Mary Chatanda: Sheria kali itungwe kupambana na Ushoga, ikiwezekana wahasiwe

Mary Chatanda: Sheria kali itungwe kupambana na Ushoga, ikiwezekana wahasiwe

Yaani leo ilitakiwa iwe siku ya mjadala kitaifa, lakini jasiri haachi asili ametafuta upenyo ili afanye shughuli
Watanzania tunapenda sherehe. Kila shughuli lazima ifanywe sherehe. Ujamaa umetuathiri sana.

Hela nyingi inatumika... Namna nyingine ya upigaji. Kuna mtu anatumia hii shughuli kula kwa urefu wa kamba yake.
 
Haya naisha hayapo fair kabisa...badala yakuomboleza kwa aliepita tunasheherekea kinyume. ..mola asamehe zambi zao...life is not fair at all
 
Mimi huyu mama! Sikuwahi kumwelewa saaaana marehemu ila kumbe nlikosea siku kama ya jana alilala yule baba usingizi wa milele, mama akatangaza katika sauti ambayo unaona kabisa ameguswa! Ila mbona amekuwa tofauti? Sherehe utafikiri anasema yule mshenzi tushamkomesha?
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kwenye Sherehe ya Kilele cha Miaka Miwili ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita iliyoandaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT) katika Uwanja wa Uhuru Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Machi, 2023.


Bila shaka na bawacha watakuwa wamejitokezaa . Mungu mbariki raisi wetu SAMIA atuongoze hivi hiviiii. Amen
 
Nchi ya TEUZI, TENGUZI, MICHONGO, UNAFIKI, UCHAWA na SHUGHULI Kama Wazaramo.
 
Ku
Uongozi wa mirathinunachangamoto zakem

Hajiamini kila akitimiza mwakaaanafatnya sherehe.
Kubalini yaishe Magu hatarudi tena huu ni wivu, mlimkubali akiwa makamu, ni haki yake kikatiba kuwa Rais.

Mbona kwa Magu mlikuwa mnaimba mapambio kila baada ya mwaka.

Msipokubaliana na hali ilivyo, Sonona itawamaliza.
 
Ccm wanachoweza ni kupongezana kqenyw ujinga na upuuzi,masuala ya msingi ya maendeleo ya wananchi hawawezi kuyasemea.
 
Mimi huyu mama! Sikuwahi kumwelewa saaaana marehemu ila kumbe nlikosea siku kama ya jana alilala yule baba usingizi wa milele, mama akatangaza katika sauti ambayo unaona kabisa ameguswa! Ila mbona amekuwa tofauti? Sherehe utafikiri anasema yule mshenzi tushamkomesha?
Hivi misiba ya ndugu zenu huwa mnasikitika miaka yote?
Mambo mengine mnafanya yaonekane mkubwa sana
 
Namsikia akimshauri Mama Samia awahasi mashoga!
 
Bawacha ni Wing mpya ya UWT

Mbowe anajua na Wadanganyika Tunajua.
 
Mnyonge mnyongeni Iakini haki yake mpeni, kongole kwa mama umejenga barabara nyingi za mitaa na mitalo ya maji machafu na kuweka mipango miji vizuri kuliko awamu zote, kwa sasa huwezi kutofautisha vijiji na miji.

Pia unajitahidi kutekeleza miradi mingi ya maji mijini hadi vijijini, kwa Sasa tutakuwa tunaoga maji ya mvua hadi vijiji.

Naona umeamua kuweka rami hadi vijijini hama hakika kanda ya ziwa ni Neema.

Bila kusahau umejitahidi sana kutoa ajira kwa vijana na kupandisha madaraja kwa watumishi wa umma kuliko awamu iliyopita.

CHANGAMOTO
Nidhamu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma ipo chini sana kuliko awamu iliyopita wamerudia tabia yao ya kufanya kazi kwa kujisikia, kuwa Miungu watu na wala rushwa.

Mfumuko wa bei kwenye bidhaa muhimu hasa chakula na mafuta unatukosesha raha hapo ndipo unapoona hela haina thamani.

Wajasiriamali wadogo wadogo hasa wamachinga kupelekwa nje ya miji na sehemu za katikati za miji kupewa mabwenyenye huo ni ukatili wa kiuchumi. Mipango miji wanapopanga miji basi hawa watu wawafikilie kuwaachia maeneo ya wazi.

Mmomonyoko wa maadili kwa vijana unatisha hii mikataba tunayoingia na wahisani tusipoiangalia kwa jicho la mbali hawa vijana watakuwa janga la taifa kwa Sasa viashiria vibaya vipo kwenye mashule.
 
Back
Top Bottom