Martha Mwaipaja atoboa siri sakata la Rose Muhando

Martha Mwaipaja atoboa siri sakata la Rose Muhando

Naelewa na ndio maana nkaeka mwishoni kuwa hata mfalme daudi alianguka zaidi yake lakini cha kwanza alichokifanya ni kukubali kueka kichwa chini na si kutafuta mtu wa kumuhurumia..

Hakuna mkamilifu ndo maana kuna kuomba toba
Kwani mfalme daudi aliwahi kuonja madawa ya kulevya? Hakika hujui ulisemalo.
 
Lakini ni kosa pale unapokuwa unaweka lawama zote kwa mtu mwingine ili wewe uhurumiwe kana kwamba hujachangia kwa namna yoyote ile kwa ulipofikia...
Lets agree to disagree mkuu
Hajaweka lawama, ameelezea aliangukaje katika dhambi hiyo. Hiyo inaitwa confession
 
Kama aliamini anachokiimba angekubali arudi kwenye umaskini ila amche Mungu. Rose ameanzana na huyo Nathan tangu mwanzo mpaka kanisa likamtenga. That was in 99 au kabla, sasa iweje leo ndo ajitambue.
Majuto ni mjukuu. Halafu hilo ni simulizi la mwaipaja, kwani kumshambulia Rose?
 
Hii stori haina ukweli, haingii akilini hata kidogo au niambiwe Rose ni mtu asiejielewa toka mwanzo.
1 Anapigishwa show za kinyonyaji yeye alichuka hatua gani
2 Analazimishwa kunywa pombe na yeye anakunywa.
3 Analazimishwa ngono na meneja, anabakwa ama inalazimishwa vipi?

Hayo yote hayawezi kufanyika kwa mtu anaejielewa. Labada Rose alikuwa hajielewi tangu mwanzo.
Unaishi dunia gani mkuu?
 
Kweli tena tujifunze kusikiliza kabla ya kuhukumu. Japo upande mwingine haiingii kabisa akilini kuwa mtu wa aina ya Rose aliwekwa chini ya udhalimu huu pasipo hiyari yake na kwamba akakosa kabisa msaada wa kujinasua eti. Huyu Nathan ni nani hadi aweze kurudisha utumwa karne hii, ana serikali yake?
 
nakubaliana na swala la rose kutumia pombe,nina ushahidi wa yeye kutumia viroba vya konyagi yeye pamoja na ma dansa wake,swali je hizo laki tatu ndo zilizompa kiburi cha kumjengea mchumba wake nyumba,ndo zilizo muwezesha kutembelea prado,kujenga nyumba yake ya kuishi huko kisasa dodoma.Huyu ni changu wa muda mrefu kwani hata historia inasema ana watoto kadhaa na kila mtoto ana baba yake.
 
Kweli tena tujifunze kusikiliza kabla ya kuhukumu. Japo upande mwingine haiingii kabisa akilini kuwa mtu wa aina ya Rose aliwekwa chini ya udhalimu huu pasipo hiyari yake na kwamba akakosa kabisa msaada wa kujinasua eti. Huyu Nathan ni nani hadi aweze kurudisha utumwa karne hii, ana serikali yake?
Niambie mambo gani yaliibuka baada ya kifo cha Mangwea
 
Rose Muhando ndiye aliyekuwa akimhudumia mchumba huyu mpya kwani alikuwa na hali duni kifedha. Rose alifikia hatua ya kumjengea nyumba kwao kwa wazazi wa mchumba wake huyu mchumba wake. Kama wahenga wasemavyo bora umfadhili mbuzi utakula mchuzi Rose alimfumania mchumba huyu mpya na mwanafunzi wa shule laivu bila chenga.

Rose Muhando alichanyikiwa na akajikuta amerudi tena na kuangukia kwenye penzi la meneja wake Nathan ambaye ni mme wa mtu.

Na wewe Martha ukaona hiyo nayo ni sababu ya kiutetezi?? Mzinzi toka lini akakosa sababu?? Alipomfumania dogo wake ikawa sababu ya kumrudia X wake mwenye mke??
Kweli nimeamini, mfu humfata mfu mwenzie. Martha, kama umefika mahali pa kumtetea Rose kwa vijisababu hivyo, ulikufa na wewe siku nyingi.
Kama aliamua kumtangaza Yesu hana sababu ya kujitetea kwa lolote kwenye dhambi hii. Jifunze na wewe kuwa; Dhambi haikai yenyewe lazima ijitafutie jirani. Uzinzi mara nyingi humkaribisha ulevi na usodoma. Pole zake, simhukumu ila namshauri asitafute mchawi bali yeye ndiye mchawi wake mwenyewe. Apatane tu na Mungu wake, anyenyekee naye Mungu atamkumbuka tu. Ni lini, sisi hatujui. Amkumbuke Samson mwisho wake aliua wengi kuliko mwanzo. Hivyo na kwa unyenyekevu wake aweza kuponya waimbaji wenzake wengi.
Aache kuwatafuta hao ma Apostle na ma Prophet waliokwisha poteza mvuto na sasa wanatafuta watu wengine watumie migongo yao kupaa tena.
Toba ni kati yake na Mungu wake tu kwani alimtenda Mungu dhambi. Ombi langu kwenu waimbaji wa muziki wa injili; Jichungeni njia zenu ziwe safi shetani asipate nafasi
 
