Gucci gang
JF-Expert Member
- Jan 7, 2018
- 2,682
- 5,277
Kuna mtoto wa ndugu huko kwao alidondosha simu yangu ilikua chaji alikula nakozi ya mgongo mpaka sahivi eneo la socket akipita baadae ya miezi mitatu analia mwenyewe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Sipendi watoto watundu watundu, kuna siku nipo hosp. Kuna mtoto kama miaka 6 hivi akaja kavamia Mkoba anataka kuufungua nikamshika mkono kwa upole, nikauminya ule mkono huku namwongelesha nikimkazia macho, “Unaitwa nani? Ninachapaaaaa! Kakae pale utulie, nilimminya kweli kweli na hakurudi tena kwangu.
Kwaamba kyoki ... Kuwashune na nndo? Kukundikyo kuwaolote mbiri yo kiseen wawa wawaHawajafunywa na vimndo hao....pole yao
Wewe ni roll model wangu. Silei watoto kama mayai. Mwanangu huwa anawasimulia wenzake kipigo anachokutana nacho.Last Jumamosi nilipata mualiko kumtembelea Sister Home kwake Mikocheni. Nilienda na Mke Wangu na Mtoto wetu mmoja wa miaka 4.5
Saa nne tulikuwa tumefika home maana tuliambiwa siku hiyo hata kinywa tukafungulie pale na jioni tukifungie pale pale. Waswahili wanasema mtu hakatai wito.
Sister ana watoto wawili, mmoja miaka 6 na mwingine 4. Tulianza kupata changamoto mapema sana baada ya kutia tu mguu pale home. Watoto wake wanalilia simu. Nikawa nawaza hii iPhone yangu nimpe mtoto achezee kweli?
Basi yule wa miaka minne akawa analia balaa anajirusha huko na kule akitaka apewe simu acheze game. Sister anacheka tu na kusema "We Junior usimsumbue Uncle bwana, basi chukua hii yangu huku ana mpeti peti" wallah nilikuwa napatwa na hasira sana.
Akaendelea kusema simu zao mle ndani zote zimeshapasuliwa vioo mara kadhaa sababu ya watoto kugombania. Wakati huo tena yule mtoto anamvuta mke wangu nywele nyuma ya kiti.
Sister anasema tu "We xxx mwache Aunt nitakuwa sikupi game ucheze" Yule Mtoto kuambiwa vile aliangua kilio kikubwa sana. Nikahisi wife uzalendo ulimshinda akamwasha kibao. Kumbe sivyo. Alikasirika sababu ya kuambiwa atanyimwa game.
Sister akawa anambembeleza wakati huo yule mwingine ametokea chumbani kwa Wazazi wake kavaa chupi ya sister kichwani. Mbaya zaidi kaja kwangu nimwone eti kavaa mask nimeshika hivi ni chupi astaghafilulah nikaachia kama mtu aliyeshika moto. Ndio Baba yake akaja iokota na kuipeleka tena room akisema wewe xxx acha michezo hiyo kwa uncle.
Tumeenda kula mezani yule mdogo kaanza tu kulia. Analia wanamuuliza nini anasema hataki maziwa anataka chocolate nikajiuliza hili si lilikuwa suala la kusema tu why alie?
Huyu mkubwa amesusa kula akaanza bembelezwa, akabembelezwa sana mwishowe akaitwa Dada amlishe mtoto wa miaka 6 analishwa? Tumerudi kukaa sitting room taabu zinaendelea wanakuja kunidandia mwilini wakitaka niwabebe, wakitaka tukacheze mpira, wakitaka tuimbe.
Muda huo wote sijaweza hata kukaa vizuri kuongea na wenyeji wangu. Wao wanacheka tu na kufurahi kiukweli Mtoto wangu akawa kama amepigwa na butwaa hivi anashangaa sana.
Wakaambiwa wakacheze kwenye bembea. Dada akaitwa akawasukume, wangu alienda ndani ya dk 10 akarudi hataki kwenda tena. Nadhani walimghasi na vile hajazoea shida na ugomvi.
Akina uncles wakarudi wanalia mmoja anadai kaangushwa na mwenzie na mwenzie anadai amegongwa, wakiwa wanabishana mmoja alimrushia remote control mwenzie ikamkosa. Sister akawa mkali akisema "wewe junior kesho hupandi gari yangu, utapanda ya baba" hii ndo adhabu yake eti.
Mpaka mchana nilikuwa nmeshachoka sana kukaa pale. Tunakula mezani yule jr akaanza kulia, wanamuuliza jun unalia nini anasema usingizi unamuuma, nilishangaa sana kumbe hata usingizi una maumivu, ikabidi achukuliwe akalazwe na mwenzie naye akawa ameinama kwenye meza kalala anaulizwa naye anasema usingizi akabebwa akalazwe, huo ni mchana.
Mpaka jioni nilishachoka kabisa na sikuwa na hamu, mke wangu alikuwa ametulia kimya na mtoto wangu amejituliza pembeni yangu, kiunyonge akitaka tuondoke.
Jumapili tumekaa sebuleni mara Mtoto wangu wa miaka 4.5 akaanza kulia nikamuuliza kulikoni tena? Akanijibu usingizi.[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]kama Mama yake asingeniwahi nadhani tungekuwa tumempeleka hospital amelazwa mashavu yamepasuka. Nlianza ona emeingiwa na pepo.
