Masahihisho: Kinachosherehekewa ni Uhuru wa Tanganyika siyo Tanzania Bara. Hatutavumilia upotoshaji

Habari P,
Tenga kati ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwako na adhimisho la kuzaliwa kwako.
Sherehe ya kuzaliwa ni ile siku mtoto amezaliwa, hivyo siku ya uhuru wa Tanganyika ni ile siku ya kupata uhuru.

Tanganyika ilidumu toka Desemba 9, 1961-April 26, 1964, takriban miaka miwili na miezi 4, na kugeuka Tanzania, hivyo maadhimisho yote ya uhuru toka hiyo 1964 ni maadhimisho ya uhuru wa Tanzania na sio Tanganyika. Uhuru ni wa Tanganyika na maadhimisho ni ya kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika, ila yanaadhimishwa na Tanzania, hivyo it's Tanzanian national day!.
P
 
Tanzania bara imetokea wapi?
Nani aliunda hilo jina Tanzania bara?
Kwanini wanaogopa kutamka neno Tanganyika?
 
Mkuu huu uongo wako unaouandika humu ni kwa manufaa ya nani ?
 
Mkuu Paskali angalia kwenye mashindano ya CECAFA under 18 Tanzania imecheza na Zanzibari. Sasa huku tunakoelekea sio kuzuri sababu upande mmoja haukaripiwi umeachwa ufanye mambo yake wakati upande mwingine huu wa bara umejaa wanafiki na wachumia tumbo
 
Zanzibar ni Nchi
 
Tanganyika iko hai
 
Mtikila aliangushwa na watanzania wote. Tusinyoosheane vidole.
 
Mtikila aliangushwa na watanzania wote. Tusinyoosheane vidole.
Ukiona watu wanasema mtu hawezi kuwa mkubwa kuliko chama cha siasa basi ujue hapo upo mahali pasipo sahihi.

Yaani watu hawaamini mawazo ya mtu mmoja kuwa yanaweza kuwa sahihi kuliko ya taasisi (chama). Na kwenye kauli hizi za mtu kutokua mkubwa kuliko chama, hapa vyama vya upinzani huungana mkono na CCM, wote huwa na msimamo huo.

Mtu akitoa mawazo tofauti na ya taasisi, piga chini. Hawezi kupata umaarufu kuliko chama
 
Hii ni kwa sababu Mwl Nyerere na viongozi wa TANU walikuwa Watanganyika na waliikomboa Tanganyika na wala si nchi nyingine yoyote ile.
Duh!!

Kuna watu wamejichomeka kwenye hii sherehe!!! Bado na hapa wanataka gawio la sherehe!!! Hii ni too much
 


Ni nani leo hii atakubali kujipanga hivyo kwenye foleni bila bunduki pembeni
 
Tanganyika a.k.a Tanzania Bara. The United Kingdom a.k.a Britain. Wapi tatizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…