Kwani mfalme daudi aliwahi kuonja madawa ya kulevya? Hakika hujui ulisemalo.Naelewa na ndio maana nkaeka mwishoni kuwa hata mfalme daudi alianguka zaidi yake lakini cha kwanza alichokifanya ni kukubali kueka kichwa chini na si kutafuta mtu wa kumuhurumia..
Hakuna mkamilifu ndo maana kuna kuomba toba
Hajaweka lawama, ameelezea aliangukaje katika dhambi hiyo. Hiyo inaitwa confessionLakini ni kosa pale unapokuwa unaweka lawama zote kwa mtu mwingine ili wewe uhurumiwe kana kwamba hujachangia kwa namna yoyote ile kwa ulipofikia...
Lets agree to disagree mkuu
Majuto ni mjukuu. Halafu hilo ni simulizi la mwaipaja, kwani kumshambulia Rose?Kama aliamini anachokiimba angekubali arudi kwenye umaskini ila amche Mungu. Rose ameanzana na huyo Nathan tangu mwanzo mpaka kanisa likamtenga. That was in 99 au kabla, sasa iweje leo ndo ajitambue.
Unaishi dunia gani mkuu?Hii stori haina ukweli, haingii akilini hata kidogo au niambiwe Rose ni mtu asiejielewa toka mwanzo.
1 Anapigishwa show za kinyonyaji yeye alichuka hatua gani
2 Analazimishwa kunywa pombe na yeye anakunywa.
3 Analazimishwa ngono na meneja, anabakwa ama inalazimishwa vipi?
Hayo yote hayawezi kufanyika kwa mtu anaejielewa. Labada Rose alikuwa hajielewi tangu mwanzo.
Maswali mazuri sana kauliza sema tu na wewe umepeleka akili likizo au umezikodisha huwezi yatazama mambo katika logic yake.Unaishi dunia gani mkuu?
Shangaa wewe my dear, yaan tajiri hajawahi kuridhika hata siku moja, sijui watu huwachukuliaje wengine.Utafikiri kuna mahali pameandikwa ukiwa house girl hutakiwi kufanikiwa kimaisha ukawa tajiri. Kuna wazulumati duniani kuliko matajiri au masikini atakudhulumu nn cha maana?
Kipofu wewe hujui music industey inavyofanya kazi.Maswali mazuri sana kauliza sema tu na wewe umepeleka akili likizo au umezikodisha huwezi yatazama mambo katika logic yake.
Niambie mambo gani yaliibuka baada ya kifo cha MangweaKweli tena tujifunze kusikiliza kabla ya kuhukumu. Japo upande mwingine haiingii kabisa akilini kuwa mtu wa aina ya Rose aliwekwa chini ya udhalimu huu pasipo hiyari yake na kwamba akakosa kabisa msaada wa kujinasua eti. Huyu Nathan ni nani hadi aweze kurudisha utumwa karne hii, ana serikali yake?
Rose Muhando ndiye aliyekuwa akimhudumia mchumba huyu mpya kwani alikuwa na hali duni kifedha. Rose alifikia hatua ya kumjengea nyumba kwao kwa wazazi wa mchumba wake huyu mchumba wake. Kama wahenga wasemavyo bora umfadhili mbuzi utakula mchuzi Rose alimfumania mchumba huyu mpya na mwanafunzi wa shule laivu bila chenga.
Rose Muhando alichanyikiwa na akajikuta amerudi tena na kuangukia kwenye penzi la meneja wake Nathan ambaye ni mme wa mtu.
Hawajui tu, kwanza tajiri hana "namuachia Mungu"atakula na wewe sahani moja. Masikini ndo wanamuachia Mungu.Shangaa wewe my dear, yaan tajiri hajawahi kuridhika hata siku moja, sijui watu huwachukuliaje wengine.
Ahsante kuna upande wa pili wasanii au waimbaji huwa hawapendi kuuzungumzia sabbu wanajua wanayoyafanya.Mkuu mimi sifahamu kitu chochote bali niliyoyaandika hapa ni maelezo ya Martha Mwaipaja ndiyo maana kwenye andiko hili jina Martha Mwaipaja limetokea kama lote, yote hii ni kwa kuwa sijafanikiwa kupandisha clip ya Martha Mwaipaja akiongea. Hivyo kama kuna sehemu pamepotoka wewe jazia tu usipate taabu.
