Watu wengi hawajaipenda series ya
Ms.Marvel Kwamba imekaa kitoto hasa kwakua zimetoka wakati mmoja na Series ya
The Boys, ukilinganisha na The boys utaaona ni ya hovyo kweli maana ipo genre ya Teen na PG 13. Binafsi mimi nimeipenda story yake kwakua hii story yake inaunganisha muvi nyingi zijazo. Eleweni kwamba kama mtu hatatazama series hii basi hataweza kuelewa
Captain Marvel 2,
Shang Chi 2 na series ya Secret Invasion.... Nitaelezea kadri nilivyoelewa hii series na theory yangu juu ya Muvi zijazo.
View attachment 2279241
Let's roll....
Inhumans ni specie ya Superhuman ambao makazi yao ni Mwezini
/Attilan, mtu akifikisha miaka fulani hupitishwa kwenye Process fulani inaitwa
Terrigenesis ambapo kijana anawekewa kitu kinaitwa
Terrigen Mist .Lakini kuna Inhumans wengine wamepata nguvu bila kuwekewa hizo Terigen Mist... Hicho ndio kinatoa nguvu zao. Mfalme wa Inhumans anaitwa
Blackngar Boltagon (Black Bolt) ambae sauti yake inaweza kuharibu kila kitu. Hopefully mlimuona kwenye Multiverse of madness, Ilinibidi niangalie Season ya Inhumans maana nilikua sijaitazama tofauti na Agents of shield.
Captain marvel ni kundi linaloundwa na superhero kadhaa wengi wakiwa wa kiume (kama sijasahau ) members wake ni
Mar-Vell, Monica Rambeau, Genis-Vell, Phyla-Vell, Khn'nr, Noh-Varr na
Carol Danvers. Katika kundi hili ni Monica na Carol ndio wenye asili ya duniani/Human Race waliobaki hapo Kree race. Sasa hawa superhero wengi wamepata nguvu kwa kutumia Technology za Kree au Genetic modification kutoka hukohuko Kree.
Ms Marvel...
Kama tulivyoona kwamba kundi la Captain marvel liliundwa zaidi na wanaume, bali pia kundi hili la Ms marvel ni kundi la superhero wa kike ambao walipata nguvu kupitia Tech's za Kree. Kundi hili linaundwa na Carol Danvers,
Kamala Khan, Sharon Ventura na Karla Sofen.
Kamala Khan ni race ya Inhuman ambapo nguvu zake ni kurefusha baadhi ya viungo vyake kama shingo,miguu,mikono nk, anaweza kuukuza mwili wake na kuufanya uwe mdogo kama ant man au anaweza kujikondesha kama karatasi, anaweza kujibadirisha kua mtu mwingine kama Skrulls, anaweza kubadirisha umbo lake na kutengeneza umbo lolote kama vile Venom
Sasa...
Kwenye Series imeonyeshwa amevaa bracelet mkononi toka kwa bibi yake ambae anaiita
Bangle ambapo inamuwezesha kuwa na uwezo huo nilioutaja hapo juu. Kamala asili yake kwenye Comics ni Inhumans ila kwenye Series hawajaonyesha kama ni inhumans...Ila kwenye Episode 2 wakati Kamala anafanya majaribu ya nguvu zake kwa kutumia ile bangel rafiki yake
Bruno alimwambia kwamba inaonyesha kua nguvu zake hazitoki kwenye Bangle bali inatoka ndani ya mwili wake so hiyo inatutaarifu kua Kamala ana nguvu zake tayari ila hazitoki kwenye bangle kama nilivyosema Kamala ni Inhuman.
Wakuu natumaini mnajua kua Kamala Khan atakuwepo kwenye muvi ya Captain Marvel 2, hivi mlishswahi kujiuliza kwanini Caro Danvers alikua kwenye Post Credit ya Shang Chi wakichunguza zile rings.?? Hapo ndio kuna connection haswa... Haikutokea bahati mbaya Carol kuwepo pale .
Kwenye flashback Episode 3 miaka ya 1940s ilionyesha watu wapo kweye pango wanatafuta hiyo bangle wakaikuta kwenye mtu mwenye mkono wa Blue ambae hatukuona sura yake...Na kubwa zaidi wale watu walikua wamesimama kwenye alama/nembo kama za Bendera ya T
en Rings. Nadhani mnaifahamu.
View attachment 2279240
View attachment 2279242
Sasa inafahamika kwamba kwenye Marvel Universe viumbe wenye rangi ya blue ni Kree, so inawezekana mkono wa mtu huyo ni Kree.
Katika kundi la Captains Marvel kuna mtu anaitwa Mar-Vell , Mar-Vell jina lake halisi ni
Walter Lawson ambae kwenye muvi ya Captain Marvel 2019 walimbadiri kua mwanamke na kumuita Dr. Wendy Lawson au Supreme Inteligence
Mar-Vell alikua anatumia kifaa kinachoitwa Universal Beam ambacho kilimuwezesha kua na nguvu za kukontrol usumaku, kupaa, speed nk kifaa hichoalikibadirisha na kuwa anakivaa mkononi akakiita
Nega Band.
So kama kwenye series wameonyesha Bangle anayovaa Kamala ilitolewa kwenye kiumbe chenye rangi ya blue ambacho naamini ni kree basi nahisi pia hiyo Bangle ndio hiyo NegaBand aliyokua anaitumia Walter Lawson.
So kuna uhusiano mkubwa kati ya Bangle ya Kamala na Rings za Shang Chi ndio maana Carol Danvers alikueepo kwenye Post Credit scene.
View attachment 2279239
Series bado inaendelea ngoja tuone itatuonyesha nini hasa ikiisha, series haipo bomba kivile ila story yake tu inavutia coz inaunganisha na muvi zijazo so vumilieni muiangalie msiwe kama yule jamaa aliyekua anaulizia kuhusu watoto wa Wanda.
Kama sijaeleweka ulizeni wenye maswali.
I'm happy to Comply!
Cc
Dinazarde Dream Queen Marc Spector Jorge WIP Kimura_shinji thephilanthropist bravocharlie