Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Wahuni kama hawa ndio wamepewa jukumu la ulinzi na usalama. Wanaokotwa barabarani bila vetting wala nini matokeo ndio haya. Dah hii nchi ina safari ndefu sana aisee, huyo polisi ni zaidi ya kibaka haishangazi kuona wananchi kushabikia mauaji
 
Huyo polisi anastahili kusimamishwa kazi.

Ndo mambo gani sasa hayo ya kufyatua risasi hewani kama siyo kutishia watu?

Ingekuwa ni juu yangu ningemfukuzia mbali kabisa maana hafai huyo....he is too trigger happy!
 
Halafu kwa nini tudaiane ushuru kwa mtutu wa bunduki, hawa TRA wanapochukua hela kwa nini wasichukue na address ili iwe kazi rahisi tu kutufuata home kudai kodi yao, TRA lazima iwe rafiki na mlipakodi waache mambo ya kihuni namna hii. Hivi Magufuli anadhani kila kitu kutumia nguvu tu
 
Ishu ni hv, huyu ndugu malima jr alienda IOM akamuacha dereva wake kwenye gari, dereva akaegesha gari upande ambao kuna maduka na migahawa na ni upande ambao huwa hawakamati labda wakubabatishe mjinga mjinga, sasa mabwana wakubwa (Majembe) wakaja akawa anataka kukamata gari, dereva anamuuliza kitambulisho jamaa akagoma, sasa dereva akaanza kumfokea ndo wananchi wakajaa kwenye tukio, walipomuomba tena atoe kitambulisho akagoma ndo wakataka kumpiga, bahati walikuja na polisi ambao walikuwa kwenye gari, baada ya kelele polisi wakatoka kutuliza presha za wananchi. Mwenye gari (Malima) alipokuja akauliza kwa nn wanataka kukamata gari na kwa nn hawataki kutoa vitambulisho majibu hayakupatikana, Polisi wakapanda kwenye gari wakawa wanaondoka, sasa cha ajabu baanda ya mwendo waa sekunde 30 wakapaki gari pembeni wakaanza kujibizana upya ndo hapo dereva akapaniki na askari akapaniki jamaa akaamua kufyatua risasi juu watu hawakukimbia. Ikabidi Polisi wamchukue Malima Jr waende nae Kituoni.
Kinachonisikitisha zaidi ni ujasiri wa wananchi kutokukumbia baaada ya huo mlio wa risasi!
 
Kuna tatizo kubwa sana na vijana wa Polisi

Hakukuwa na haja ya kupiga risasi bila uwepo wa tishio la amani

Halafu Polisi anasema ameapa na anaonyesha mkanda wenye bendera.
Masikini ya mungu hajui kuwa anapaswa kuongea kwa mamlaka si kusukuma mtu

Kumsukuma mtu ni 'provocation' na yeye ana silaha iliyokuwa tayari.
Kwa maana nyingine alitaka Adam a react halafu amfyatulie risasi.

Kama angeona ipo haja, angemuomba mkubwa wake aje kufanya 'arrest'
Yeye ana kiwango cha ku arrest na sijui kama anajua hilo

Anavyoongea ni kwa majivuno kwamba ni serikali, si kwa mamlaka kama mtunza sheria
Amejawa na jazba akiwa na silaha bila kujua hiyo ni precursor ya matumizi ya silaha
 
Umeisha sema watu walizingara sehemu Hiyo wakifikiri kuna jambazi, ili kutuliza au kumuokoa Mtu ktk mazingira hayo polisi au Mtu yeyote mwenye kibali cha silaha ana ruhusiwa kupiga risasi hewani Kama warning kwa watu wenye nia ya kutenda uovu. Na sababu za majembe kuivamia hiyo gari huja elezea , hivyo habari inakuwa haija balance
Mkuu umeona hiyo video lkn... Mbona police anamtishia malima kabisa
 
Umeisha sema watu walizingara sehemu Hiyo wakifikiri kuna jambazi, ili kutuliza au kumuokoa Mtu ktk mazingira hayo polisi au Mtu yeyote mwenye kibali cha silaha ana ruhusiwa kupiga risasi hewani Kama warning kwa watu wenye nia ya kutenda uovu. Na sababu za majembe kuivamia hiyo gari huja elezea , hivyo habari inakuwa haija balance

Umeangalia video? Au unaongea tu?
 