Umesema ukweli mtupu namefanya kazi na hawa waimbaji wa mziki wa injili hasa wa kike ninawafahamu wote na tabia zao atokee mmoja hapa abishe nitaanika kila upumbavu ambao huwa wanafanya sema Neema tu ya Mungu inatufanya tuliyo nyuma ya umaarufu wa majina yao tukae kimya.SIO kweli.
Ni kweli kabisa Nathan alikuwa Menaja wake.
Kama ni hivyo amewezaje kuwa magari mengi na majumba? Kama sio mafanikio kutoka kwa meneja wake?
.
Rose alishiba kiburi.
Tunaomjua Rose hakuwa ameokoka.
Unajua wakati yupo kwaya ya Chimuli Rose Mhando alikuwa anafanya kazi za house girl?
Alipoinuka Kimusiki hakukumbuka alipo toka.
Hata kanisa alilokuwa anasali alikuja kuhama.
Huyu Nathan watu wanamchukulia poa tu. Ni matajiri wa kutisha hapa dodoma. Hapa dodoma ukisema unapesa unajiita mimi ni maluganji. Mwaluganji ni baba yake Nathan ambaye wakati huo alikuwa ni mtu tajiri sana. sasa Nathan si mtu wa kumdhurumu Rose Mhando.
Mwaipaja msiteteane kwa ujinga ujinga. Bila Msama na hawa akina Nathani wahindi wangewafanya vibaya sana. Wakina Nathani na kina Msama wamejitolea kuwatoa katika makucha ya wahindi wa kariakoo leo mnasema walikuwa wanawaibia.
Tutawasikia sana mkiweweseka. Rose maisha haya kwenda kombo na kutumia dawa au pombe au kufirisika yalianza muda mrefu sana Je wewe Mwaipaja ulimsaidia nini?
Wengi wenu mlikuwa mkimkwepa ili msije mkafananishwa naye leo mnajifanya mtetezi wake shame!
Rose Mhando yaliyomkuta yamemkuta atarejea tena kwa nguvu mpya na ujasiri wa Bwana.
Mwaipaja umefanya kosa kubwa kutaja hadhalani mambo ya mtu binafsi (Personal) wewe ni nani?. Wewe ya kwako ni yapi? Tunajua waimbaji wa Injili maarufu wengi wenu mmeachika na waliobaki ndoa zao ziko hoi kabisa.
Una hakika.? Mkuu. Unaweza kututhibitishia hilo? Usisahu kuna watu wanawajua hao watu kuliko wewe unavyowafahamu kupitia hii mitandao ya kijamii.Yes, baada ya kumuingiza kwenye madawa unahisi angekua tena yule Rose wa zamani? hayo yote uliyoyasema ni matokeo ya madawa ya kulevya aliyokua anapewa na huyo Nathan.
Hapo hawezi kuchomoka.
Kwa hiyo wewe unaewajua unataka kututhibitishia kua Rose hatumii madawa?Una hakika.? Mkuu. Unaweza kututhibitishia hilo? Usisahu kuna watu wanawajua hao watu kuliko wewe unavyowafahamu kupitia hii mitandao ya kijamii.
Nimekuuliza una hakika.! Unawafahamu,? Najua mapenzi hupofusha najua binafsi unaumizwa na hali ya Rose nikuhakikishie sio peke yako tuko wengi sana tunao umizwa na ile hali.Kwa hiyo wewe unaewajua unataka kututhibitishia kua Rose hatumii madawa?
Ina maana Rose alikuwa akimuheshimu huyo Nathan kuliko Mungu wake na kama kuwa na Nathan ilikuwa ni kosa je,vipi alivyomfumania huyo mchumba wake ilimbidi arudi kwa Nathan....
Lengo la aliyetoa story ni kumuonesha Rose kama ni mtu aliyeonewa kana kwamba alikuwa hana akili na utashi wa kiroho kumuongoza.. Inabidi wakubali kuw a ROSE KAMA ROSE NAYE ALITELEZA ..hii itamsaidia kutoka huko, Kama Daudi aliteleza kwa kuua kwa ajili ya mwanamke je, Rose amefanya kubwa lipi hadi asisamehewe