MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Waswahili walimenya kwamba mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Huu ndiyo ukweli wenyewe kwamba Mama anajitahidi tu kusimamia kua katika utawala wake haki inatendeka.
Ikitokea wewe umetuhumiwa kufanya tukio flani hiyo ni juu yako wewe, serikali inachosimamia ni kusisitiza haki itendeke kwa kila mtu ila haiwezi kamwe kuingilia uamuzi wa mahakama ambayo ni mhimili mwingine kabisa. Kama ulitenda kosa utahukumiwa kwa stahiki yake, kama hukutenda basi utahukumiwa hivyo hivyo. Serikali kazi yake ni kusisitiza utawala bora na wa sheria.
Mambo ya kusema kua Rais ametia mkono wake kuhusu kukamatwa kwa flani flani eti kwa sababu alikua kiongozi ni maneno yaliyokosa staha kwa kiongozi wa nchi. Kama ulikosa wewe basi hiyo ni juu yako na mzigo wako, kamwe serikali haiwezi kuhusika na wewe. Haki yako iko mahakamani kama inavyoelekeza katiba ya nchi.
Kuhusu Mama kuhojiwa na BBC Kisha kutoa majibu kuhusu shauri la Mhe Mbowe na wenzake, alivyojibu ndiyo anavyojua yeye,ndizo taarifa alizopewa na vyombo husika, kama vyombo havikumpa ukweli basi mahakama itathibisha. Pia kuhusu suala la Sabaya serikali inahusikaje na matendo yake ya kinyume na sheria? Mnataka imbebe mtu anayevunja sheria? Kila mtu atabeba mzigo wake na atahukumiwa nao yeye. Hujaridhika basi kata rufaa bado utapata stahiki yako.
Tusimlaumu Mhe Rais bure kuhusu maamuzi ya mahakama, kama watakosea polisi hiyo ni wao wenyewe na makosa yao, kama atakosa DPP huyu ni yeye na weledi wake, kama itakosa mahakama basi ni yenyewe na mapungufu yake. Rais hana mamlaka na kutoa maamuzi ya kesi ya mtuhumiwa yeyote, anayo mamlaka ya kutoa vibali vya kusamehe wafungue waliokwisha hukumiwa chini ya katiba ya nchi kupitia bosi ya PAROLE.