miaka ya nyuma nilikuwa nawawazia sana wasanii wetu, nilikuwa nawaona kwa TV na hata kuwasikiliza kwa radio mbali mbali wakilalamika kuhusu kazi zao kuibiwa na ingawa wanawasilisha malalamiko yako serikalini kupita BASATA ila serikali bado inafumbia macho na wala haiwasaidii. ila kipindi cha kampeni unaskia wakizunguka na wanasiasa na hata nyimbo zao zinazopendwa wanazibadili na kidogo na kukipaisha chama tawala, nikawa nasema kwa nini WASIKATAE kwa nini serikali inawatafuta kipindi cha kampeni tu na baada ya hapo inawaacha wanaibiwa kazi zao na wala haiwainui wafuraie matunda ya kazi zao. ila sasa nashukuru marlaw ametokea na ameongea kwamba uchaguzi ujao hataki shobo na wanasiasa hivyo wamuache. i wish kama wasanii wengine wakafuata njia ya ndg marlaw, umwamba umwamba unamwaga mboga nami natupa ugali.