Nakubaliana na wewe kwenye hili👆👆👆
Lakini kwa hili 👆 👆👆, HAPANA KUBWA KABISA..!!
Na nakukemea waziwazi kabisa kuwa, kwa wazo hilo umekeunga ndugu yangu
Tindo. Na kwa hiyo namuapiza shetani aliyeweka roho ya ugomvi na machafuko ndani yako ashindwe kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareth...!
Kwa hili, una maana ya kuwa Freeman Mbowe atangaze mapigano kati ya walio madarakani serikalini na bunduki zao dhidi ya wananchi wasio na silaha...!
Is this what you want
Tindo...?
Hili halimhitaji Mbowe kukuambia anza kupigana nao kwa nguvu za mwili wa damu na nyama...
Wewe kama unaona njia sahihi ya mazungumzo ya amani mezani inakuchelewesha, unaweza tu kuanza wewe kupigana nao na wakitokea watakao kuunga mkono, basi mnaliendeleza kwa pamoja....!!
But I am strongly sure that, kwa njia hii Mbowe na CHADEMA together are in the right track....
Labda ungeweza kushauri kuwa, CHADEMA wanapaswa kuwa aggressive a little bit kwa kuilazimisha serikali na chama kilicho kwenye dola yaani CCM kufanya vitu fulani fulani especially kutoyafanya mazungumzo kuwa ni siri kati ya viongozi wa CHADEMA na CCM/SERIKALI...
Tuwaambie kuwa maridhiano hayo wanayoyafanya ni mali ya wananchi na wao tumewapa dhamana na nafasi tu ya kuzungumza kwa niaba yetu sote...
Na kwa hiyo lazima kuwe na updates za mara kwa mara ya nini kinaendelea na kuwe na framework ya process yote ya dialogue hiyo kuonyesha yameanza na yanatakiwa kuisha lini...
Isiwe ni mazungumzo yasiyo na mwisho. Mazungumzo ya namna hiyo ni mchezo usio na tija huku yakila fedha ya umma tu....
Lakini kuomba kutokee machafuko kwa sababu iwayo yoyote is not an alternative solution ya changamoto za nchi hii zaidi kwamba italeta adha na maumivu yasiyo na sababu kwa watoto wetu bure.....
Tindo, CCM hii itatoka madarakani bila ya wananchi kupigana sisi kwa sisi. Hawa taratibu wameshaanza kujinyonga wenyewe na mwisho watakata roho kabisa...!