TASK FORCE
JF-Expert Member
- Apr 7, 2017
- 2,465
- 3,459
Huyo polisi anastahili kusimamishwa kazi.
Ndo mambo gani sasa hayo ya kufyatua risasi hewani kama siyo kutishia watu?
Ingekuwa ni juu yangu ningemfukuzia mbali kabisa maana hafai huyo....he is too trigger happy!
Utasikia shitaka lake sasaIshu ni hv, huyu ndugu malima jr alienda IOM akamuacha dereva wake kwenye gari, dereva akaegesha gari upande ambao kuna maduka na migahawa na ni upande ambao huwa hawakamati labda wakubabatishe mjinga mjinga, sasa mabwana wakubwa (Majembe) wakaja akawa anataka kukamata gari, dereva anamuuliza kitambulisho jamaa akagoma, sasa dereva akaanza kumfokea ndo wananchi wakajaa kwenye tukio, walipomuomba tena atoe kitambulisho akagoma ndo wakataka kumpiga, bahati walikuja na polisi ambao walikuwa kwenye gari, baada ya kelele polisi wakatoka kutuliza presha za wananchi. Mwenye gari (Malima) alipokuja akauliza kwa nn wanataka kukamata gari na kwa nn hawataki kutoa vitambulisho majibu hayakupatikana, Polisi wakapanda kwenye gari wakawa wanaondoka, sasa cha ajabu baanda ya mwendo waa sekunde 30 wakapaki gari pembeni wakaanza kujibizana upya ndo hapo dereva akapaniki na askari akapaniki jamaa akaamua kufyatua risasi juu watu hawakukimbia. Ikabidi Polisi wamchukue Malima Jr waende nae Kituoni.
Hii ni kwa mujibu wa kitabu gani cha sheria mkuu? Kwa hiyo ukiwa na silaha inatakiwa uwe kama bubu.We bwana mdogo hivi unajua kuwa askari akishika siraha ya moto haruhusiwi kubishana na raia au kuonesha jazba za waziwazi namna ile
Inasikitisha sanaYani sijui hata Kama alipitia mafunzo huyu polisi, enzi zileeee kulikuwa na somo pale polisi la jinsi ya kuzuia hasira, na huyu zingekuwa zama zile tayari kazi alikuwa Hana kwa makosa kadhaa niliyoyabaini hapo.....
Tzzzz hiyoMkuu we acha tu. Kuna mambo ukiyafikiri kwa kina wazimu utaambatana na wewe
Askari yupo sahihi kufyatua risasi hewani ila hayo maneno yaliyokuwa yanamtoka mdomoni ndo yameondoa dhana yote ya kufyatua hewani....
Labda usubiri siku utakayopewa zamu ya kupokea jeneza langu Airport. Otherwise, endelea na majukumu yako ya ulinzi dada.Huna lolote kaa ulee watoto, ukiingia anga za wanaume ujue umekwisha huu mdomo wako utakusaidia jf tu.
Samahani ndugu hivi majembe ndio nini mnaniacha njia pandaHaku park sehemu isiyoruhusiwa, gari lilikuwa limeegeshwa na dereva akiwemo ndani, na liliegeshwa upande wenye maduka ambao unaruhusiwa, ila mara nyingi huwa wanapenda kusumbua na hata kusababisha wenye maduka kukosa wateja kwa kuogopa kukamatwa na hao majembe
wameshapinda na maisha.nimeiona video yani hawa askari wetu aisee, daah,
Nimependa hiyoHivyo ndivyo polisi wetu wapopandwa na hasira na kuua raia wasio na hatia; baadae kuweza kupoteza ushaidi unasikia, polisi imefanikiwa kuuwa jambazi moja na mengine kutoweka na kutokomea kusikojulika baada ya jambazi kuanza kurushia polisi risasi. Polisi hao waliweka mtego na kuwanasa kabla ya kufanikiwa kuiba. Kumbe maskini ya mungu tukio halikuwa hivyo. Dhuu Tanzania bado tuna safari ndefu sana kupata haki ya kila mwenye haki.
Umeeleza kishabiki, dhidi ya polisi. Jaribu kuwa mkweli.Polisi waliwatisha wananchi waliozunguka gari au walimtisha Malima ?Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.
Yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.
Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.
Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.
Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.
Kweli kabisa ila hapo ila hayo maneno ya askari sijayapenda ila huenda wametafsiri vibaya kauli za mkulu anapowaambia wafanye kazi wasiogopeKupaki kwenye hifadhi ya barabara ni kosa lakini wao wanamfanya mtuhumiwa kama GAIDI lililokuwa liktafuzwa kwa miaka mingi...
Kwann tena!?mkuu umekosea