Hofu sio lazima itolewe hadharani mkuu! Kwenye sehemu muafaka, yeye afoke kama anavyojua lakini viongozi wake awape stahi zao!.
Nadhani utofauti wangu na wewe katika hili ni kuwa ni sehemu gani hasa hiyo hofu inafaa kujengewa! Mimi napendekeza kwenye vikao au ofisini, hapo aongee, agonge meza na aandike barua za maonyo kadri awezavyo! Wakija huku nje wanakuwa kitu kimoja.
Kufokeana hadharani kwanza kunapunguza heshima kwa wananchi, kila mwananchi anakuona ukikoromewa hadharani, kila atakalokuwa anafanya watu watasema hawezi kitu ndo maana anakoromewa kila siku na mkuu wake!
Kwani shida iko wapi, kama ukimpa waziri guidelines unazozitaka na timeframe na kumwambia akishidwa kutekeleza anafukuzwa?
Shida ya huu utaratibu unasababisha waziri anajihami ili kumfurahisha mteuzi wake! Ngoja nikupe mfano, wakati waziri wa uvuvi anateuliwa alisema akiwa kagera kuwa uvuvi haramu usipoisha anajiuzuru! Hebu nenda kanda ya ziwa uliza kuhsu huo uvuvi kama umeisha au huyo waziri kajiuzuru!
Alichokifanya ni kutoa tamko la uoga maana kateuliwa huku akiwa hana mkakati muafaka wa kumaliza uvuvi haramu!
Halafu tukiongea kuhusu kujenga hofu simaanishi kwa watu wote, namaanisha kwa viongozi hasa walio chini yake wasifanye kazi kwa hofu! Maeneo mengine hofu inaweza kutumika, najua hilo na nalitambua. Mfano kumjengea jambazi hofu ni njia mojawapo ya kumshinda!
Hofu tunayoijadili hapa ni tofauti kidogo.