Maridhiano yanayoendelea ni hadaa kwa Taifa. Vyama vijitoe kabla havijakaangwa


Hilo ndio suluhisho sio kujikomba kana kwamba mama Samiah ana jema Sana.
 
Hakuna chama chochote cha upinzani ambacho hakina mapandikizi,ccm ni habari nyengine upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm sio cuf,act wala nani uko

Acha kauli zilizopitwa na wakati.

Una maanisha utakatifu utaletwa na shetani?. Yani ccm ( shetani) ndio ataleta upinzani wa kweli (utakatifu). Tuache kuongea mambo ambayo siyo realistic.
 
Huyu mama Ni majanga. Sijui wanampendea Nini? Nilidhani atakuja na mambo tofauti kumbe naye ni mnafiki unazuia wapinzani kufanya siasa halafu unakopa Trilioni 91 na tozo juu.
 
Acha kauli zilizopitwa na wakati.

Una maanisha utakatifu utaletwa na shetani?. Yani ccm ( shetani) ndio ataleta upinzani wa kweli (utakatifu). Tuache kuongea mambo ambayo siyo realistic.
Kwa hiyo unakataa kuwa chadema hakuna mapandikizi ya ccm?
 
Maridhiano ya nini? Awaambie wananchi wameongea nini kwenye maridhiano
Ameongea Marekani huko ndio walipa kodi wapo?
Heche kanyaga twende!
Huku ni kupotezeana muda na kuwadanganya wananchiโ€ฆ
Kundi kubwa limeenda Marekani kufanya nini? Mwenyekiti na Makamu why?
Kuna watakaochukia but tusidanganyane lipo jamboโ€ฆ
 
Dj anajua ila maridhiano ambayo hayana time frame ni kama kuhadaa watu
 
Mbowe aache kuitumia CDM kufanya maridhiano ya kitapeli. Kama ana maslahi yake binafsi na hayo maridhiano, basi aachie uenyekiti lakini sio kugeuza watu kuwa mateka wa CCM. Machafuko pekee ndio njia ya kuheshimiana sio zaidi ya hapo.
 
kumbe hata huyajui maridhiano.
maridhiano ni baina ya ccm na CHADEMA wewe unasema vyama vyote.

jichunguze kwanza
 
Mbowe aache kuitumia CDM kufanya maridhiano ya kitapeli. Kama ana maslahi yake binafsi na hayo maridhiano, basi aachie uenyekiti lakini sio kugeuza watu kuwa mateka wa CCM.
Nakubaliana na wewe kwenye hili๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†
Machafuko pekee ndio njia ya kuheshimiana sio zaidi ya hapo.
Lakini kwa hili ๐Ÿ‘† ๐Ÿ‘†๐Ÿ‘†, HAPANA KUBWA KABISA..!!

Na nakukemea waziwazi kabisa kuwa, kwa wazo hilo umekeunga ndugu yangu Tindo. Na kwa hiyo namuapiza shetani aliyeweka roho ya ugomvi na machafuko ndani yako ashindwe kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareth...!

Kwa hili, una maana ya kuwa Freeman Mbowe atangaze mapigano kati ya walio madarakani serikalini na bunduki zao dhidi ya wananchi wasio na silaha...!

Is this what you want Tindo...?

Hili halimhitaji Mbowe kukuambia anza kupigana nao kwa nguvu za mwili wa damu na nyama...

Wewe kama unaona njia sahihi ya mazungumzo ya amani mezani inakuchelewesha, unaweza tu kuanza wewe kupigana nao na wakitokea watakao kuunga mkono, basi mnaliendeleza kwa pamoja....!!

But I am strongly sure that, kwa njia hii Mbowe na CHADEMA together are in the right track....

Labda ungeweza kushauri kuwa, CHADEMA wanapaswa kuwa aggressive a little bit kwa kuilazimisha serikali na chama kilicho kwenye dola yaani CCM kufanya vitu fulani fulani especially kutoyafanya mazungumzo kuwa ni siri kati ya viongozi wa CHADEMA na CCM/SERIKALI...

Tuwaambie kuwa maridhiano hayo wanayoyafanya ni mali ya wananchi na wao tumewapa dhamana na nafasi tu ya kuzungumza kwa niaba yetu sote...