Nlikuja muuliza toka lini usingizi umekuwa ugonjwa kwake au maumivu? Nilimuuliza siku zote hufanyaje akajibu huenda chumbani akapanda kitandani akalala. Then swali langu likawa leo amepatwa na nini? Akaomba msamaha. Sorry Daddy!
Nikashusha pumzi. Nika rewind matukio yooooote ya Jumamosi kwa sister it was like a little hell. Na mtoto wangu alitaka eti aige that life. Nikashangaa wenzangu wanaleaje Watoto, nami nakosea wapi?
Well, watoto wangu tunacheza, tunataniana, tunaimba n.k but kwa wakati. Na hawashiki simu yangu kuchezea nakaa mpaka mwezi sisikii wanalia. Mfano huyu wa miaka 6 anaanzaje kulia? Huyu wa miaka 4 anaweza ongea why alie?
Siwezi enda kwa sister tena na hata home simwaliki kuja na watoto wake. Acha tuwe tunaonana juu kwa juu. Sitaki tuje kutafutiana lawama baadaye. Sitaki undugu lawama. Kama ameamua kufuga tushetani akae nato peke yake. Sitaki kabisa.
Aiseee nimekulia kwenye Hilo jicho !bi mkubwa wangu akikukata Hilo moja tu anakua kakueleza kila kitu!usiombe ndio ujichetue mbele ya mgeni au uende ugenini ujitie una maruhani ni jicho moja tu unafyata!Kweli it's a lost art wazazi wa sasa hawana hii artAnafanyajeee!?? Hahahaha duh! Basi tu..
Huenda unasura fulani hivi ya upole... Jifunze telecommunication... Kuna uso au jicho huwa nilikilitupa mita 49 dogo anajua hii hapana.. na kuna lile la usifanye kitu bila kuuliza na la approval...
Nitaanza kuendesha warsha juu ya hili... Its a lost art.
ha haaaaaMkuu umenikumbusha miaka ya 90, nilienda kwa baba mdogo. Kuna mtoto mwenye umri ambao anaweza kutembea.
Kimbembe kilianza alipoanza kunyweshwa uji.
Akizingua anaambiwa tema mate tumpige mgeni, anatema mate kwenye kiganja chake, kisha anakuja kwangu anaipiga plus kuniachia mate yake. Mara ya kwanza sikuelewa kilichotokea, nikahisi naota. Alivyorudia mara ya pili nilimuachia konzi ambalo hadi leo hajawahi kulisahau na nikajiondokea zangu
Cha muhimu kila mtu akae nyumbani kwake na maujinga yake
Watoto wana akili sana, mimi kuna watu nimewapa hifadhi kwa muda, sasa wana mtoto wao wa kike ana miaka 6, na mimi nna wa kike ana miaka 7. Niko friendly sana kwa mwanangu ila ni mkali likija suala la ujinga ujinga sitak sema nwanangu ni easy kuiga ujinga wa wengine.🤣🤣🤣🤣🤣🤣aisee nina hako katabia pia huwa nadeal nao ki silencer na huwa hawasogei tena na hapo ndio utajua watoto wana akili sana ila huwa wanakujaribu kwanza kutest mitambo wakiona unawachekea wanaongeza utundu
Watoto wengine ni wa dawa[emoji1787]Hapo wazazi wanaogopa kususiwa!
Watoto washajua wazazi wao wanajikomba.
Biblia inasema 'mtoto usimnyimwe fimbo'Watoto kama hao inabidi warukie konzi tu...
Rudia kusoma tena, huyo jamaa alivyoandika inaonyesha kabisa maisha ya dada yake ni mazuri kabisa (probably zaidi ya maisha yake yeye), sema yupo concerned na malezi ya wapwa zake, of which it is true kwa mjibu wa aliyoyaandika!All I got from this post ni dharau na kujiona Upo kwenye class tofauti sana na Dada yako kiasi cha kupaita Jehanum!
Ujinga na Ulimbukeni
Ipo siku atatoka kavaa kondom kama soksiJuniyaa kaja na chupi ya mama yake kichwani
Dah... Mama Rashidi katisha...Nimekumbuka mtoto wa sister alikuwa ana miaka ya kutembea na baby walker yaan alikuwa atulii na kapita huku katokea huku na sister alikuwa hamchapi basi kerooo
Sasa siku hiyo kaletwa nyumbani tulikuwa na paka mbabe hatari jike tulimpachika jina mama rashidi
Dogo akaanza vurugu zake kupita huku kashika paka mkia na kuuvuta basi paka aka mama rashidi aliubana mkono wake kwa kucha za miguu na mikono akampa mn'gato huku kaubana mkono ndo nashtuka dogo anapiga yowe huku anatuangalia wajomba zake tutoe msaada
Paka Mama rashdi alivyofanya uhalifu akakakimbia spidi kuondoka eneo la tukio yaan hapo dogo utundu ukamuisha akalia sana mpaka akanyamaza hakuna aliembembeleza
Sasa baadae nimejisahau naona dogo kapiga yowe zito nashtuka kuna nini kumbe kamuona paka anarudi zake ndani
Hapo tumenyweshwa chai ya rangi lazimaJuniyaa kaja na chupi ya mama yake kichwani
Hawa watoto wanaweza ati hata kyupi iwe na tobo anaileta tu😂😂Hapo tumenyweshwa chai ya rangi lazima
😂😂😂😂😂aisee niache mimi kha, kwani wanandoa wanatumia condom?Ipo siku atatoka kavaa kondom kama soksi