Umeisha sema watu walizingara sehemu Hiyo wakifikiri kuna jambazi, ili kutuliza au kumuokoa Mtu ktk mazingira hayo polisi au Mtu yeyote mwenye kibali cha silaha ana ruhusiwa kupiga risasi hewani Kama warning kwa watu wenye nia ya kutenda uovu. Na sababu za majembe kuivamia hiyo gari huja elezea , hivyo habari inakuwa haija balance
Hata kusoma hujui ndugu, Majembe alitaka kukamata gari alipoambiwa atoe kitambulisho akagoma
 
Hakuna watu wanaopewa training namna ya kukamata wahalifu au kudeal na RAIA kwenye msongamano kama polisi,Ila wanapenda Sana kujionyesha wao ndiyo Serikali. na huyu akifukuzwa kazi wengine watajifunza.
Kabisa wakiwa siriaz huyu kazi hana, kavunja pakubwa mno taratibu/sheria za matumizi na kubehave ukiwa na siraha ya moto mkononi,
 
Kighoma Malima karithisha Watoto wake wote Msimamo na kujiamini, Huyu Adam Ana Mdogo wake ni Daktari Mkuu Temeke na Mdogo wao yupo New York kwny Kamisheni ya Wanasayansi Nguli wa Reseach Duniani!

Dodoma kwny NEC iliyoisha Adam aliahidi angesimama binafsi kumhoji JPM kitendo cha kumfukuza Sophia Simba na Madabida kwa kumshabikia Lowassa wakati haikuwa haramu kabla ya Chama kuteua Mgombea akaishia Lupango![emoji12][emoji12]

Adam aongeze Umakini vyombo bya Dola havina Rafiki, ajikumbushe kilichomkuta Mkuu wa Usalama wa Taifa Hayati Imran Kombe!
 
Ningekua Mimi ndio mkuu wa kazi wa hao askari,ningewalaza mahabusu kwanza, kwa mjibu wa video hapo juu inaonyesha hakukua na sababu ya msingi sana kufyatua risasi nakuwatisha watu.Haya yote ni matokeo yakuchukua watu wasiojielewa na vilaza.
 
Kwa hiyo kama umekula kiapo ndio ufanye mambo ya kijinga?? Nchi hii bado sana.
 
Hawa askari wa sasa naona wanahitaji tena mafunzo aise Mwigulu Nchemba yupo humu ndani, wataacha huu uababe wa kizamani lini? Na ndiyo maana wanataka kuhakiki vyeti na ikiwezekana mental state zao, je wako sawa, hakuna mabangi bangi au vileo? Ila hii issue dhahiri kabisa kuna dalili za rushwa, tatizo wamekutana na kigingi, pole Mh Adam Malima
 
Umeangalia video? Au unaongea tu?
Nine soma maelezo yako, kwani yanatofauti na ulicho kieleza? Kama ni hivyo rekebisha maelezo yako yaendane na Hiyo video yako . Muda wa kuangalia video na kusoma maelezo unakuwa haba.
 
K
Hapo malima alikuwa analeta ile unajua mm ni nani, ukiona hadi huyo polisi kamind kiasi hiko, kuna kitu alikuwa kafanyiwa na jamaa. Kumbuka yule traffic alietukanwa na mke wa waziri maiga, hawa watu wenye uwezo kifedha wamekuwa wakiwadharau askari wetu
Kikawaida/kitaratibu/kiitifaki mbunge ni mtu mwenye heshima katika jamii , askari alipaswa kutoa salamu ya saluti , askari wetu hawajui mipaka yao!
 
Haikuwa na umuhimu kwa Polisi kufyatua risasi juu kwa sababu hakuna aliyekuwa anamtishia au kutishia amani ya wananchi.

Ndio maana wanaporwa silaha kirahisi kwa kiherehere kisicho na sababu. Nadhani angesuburi kuona rabsha inayotishia amani ndio atumie hiyo SMG.
Akishapagawa namna hiyo akiwa na bunduki dawa ni kuwa mpole maana hashindwi kukulipua na liwalo na liwe. Kwa jinsi askari huyo anavyolalamika ni dhahiri uvumilivu ulikuwa unaelekea kuisha


Pole sana Adam.
 
Back
Top Bottom