Na kwa hiyo lazima kuwe na updates za mara kwa mara ya nini kinaendelea na kuwe na framework ya process yote ya dialogue hiyo kuonyesha yameanza na yanatakiwa kuisha lini...

Isiwe ni mazungumzo yasiyo na mwisho. Mazungumzo ya namna hiyo ni mchezo usio na tija huku yakila fedha ya umma tu....

Lakini kuomba kutokee machafuko kwa sababu iwayo yoyote is not an alternative solution ya changamoto za nchi hii zaidi kwamba italeta adha na maumivu yasiyo na sababu kwa watoto wetu bure.....

Tindo, CCM hii itatoka madarakani bila ya wananchi kupigana sisi kwa sisi. Hawa taratibu wameshaanza kujinyonga wenyewe na mwisho watakata roho kabisa...!
 

Rahisi kupinga ! Tupe mawazo yangu tutaenda vipi mbele kama taifa ukizingatia Watanzania ni waoga sana hata kuandamana ni shida
 
Rahisi kupinga ! Tupe mawazo yangu tutaenda vipi mbele kama taifa ukizingatia Watanzania ni waoga sana hata kuandamana ni shida
Kwani wewe Kamundu siyo mtanzania..?

Kama ni mtanzania, kwanini unajitoa? Ina maana na wewe ni mwoga vilevile, au siyo...?

Kama jibu ni HAPANA, basi kumbe unaweza kuanza kuvaa wewe ujasiri wa kuanzisha maandamano or any other kind of physical confrontations dhidi ya watawala ili ku - achieve political ambitions zenu...!

Yaani nyie ni kama vimbwa koko vile vioga. Mnabweka mkiwa pembeni kwa kuhimiza wengine waanzishe vurugu za kisiasa huku nyie wenyewe mkiwa mmejificha vyumbani msiguse sekeseke hilo hata kwa vidole vyenu...!

Mnakosea. Vita hivi vinapiganwa kwa HEKIMA na MAARIFA.. Tundu Lissu kalisema hili several times sijui kwa nini hamuelewi...

Mtawezaje kupigana na watu wenye silaha huku nyie mkiwa mikono mitupu? Mtakuwa hamna akili kuingia kwenye vita ya namna hiyo...!!

Acheni watu wazungumze ili kumaliza tofauti zao za kisiasa. Kama kuna mahali wanakosea, shaurini namna ya kuboresha ili mwisho wa siku nchi hii ubaki salama na yenye umoja...

Nchi na wananchi wa nchi hawana shida. Shida ni baadhi ya viongozi wachache ndani ya CCM...

Hatuhitaji kutumia bomu la nuclear kuua panya ndani ya nyumba yetu....!
 
Aliyetengeneza uwepo wa jambo hilo anajulikana ni CCM.

Tusishangae haya
 

Sipingi unachoamini, lakini narudia tena, bila machafuko ni kupotezeana muda. Sihitaji kuambiwa na Mbowe maana tayari Mbowe ameshasalimu amri. Kenya hapo baada ya machafuko leo hii heshima ni tele. Mazungumzo ya mezani wakati wapinzani wanaonekana ni waoga, hakuna maridhiano hapo bali ni kuchorana.
 
Rahisi kupinga ! Tupe mawazo yangu tutaenda vipi mbele kama taifa ukizingatia Watanzania ni waoga sana hata kuandamana ni shida
MAandamano yanaweza kuwa suluhisho na labda yakawa chanzo cha shida mpya.

Kwa hali yetu Tanzania tunapaswa kuanza kujenga misingi kuanzia chini. Kuondokana na siasa za uharanakati na kupalilia siasa za mikakati.

CCM imejitwalia mamlaka ya kupenya kwenye viapo vya majeshi yetu halafu sisi wananchi tumebung'aa na kushadidia propaganda hatarishi za nchi yetu.

Ninaongea kwa dhati moyoni kwamba. Vita ama machafuko nchini havitaletwa na upinzani bali watawala ambao watayapigania maslahi yao na siyo maslahi ya nchi.


Nimewaza kwamba. Hadaa ya maridhiano inatumika kama taswira ya nia njema ya serikali iweze kukopesheka huko duniani.


Wananchi wanahitaji kujengwa na siyo kupelekeshwa. Mwisho wa siasa za kiushabiki ni mchezo wa mauti kwetu sote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