Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
HAKI NA WAJIBU
Vyama vinavyoendelea na maridhiano ni vile ambavyo ni ngazi na busati la CCM kuendelea kuwahadaa Watanzania ili iendelee kuwatawala kwa minajili ya kulinda ukwasi wa kikundi cha watawala kinachokwapua rasilimali za nchi na kujimilikisha uhalali wa kuamua nani aishi na nani afe ndani ya Tanzania.
Maridhiano tanayoendelea yanakiuka Katiba na Sheria za nchi. Yasitishwe.
- Katiba na sheria vinatoa haki na kila upande yaani raia na dola wana wajibu wa kufana ili sheria itekelezeke.
- Rais anamsema mtangulizi wake kuhusu utawala wa mabavu na vitisho lakini yeye hajafanya lolote kufuta mabavu hayo anataka maridhiano yaendelee huku akiagiza vyombo vya dola kuzuia mikutano ya kisheria ya vyama.
- Vyama vinaitwa meza ya maridhiano kana kwamba sheria zinazoruhusu shughuli za siasa zimekosewa na hazitekelezeki.
- CCM imeweka mapandikizi ndani ya vyama hivyo kasoro kimoja hivyo wanajiona wapo salama kushiriki maridhiano ambayo ni HADAA kubwa kwa Taifa.
- Bunge linatumika kuchafuana wenyewe kwa wenyewe badala ya kuisimamia nchi. Siass imezuiwa kufanyika na hakuna tamko wala azimio la Bunge kuhusu hili.
- CCM inafanya mikutano yake na maabdamano huku ikipewa ulinzi lakini vyama vingine wanazuiwa wakiambiwa hakuna ulinzi lakini jeshi hilo hilo lina kikosi cha mauaji kinachoenda kuwashambulia kwa silaha za kivita endapo watakaidi agizo haramu la kusitisha mikutano yao.
- Mahakama ambayo ndiyo inawajibu wa kutafsiri sheria inapokea mashtaka na kutoa hukumu kwa wanaokaidi maagizo haramu yanayokiuka sheria na katiba kuhusu mikutano na maandamano