Mkuu mimi sifahamu kitu chochote bali niliyoyaandika hapa ni maelezo ya Martha Mwaipaja ndiyo maana kwenye andiko hili jina Martha Mwaipaja limetokea kama lote, yote hii ni kwa kuwa sijafanikiwa kupandisha clip ya Martha Mwaipaja akiongea. Hivyo kama kuna sehemu pamepotoka wewe jazia tu usipate taabu.
Ahsante kuna upande wa pili wasanii au waimbaji huwa hawapendi kuuzungumzia sabbu wanajua wanayoyafanya.
Maisha ya waimbaji wengi wa muziki wa injili wa kike ni Matatizo matupu.
Mwanamke akishapata jina kubwa huwa anatamani awe na mabawa aruke juu zaidi ya uwezo wa mbawa zake.! Ukiona mwanamke amesimama vema kwenye muziki wa injili kwa muda mrefu na jina lake bado lina nguvu jua ama ana mume ambaye ni very strong! Au ana meneja ambaye ni jeuri sana.
Ni kweli kuna wakati inabidi nguvu ya ziada itumike ikiwepo kumchapa vibao pale ambapo unaona kabisa anakoelekea ni tatizo kwake na kazi iliyo mbele yake.
Hebu angalia nyuma ya maisha ya waimbaji kama Florah Mbasha je yuko wapi leo, Bahati Bukuku je kayapitia yapi?
Hao ni wachache lakini nyuma ya muimbaji wa Injili unayemuona wewe jukwaani kuna mtu ambaye analazimika kufanya kazi ya Ziada.
Siku nikipata nafasi kwa ruhusa yake nitaeleza hapa kuhusu Nathan. Kule alikomtoa Rose muhando pale alipomfikisha na mpaka kuporomoka kwa Rose muhando.! Msisahau kashfa za Rose muhando na Nathani hazikuanza leo ziandikwa sana na magazeti ya Erick shigongo.!
Lakini kwa wakati wote huo Rose alikuwa bado chini ya usimamizi wa Nathani na alikuwa anafanya vizuri sana.! Kwenye anga la muziki wa Injili. Baada ya Rose kuondoka kwenye mikono ya Nathani kipi kimeendelea..? Msama na kundi lake wanajua. Na wale waliokuwa wanamsimamia kule Dodoma wanajua.
Nakumbuka niliwahi leta uzi hapa
"nikisema nataka kumshtaki Rose muhando"!
. Na baadhi ya wadau walichangia sana kwenye ule uzi
Mwisho Rose anachohitaji kwa sasa ni mtu makini nayejua thamani ya muombaji kama Rose, ashughurike na Afya yake kisha amrudishe kwenye anga za muziki wa injili naamini bado ana uwezo mkubwa sana.