Watoto wako kwao, ukiona wanakufanyia fujo ondoka wewe, usepe zako. Kwanini uanze kuwafinya, kuwakazia macho sijui kuwachapa, wanakuhusu nini watoto wa wenzio?
Mtoto kuja kucheza au kufanya fujo kwako ni "friendly gesture" na kukukaribisha na kukufahamisha "instictively" kuwa "feel free in our territory". Elewa kuwa bado hawana upeo ulio nao wewe kwa umri wako na hiyo ya kimchezo mchezo ndio upeo wao ulipo, Hawana cha kuogopa au kuwa na hofu na wewe mpaka wahisi au wuwatie hofu.
Kumpiga mtoto, kumbadilishia hisia, kumkazia macho na au hata kutoonesha upendo kwake ni udhaifu kwa upande wako sio upande wa watoto na ufanyapo hivyo umeshajenga uadui na hyo mtoto maisha wa kutoweza kuwa karibu nawe tena, ni nani atataka kuwa karibu na adui ambae unamkaribisha kwako mcheze, mfurahi anakuumiza?
Hivi hamuelewi kuwa ni haki ya mtoto kucheza na ni kumjenga ki akili na kimawazo kumuachia ajisikie huru kwao? Boundaries na watoto haziwekwi kwa ukali au kukurupuka zinawekwa kwa kusemeshwa kirafiki na tone nzuri kama vile unaongea na mtu mzima mwenzio unaempenda. Mtoto atajifunza haraka na kukuelewa haraka na kuwa rafiki wako wa maisha ukifanya hivyo.
Ni mijitu mijinga inayokwenda nyumba za watu ikakuta watoto wanafanya utundu kwa kuwakaribisha, ki namna yaoa, ikaanza kuwashambilia. Si umite mwenyeji wako pembeni umueleze kuhusu wanawe na awaondoe hapo karibu yako kwaani hukuja kwa ajili ya kucheza na watoto, mwenyeji wako atakuelewa na atafahamu namna ya kuwazuia watoto.
Na walezi wanatakiwa waelewe kuwa ukimualika mtu, hujamualika kuja kucheza na wanao, kwa hiyo unawafahamisha kabisa watoto, kuwa kunakuja wageni na mkisha salimia mkae mbali na wageni, hususan wanaowazidi umri. Na wakija na watoto wenzenu, mtatumia, sehemu hii kuchezza nao, mtawaonesha kabisa sehemu watakayokuwa na wenzao.
Yote ni malezi tu.
Tuna safari ndefu sana ya kwenda Tanzania.