DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Zembwela.asubuhi leo kakumbushia kwamba ingekuwa enzi.za.hayati magufuli leo tungesikia tumbua moja ndefu kuanzia TRA longroom meneja mpaka yule aliyemsafisha kwenye press.

Kiuzoefu wafanyakazi wengi.wa.TRA si.lazima wawe Tiss ila.wanafanya kazi kwa.ukaribu.sana.na.tiss waliokuwa.assigned bandarini.

Sababu wengi huwa.wanapata.utajiri.wa.ghafla na.wa. rushwa hivyo kupelekea kujiona ni watu.wa. daraja la.juu hivyo kumiliki silaha kihalali ni.kawaida.

Ipo trend ya vijana wa.TRA walioko.sehemu.zenye pesa nyingi kumiliki silaha ni kama fashion kwao.

Kwa kuishi na wanajeshi.halisi hakuna mtu wa.jeshi.halisi anaweza kufanya aliyoyafanya Derick Junior jinajunior.tuu linaonesha penginesilaha.karithi toka kwa baba.
Kweli aiseeee!
 
Na kwa kukuthibitishia Hilo. Jioni ya Jana Muliro amewahi TBC jioni wakati ambao anaamini kwamba watu wote wamepumzika majumbani na kutumia chombo hicho kukanusha vikali uhusika wa jamaa na vyombo vya Dola. Kazi aliyokua anafanya Muliro Jana ni kuongea na media tu kuhusu Hilo tukio.

Jiulize na matukio mangapi yanayofnana na Hilo ambayo polisi wametumia nguvu kubwa namna hiyo kuiaminisha media kuwa watuhumiwa hawahusiki na vyombo vyao?

Kuna jambo unashindwa kujiuliza. Kwani Hawa watu wanaishi kwenye space au Dunia tofauti? Sio kwamba tunaishi nao na tunajua whereabouts zao, kazi zao na familia zao? Wana marafiki na watu wanaowafahamu ambao tunaishi nao? Inakuaje unakataa kumhudisha na kazi anayofanya kwamba ndio pamoja na nyege zitokanazo na pombe, ulimbikeni na mambo mengine Ndio driving force ya kufanya huo uhalifu? Au mesahau ya Afande kwenda kung'ang'ania demu Boardroom sinza huku akiwa amelewa na akamsindikiza kuzimu mlinzi? Imeahahulika? Au pale ilishindikana kucover up sababu ya defender na uniform ya polisi?

Hii inakua ngumu Kwa sababu ya attachment ya dogo na msaidizi wa namba Moja, Ili kulinda hadhi na heshima ya ofisi namba Moja. Utungwaji wa Sheria zinalonge kuwapemdelea watu wa aina Fulani madhara yake ni makubwa kwa jamii ya watu wengi! Dogo akidefend alikua kazini na kwamba jamaa alikua anaingilia majukumu yake na alifanya vile Ili kumpunguza kasi ya kufuatilia nani atapinga wakati Sheria imeweka wazi kwamba hawana jinai?
Fallen State
Ili raia wa nchi hii waweze kuondokana na madhila kama haya inahitajika kafara kubwa sana ili kukomesha upuuzi wa aina hii, bila ya hivyo waTanzania wataendelea kuumia na Mikasa ya namna hii mpaka kiama.
 
Hili ndilo la Muhimu zaidi.
Kinachotutafuna ni kwamba wenye akili na wanaoujua nini kifanyike wameingiwa na hofu na kuchagua kukaa kimya na kuwaacha wajinga wafanye watakavyo! Na kinachofanyika hapa ni wajinga wanejiinua!
 
Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi.

Tukio la kutisha lilitokea jana usiku (26.10.2024) katika klabu maarufu inayojulikana kama 1245 Lounge, Bar and Restaurant iliyopo Masaki, ambapo Afisa Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Derick Junior Lima (maarufu kama Chief Abayomi) alianzisha fujo na kujaribu kumpiga risasi Julian Bujulu baada ya kutokea sintofahamu kati ya Derick na Julian iliyosababishwa na Derick kujaribu kulazimisha kuondoka na mwanamke aliekuwa ameenda kustarehe katika Club hiyo akiambatana na Julian.

