GE2025 Mary Nagu achukua fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Hanang

GE2025 Mary Nagu achukua fomu ya kuwania Ubunge jimbo la Hanang

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Mwanasiasa mkongwe na mzoefu, Dkt. Mary Michael Nagu, amejiunga rasmi katika mchakato wa uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuchukua fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Hanang kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Dkt. Nagu, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Hanang kwa vipindi kadhaa na pia kuhudumu kama Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amesema amerudi tena kuomba ridhaa ya wananchi kupitia chama chake ili kuendeleza kasi ya maendeleo na kulinda maslahi ya wananchi wa Hanang.

mary nagu.png
 
Halafu utasikia vijana wanaitwa wazembe hawajiajiri, Mama Marry Nagu namsikia toka miaka ya 90 huko mpaka leo yeye hajiajiri tu.

Nangu nyau - ndani ya viunga vya Tehrani.
vijana 1800 wameajiriwa tra, 3000 wako jwtz, 2000 wako police, 12000 manesi na madaktari, wachieni vijana wakomavu watoe mchango, morani bila ngariba haliwezi kuwa jando
 
Duh mi tokea nipo mdogodogo naenda kule Oysterbay kuwatembelea ndugu zangu alikua kiongozi maana ni jirani yao sasa hv tena umri wangu umesogea bado anautaka tena,kweli njaa haina baunsa.
kwahiyo unadhani ananjaa? we vipi huwezi wakilisha watu una njaa utaishia kuwa chawa
 
Back
Top Bottom