Mkuu mimi sifahamu kitu chochote bali niliyoyaandika hapa ni maelezo ya Martha Mwaipaja ndiyo maana kwenye andiko hili jina Martha Mwaipaja limetokea kama lote, yote hii ni kwa kuwa sijafanikiwa kupandisha clip ya Martha Mwaipaja akiongea. Hivyo kama kuna sehemu pamepotoka wewe jazia tu usipate taabu.
Ahsante kuna upande wa pili wasanii au waimbaji huwa hawapendi kuuzungumzia sabbu wanajua wanayoyafanya.
Maisha ya waimbaji wengi wa muziki wa injili wa kike ni Matatizo matupu.

Mwanamke akishapata jina kubwa huwa anatamani awe na mabawa aruke juu zaidi ya uwezo wa mbawa zake.! Ukiona mwanamke amesimama vema kwenye muziki wa injili kwa muda mrefu na jina lake bado lina nguvu jua ama ana mume ambaye ni very strong! Au ana meneja ambaye ni jeuri sana.
Ni kweli kuna wakati inabidi nguvu ya ziada itumike ikiwepo kumchapa vibao pale ambapo unaona kabisa anakoelekea ni tatizo kwake na kazi iliyo mbele yake.

Hebu angalia nyuma ya maisha ya waimbaji kama Florah Mbasha je yuko wapi leo, Bahati Bukuku je kayapitia yapi?
Hao ni wachache lakini nyuma ya muimbaji wa Injili unayemuona wewe jukwaani kuna mtu ambaye analazimika kufanya kazi ya Ziada.

Siku nikipata nafasi kwa ruhusa yake nitaeleza hapa kuhusu Nathan. Kule alikomtoa Rose muhando pale alipomfikisha na mpaka kuporomoka kwa Rose muhando.! Msisahau kashfa za Rose muhando na Nathani hazikuanza leo ziandikwa sana na magazeti ya Erick shigongo.!
Lakini kwa wakati wote huo Rose alikuwa bado chini ya usimamizi wa Nathani na alikuwa anafanya vizuri sana.! Kwenye anga la muziki wa Injili. Baada ya Rose kuondoka kwenye mikono ya Nathani kipi kimeendelea..? Msama na kundi lake wanajua. Na wale waliokuwa wanamsimamia kule Dodoma wanajua.

Nakumbuka niliwahi leta uzi hapa

"nikisema nataka kumshtaki Rose muhando"!

. Na baadhi ya wadau walichangia sana kwenye ule uzi

Mwisho Rose anachohitaji kwa sasa ni mtu makini nayejua thamani ya muombaji kama Rose, ashughurike na Afya yake kisha amrudishe kwenye anga za muziki wa injili naamini bado ana uwezo mkubwa sana.
 
SIO kweli.

Ni kweli kabisa Nathan alikuwa Menaja wake.

Kama ni hivyo amewezaje kuwa magari mengi na majumba? Kama sio mafanikio kutoka kwa meneja wake?
.
Rose alishiba kiburi.

Tunaomjua Rose hakuwa ameokoka.

Unajua wakati yupo kwaya ya Chimuli Rose Mhando alikuwa anafanya kazi za house girl?

Alipoinuka Kimusiki hakukumbuka alipo toka.

Hata kanisa alilokuwa anasali alikuja kuhama.

Huyu Nathan watu wanamchukulia poa tu. Ni matajiri wa kutisha hapa dodoma. Hapa dodoma ukisema unapesa unajiita mimi ni maluganji. Mwaluganji ni baba yake Nathan ambaye wakati huo alikuwa ni mtu tajiri sana. sasa Nathan si mtu wa kumdhurumu Rose Mhando.

Mwaipaja msiteteane kwa ujinga ujinga. Bila Msama na hawa akina Nathani wahindi wangewafanya vibaya sana. Wakina Nathani na kina Msama wamejitolea kuwatoa katika makucha ya wahindi wa kariakoo leo mnasema walikuwa wanawaibia.

Tutawasikia sana mkiweweseka. Rose maisha haya kwenda kombo na kutumia dawa au pombe au kufirisika yalianza muda mrefu sana Je wewe Mwaipaja ulimsaidia nini?

Wengi wenu mlikuwa mkimkwepa ili msije mkafananishwa naye leo mnajifanya mtetezi wake shame!