Taarifa zinaeleza zaidi kwamba Derick ni mtu mwenye mke na watoto na kwamba mwanamke anayehusishwa na ugomvi huo ni Dada yake Julian ambapo walikuwa wametoka pamoja kwenda kwenye starehe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ghasia zilianza baada ya Derick kutaka kuondoka na mwanamke huyo kwa nguvu bila kujali yupo na kina nani, jambo lililopelekea Kaka mtu kuingilia kati akizuia Dada yake kuondoka na Derick. Mzozo huo ulipopamba moto, Derick alitoa bastola akiwa na lengo la kumpiga risasi Julian lakini kwa bahati nzuri, bastola ya Derick iligoma kutoa risasi. Baada ya kushindwa kupiga risasi, kwa hasira Derick aliamua kumpiga Julian kichwani kwa kutumia kitako cha bunduki hiyo na kumsababishia majeraha makubwa.

Kamera za CCTV katika klabu hiyo zimenasa tukio zima jinsi Derick alivyotenda na kusababisha majeruhi makubwa kichwani yaliyopelekea kuwahishwa hospitali na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo amelazwa kwa matibabu zaidi.

Mpaka wakati huu, Derick Lima anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay huku uchunguzi ukiendelea. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba haki haitatendeka kutokana na uhusiano wake wa karibu na wakubwa. Mpaka sasa kuna baadhi ya “Matajiri” wa mjini ambao wamekuwa wakimtumia Derick katika kukwepa kodi na kutekeleza mambo yao haramu wamekuwa wanaendelea na jitihada kuhakikisha anatoka mikononi mwa polisi bila kuwa na kesi.

Polisi wamechukua mashine za CCTV katika Club hiyo na katika kuhakikisha mmiliki wa Club hiyo anaminywa na asitoe ushirikiano, wameachia makusudi video inayomuonyesha mmiliki huyo akifanya mapenzi na mmoja wa aliekuwa mfanyakazi wake katika moja ya ofisi za Club hiyo.

UPDATE: Polisi wamemkamata Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'
Daaah
 
Bila kujali wadhifa wake huyu ame attempt to shoot another person with a gun, haitajalisha anaitwa junior derrick mkila inavyodaiwa ni mtoto wa mstaafu naibu gavana wa benki kuu na mwajiriwa wa Mamlaka ya mapato tanzania kitengo cha customs bandarini kwenye kutoa mizigo.
haki ionekane ikitendeka pasipo kujali uwezo wake wa kifedha, kibiashara za vipodozi kariakoo au kimamlaka hii halihitaji wala kuzungushwa sana kama la afande
Hili la kuwa mtoto wa mzee Mkila haliniingii akilini,yule mzee ni muislam safi sana yeye na mke wake,hilo jina Derick ni la kikristo inawezekana vipi,mumuache mzee wa watu apumzike kustaafu kwake!
 
Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi.

Tukio la kutisha lilitokea jana usiku (26.10.2024) katika klabu maarufu inayojulikana kama 1245 Lounge, Bar and Restaurant iliyopo Masaki, ambapo Afisa Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Derick Junior Lima (maarufu kama Chief Abayomi) alianzisha fujo na kujaribu kumpiga risasi Julian Bujulu baada ya kutokea sintofahamu kati ya Derick na Julian iliyosababishwa na Derick kujaribu kulazimisha kuondoka na mwanamke aliekuwa ameenda kustarehe katika Club hiyo akiambatana na Julian.

Taarifa zinaeleza zaidi kwamba Derick ni mtu mwenye mke na watoto na kwamba mwanamke anayehusishwa na ugomvi huo ni Dada yake Julian ambapo walikuwa wametoka pamoja kwenda kwenye starehe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ghasia zilianza baada ya Derick kutaka kuondoka na mwanamke huyo kwa nguvu bila kujali yupo na kina nani, jambo lililopelekea Kaka mtu kuingilia kati akizuia Dada yake kuondoka na Derick. Mzozo huo ulipopamba moto, Derick alitoa bastola akiwa na lengo la kumpiga risasi Julian lakini kwa bahati nzuri, bastola ya Derick iligoma kutoa risasi. Baada ya kushindwa kupiga risasi, kwa hasira Derick aliamua kumpiga Julian kichwani kwa kutumia kitako cha bunduki hiyo na kumsababishia majeraha makubwa.

Kamera za CCTV katika klabu hiyo zimenasa tukio zima jinsi Derick alivyotenda na kusababisha majeruhi makubwa kichwani yaliyopelekea kuwahishwa hospitali na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo amelazwa kwa matibabu zaidi.

Mpaka wakati huu, Derick Lima anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay huku uchunguzi ukiendelea. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba haki haitatendeka kutokana na uhusiano wake wa karibu na wakubwa. Mpaka sasa kuna baadhi ya “Matajiri” wa mjini ambao wamekuwa wakimtumia Derick katika kukwepa kodi na kutekeleza mambo yao haramu wamekuwa wanaendelea na jitihada kuhakikisha anatoka mikononi mwa polisi bila kuwa na kesi.

