Marumo watangaza kiingilio bure mechi yao ya marudiano dhidi ya Yanga

Hao jamaa karibia mechi zao zote utaratibu ni huo huo ila mashabiki uwanjani hawafiki hata 1000, hiyo timu kwa South Africa haina mashabiki wengi ni kama Dodoma fc au Namungo tu
 
Natamani Kila mtanzania angejua hili. Mana kujua kitu kama hiki ni haki yake kama mtanzania
 
Timu za Tanzania zijifunze Simba na Wydad waliwaza mapato makubwa matokeo yake wakapata mashabiki wachache
 
Hao dawa Yao ni kuwasaka dk 30 za mwanzo mwe mmeshawapiga hata kimoja cha kuwavuruga , alaf mnakuwa mnavizia uzuri mbio za tuisila na mayele sio mchoyo lazima watoboke
Nimwombe Mayele asiwe mchoyo kuna nafasi nyingi sana Yanga wanakosa kwa uchoyo wake anataka afunge yeye tu na Azizi ki anapoteza sana mipira
 
Ingekuwa hiyo inasumbua basi Simba ingekula 7 kule Wydad. Yanga inagombania kufungwa 3-1 ili isonge final. Eti Diara,Baca,Job, Lumalisa, Djuma Shaban, Mwamnyeto, Bangala Aucho,waruhusu goli 3 ndani ya dk 90 na huku akina Mayele,Musonda,Aziz Key [emoji360] , Mudathil wale, Morroco,Kisinda dk 90 washindwe tupia goli 1. Labda wawe wagonjwa wote
 
 
Kwahiyo mchawi nauli tu hadi kwa madiba😅
 
Yanga inawachezaji wengi wenye uzoefu na mechi za aina hiyo. Hivyo usitegemee kama watatetereka hata kama uwanja utajaa mashabiki walioingia bure.

Mimi macho na akili yangu yote ipo kwenye plan ya Kocha Nabi. Je, atapanga kikosi cha aina gani? Natamani kuona siku hiyo timu ikijaza mabeki na viungo wengi! Halafu na mshambuliaji mmoja tu (Mayele) pale mbele. Yaani kama alivyofanya tu kule Nigeria dhidi ya Rivers United.
 
Mwaka huu Kolos watashabikia timu kibao hadi zitafika milioni! Kweli Simba imelitia aibu sana Taifa hata kombe la mbuzi hamna? Kwanini kolokoloni Mvua msingezianza Tangu mwanzo wa msimu? Mmeshtuka kumekucha!! Hii ndio shida ya kubadilisha mganga katikati ya msimu!!

Huku kwetu Buza Kwa Mpalanger makolo wamesahau timu yao nimeona wamejigawa, wengine sasa ni mashabiki wa Moro United, Pamba ya Mwanza, Wydad, Raja Athletic, Al Hilal, Singapore Big Stars, River United , Marumo, wengine sasa ni Man City dam dam na wengine Arsenal!

Sasa Kuna wale Kolos wanaosubiri Yanga iingie fainali washabikie mpinzani wa Yanga!

Kolos endeleeni kufa kiume!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…