Rose Mhando yaliyomkuta yamemkuta atarejea tena kwa nguvu mpya na ujasiri wa Bwana.

Mwaipaja umefanya kosa kubwa kutaja hadhalani mambo ya mtu binafsi (Personal) wewe ni nani?. Wewe ya kwako ni yapi? Tunajua waimbaji wa Injili maarufu wengi wenu mmeachika na waliobaki ndoa zao ziko hoi kabisa.
Umesema ukweli mtupu namefanya kazi na hawa waimbaji wa mziki wa injili hasa wa kike ninawafahamu wote na tabia zao atokee mmoja hapa abishe nitaanika kila upumbavu ambao huwa wanafanya sema Neema tu ya Mungu inatufanya tuliyo nyuma ya umaarufu wa majina yao tukae kimya.
Kuna vita kubwa sana ya kiroho kwenye muziki wa injili na hao wanaosikika leo wapo kwa sabbu kuna watu wanachomwa na kuumia sana kwa matendo yao lakini wanawabeba sabbu ni dhamana yao.
Nina hakika kama Rose angekuwa bado kwenye mikono ya Nathan asingefika hapo alipo leo.
 
Yes, baada ya kumuingiza kwenye madawa unahisi angekua tena yule Rose wa zamani? hayo yote uliyoyasema ni matokeo ya madawa ya kulevya aliyokua anapewa na huyo Nathan.

Hapo hawezi kuchomoka.
Una hakika.? Mkuu. Unaweza kututhibitishia hilo? Usisahu kuna watu wanawajua hao watu kuliko wewe unavyowafahamu kupitia hii mitandao ya kijamii.
 
Una hakika.? Mkuu. Unaweza kututhibitishia hilo? Usisahu kuna watu wanawajua hao watu kuliko wewe unavyowafahamu kupitia hii mitandao ya kijamii.
Kwa hiyo wewe unaewajua unataka kututhibitishia kua Rose hatumii madawa?
 
Amekuwa akitumia ngada kitambo sana ......baada ya kupigika kifedha akajingiza huko,MI stress
Mambo ya kuondoa uchovu fiksi tu

Ova
 
Kwa hiyo wewe unaewajua unataka kututhibitishia kua Rose hatumii madawa?
Nimekuuliza una hakika.! Unawafahamu,? Najua mapenzi hupofusha najua binafsi unaumizwa na hali ya Rose nikuhakikishie sio peke yako tuko wengi sana tunao umizwa na ile hali.
Jambo la maana hapa ingekuwa tunajadili namna bora ya kumsaidia kuondokana na hali aliyopo sasa.sabbu kuzidi kupotea kwake hakunisaidii mimi wewe wala familia yake( hasa watoto wake) kama mzazi naweza kuu hisi uchungu ambao watoto wake wanaupata.! Ana watoto wakubwa na wenye akili sana.!

Je njia bora ya kumsaidia Rose ni ipi?
Kuna uzi nimeanzisha humu nikiomba msaada kwa Mh Rais kama anaweza kutusaidia kwa hili. Kama walivyo saidiwa akina Ray C. Na wengine.
Ninajua JF ina watu wenye taaluma na vipawa tofauti ni vema tukajitoa kwenye hili kwa msaada wa mawazo ama namna nyingine

Hata kama haitakuwa kwa faida yake basi faida ya watoto wake naamini kizazi kijacho kitaheshimu zaidi mchango wetu kuliko kutupiana lawama zisizo na msingi ama faida yoyote.
 
Ina maana Rose alikuwa akimuheshimu huyo Nathan kuliko Mungu wake na kama kuwa na Nathan ilikuwa ni kosa je,vipi alivyomfumania huyo mchumba wake ilimbidi arudi kwa Nathan....

Lengo la aliyetoa story ni kumuonesha Rose kama ni mtu aliyeonewa kana kwamba alikuwa hana akili na utashi wa kiroho kumuongoza.. Inabidi wakubali kuw a ROSE KAMA ROSE NAYE ALITELEZA ..hii itamsaidia kutoka huko, Kama Daudi aliteleza kwa kuua kwa ajili ya mwanamke je, Rose amefanya kubwa lipi hadi asisamehewe

Natumaini hujawahi kupitia magumu ya maisha usiombe ndugu, hii critical thinking yako utaitupa kule, huwa tunahukumubsana tukiwa pembeni, ukiingia ulingoni ni kilio
 
Wengi naona mnamtuhumu sana Rose kama alijipoteza mwenyewe na inaonekana mnamjua vizuri hasa story za maisha yake halisii...! Kwanza rose nasikia alikuwa muslim na hakuokoka kabisa alikuwa anafanya injili kama Biasharaa... Sema tumuombee tu aponee yule mama ni zaidi ya Kipajiii...
 
Back
Top Bottom