Polisi wamechukua mashine za CCTV katika Club hiyo na katika kuhakikisha mmiliki wa Club hiyo anaminywa na asitoe ushirikiano, wameachia makusudi video inayomuonyesha mmiliki huyo akifanya mapenzi na mmoja wa aliekuwa mfanyakazi wake katika moja ya ofisi za Club hiyo.

UPDATE: Polisi wamemkamata Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'
Derick hakupaniki Bure.
Kwake yeye binafsi hajakosea alichokifanya.🥱
 
Acheni kudanganyana, nimeona komenti nyingi watu humu wakitamba kuwa wangekuwa wao wangemdhibiti huyo jamaa aliyejihami na silaha ( bastola) wangemdhibiti kwa mapigo ya ngumi.

Hiyo siyo movie ni uhalisia mbele ya macho ya wengi, mtu anapojihami na silaha kanuni zifuatazo zifuate Ili uwe Salama:-
1. Kuwa mtulivu na nyanyua mikono juu kuashiria kuwa hauna Nia ya kupigana naye.
2. Epuka kuongea maneno yenye kumfanya aamue kukushambulia kwa silaha.

3. Muombe idhini ya kuondoka kwa unyenyekevu Ili unusuru uhai wako,

4. Kubaliana na matakwa yake wakati huo ( kama mnagombania mwanamke, pesa n.k)
5. Usijaribu kuonesha Nia ya kupigana naye:

MUHIMU: kujaribu kupambana na mtu anayejihami na silaha kama huna ujuzi wa SILAHA ni kuweka dau la kucheza kamari maisha Yako.
Mtu mwenye ujuzi wa SILAHA anatambua aina ya bunduki, uwezo wake, muda ambao silaha imewekwa tayari kwa mapigo na pia ni rahisi kujua kuwa silaha si halisi ( fake)

Ni muhimu kutambua kuwa kumdhibiti mtu mwenye silaha katika umbali mfupi ( close range) inahitaji mafunzo maalumu ya Hali ya juu yanayokupa uhakika wa haraka wa kutekeleza matendo kusudiwa.

Mafunzo hayo asilimia kubwa hutolewa kwa askari wa vikosi maalumu vya kijeshi ( komandoo).

Msijaribu hata siku moja kumvamia mtu aliyejihami na silaha bila kuwa na sanaa za kimapigano, mtakufa kirahisi sana.

"Play safe, a muzzle plays death games"
Uko sahihi sana mkuu
Lakini ni lazima uangalie ni mtu wa aina gani ambaye yuko na hiyo bastola
Huyu jamaa angeuawa kwa mimi ningetafsiri kama amekufa kizembe sijui alikuwa na ulevi kiasi gani huwenda ndiyo sababu lakini kama hakuwa amelewa kiasi hicho amefanya uzembe mkubwa sana

Huyu jamaa ambaye tunaambiwa ni usalama siyo mtu makini na sijui kama ana mafunzo ya aina gani
Askari aliyefika hatua ya kumnyooshea mtuhumiwa bastola na kumpa amri huwa hakai naye karibu hata kidogo kwa sababu wana mafunzo ya kwamba kuwa karibu na mtu huyo wewe pia upo kwenye hatari zaidi

Bastola siyo ya kuogopa kiasi hiyo
Bastola ni hatari kwa sababu inaweza kufanya shambulizi mshambuliaji akiwa mbali hata mita ishirini au zaidi hiyo ni sifa kuu ya kuogopa kwa bastola
Ukiwa umeshikana na mimi au mtu yoyote na una kisu au panga hizo silaha zinaweza kuwa hatari zaidi kuliko ukiwa umeshika bastola
Huwezi kutii tii amri za chizi hujui akili zake zikoje wakati kabisa mazingira yanaruhusu kusave utakufa kwa uzembe
 
Wamiliki wengi wa silaha sahvi ni wpmbv na wjng na hawana uzoefu,mbinu za kuitumia
Naongea hivi maana nna ushahidi
Kabisa kwa nlichowahi kukiona

Ova
 
Huyo jamaa nikimuangalia pamoja na bastola yake namuona kabisa haijui sanaa ya mapigano. Angeugusa muziki wa mtu kama mimi, angekiona cha moto. Sema kakutana na ASIYEJUA mwenzake akamuonea. Dah. HASIRA
Yani huyo jamaa fala kweli kweli otakuwa ni hawa wanaume wa chips yai yani anarusha teke utadhani anacheza kwaito
 
Back
Top Bottom