maridhiano bila kutekelezwa kwa sababu za msingi zikiwemo; Haki kwa wahanga wa Mo29, kurudiwa kwa uchaguzi huru, kufutwa kesi ya mchongo ya uhaini ya Lissu, kuachiwa kwa wafungwa wote wa kisiasa, kuwajibika kwa watuhumiwa wa mauaji ya Oktoba 29, kuwajibika kwa watekaji, ratiba ya kupatikana katiba mpya, kitakuwa ni kitanzi kwa Chadema.
Chadema kamwe isiingie kwenye mtego huo, Chadema ijiulize kwanini CCM akiwemo mama Samia wanalazimisha Maridhiano?
By, Quinine.