kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Kama hutaona kwamba mfumo wa mahakama umeachwa uwe huru,na kwamba serikali ikiamua huwezi kushinda kesi kirahisi,basi wewe ni wa kuonewa huruma sana.
Mimi nilikuwa naipenda CDM na nimewahi kupata kesi za kubambikiwa na jamhuri.Najua jinsi waendesha mashitaka walivyo mafundi wa kutengeneza ushahidi wa uongo na ukatiwa hatiani hata kama hujafanya kosa.
Waendesha mashitaka ambao ndiyo serikali,ndio walioamua kesi iisheje kwa kutoipa tena uzito. Na hii haijatokea bahati mbaya.
Msipotambua kuwa hii ni kwa sababu ya misimamo ya mama,hamtakuwa tofauti na punda

Pamoja na yote yanayoendelea kuhusu Mdude, ambayo nisingependa kuyarudia hapa, kinachopaswa kufahamika ni kwamba Mdude Nyagali alitolewa gerezani baada ya kuishinda serikali ya Tanzania Mahakamani.
Hakutolewa kwa Msamaha wa Rais wala hakutolewa kwa Huruma ya Mtu yeyote yule, alishinda Kesi ya kubambikwa, ya uongo iliyotungwa ili kumkomoa, shukrani kwa Chama chake na Jopo la Mawakili wake wakiongozwa na Mangula.
Wale wanaotaka anyamaze kama zuzu, yaani akae tu kimya kama ndondocha wa kiarabu pamoja na unyama wote aliotendewa kuanzia kule walikoshindwa kumuua baada ya Mungu na Wazungu kuingilia kati, hadi hizi njama za madawa ya kulevya, hatukuwasikia wakikemea unyama aliotendewa, na itambulike wazi kwamba waliomtesa na ambao walitaka kumuua Mdude bado wapo na wapo madarakani, kuanzia viongozi wa juu, watekaji, polisi na wengine wengi, aliyepungua ni mmoja tu, kwahiyo tunapomkosoa Mdude kwa kauli zake tufikirie pia aliyotendewa na watu hawahawa tunaowatetea.