Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,379
- 41,294
Hivi unawezaje kuwa na mke na watoto ukaishia club mpaka asubuhi na ukataka kubeba mwanamke uende naye na huyo mke nyumbani anafanya nini? anajuwa mume wake yuko club? najiuliza tu inawezekana vipi una family ukatoka usiku mpaka asubuhi na mke anakusubiri tu? tushukuru sisi wenye family zetu usiku ziko family mitihani kwa kweli.
Wanaumeeeeeeee
Njoweniii mjibu hoja hapa, nyie kuwezaaa...!!!
Nke umuache nyumbani ulale wima na glasi mkononi hadi asubuhi si adhabu hiyoo...!!!
Ila tuache masihara, kuna ujumbe nimeuona unasambaa ukisema, WAJANE SIO WALIOFIWA NA MUME TUU, HATA WALIOOLEWA NA WALEVI.....
Huruma kwao hakyanani, kwenye hekaheka za maisha nilishawahi kudeti na mwanaume anayekesha bar na kubadili bar moja baada ya nyingine halafu asubuhi anarudi nyumbani yuko mbwiii...!!
Siku moja nikamtolea uvivu, nikamwambia kwani guest shilingi ngapi?
Sababu ukitoka kunywa unakuwa uko mwenye starehe zako basi ukikesha hadi asubuhi usirudi nyumbani na shombo za pombe, chukua guesti lala huko badili tisheti na suriali amka agiza supu zimua na chupa mbili kutoa heng'iova halafu rudi nyumbani ukiwa soba.
Kasinde Matata.