Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Haya yote yalishasemwa na Tundu lisu,alisema wazi kuwa hawa watu wakishamaliza kwa wapinzani basi watawageukia watawala.
 
Kinachosikitisha ni kwamba RAIA WA TANZANIA sasa hivi HAWAOGOPI tena bunduki, kwa enzi za zamani hapo watu walishatoka mbio na taharuki, lakini sasa hivi wanamuangalia na kumwambia HANA MAMLAKA ya kutoa bunduki! HII INAASHIRIA NINI?
Iko siku wakikasirishwa kweli kweli wataingia barabarani kwa mamilioni na hakuna risasi zitakazotosha. Huu ndiyo ukweli mchungu; mazingira yanawajengea watz usugu na woga unaendelea kuwatoka.
 
Hata kama angetemewa mate usini huwezi piga risasi kijinga tena zihesabiwe hizo risasi akatwe kwenye mshahara wake kodi yangu haiwezi kutumika kupiga wananchi biti
Sadly kwa akili hizo huna mamlaka hata ya kumfukuza mchunga ng'ombe aliye ajiriwa na baba yako kijijini.
 
Yaani huyo askari kama mimi ndiye IGP namfuta kazi na kumuweka ndani mara moja kutokana na mstumizi mabaya ya silaha. Nadhani hana akili nzuri au amevuta bangi. Haiwezekani kuchezea bjnduki kama manati. Askari wa namna hii siyo salama. Na huyu kama kungekuwa hakuna watu angeua. Hatupo salama sana kwa askari wa namna hii. Haya ndiyo yale yaliyomkuta Nape. Cha ajabu hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa. Shame on him!
 
Usilolijua ni msitu wa mpingo kuhusu elimu.

Polisi, katumia busara sana, ila watu wengi ni wanafiki sana na ni mapopo katika fikira zao nawe ukiwemo.

Hilo tukio , lina mitazamo mingi ila hitimisho ni kuwa polisi aliongezea hiyo ya hewani ili kutuliza wapuuzi ambao wangetaka kufuata kituoni, maana huwa hamkosekani wa kukimbia nyuma ya gari la polisi kwenda kituoni.
Sikulaumu kwa huo Mtazamo wako,sio kosa lako.

1[emoji830]Elimu
2[emoji830]Elimu
3[emoji830]Elimu

Vyeti
 
Adam hakutishiwa na silaha mwangalie hiyo clips vizuri pale inaonekana Dreva wa Adam alitoa lugha ya kejeli kwa askari.
Na hiyo ndiyo ilipelekea askari kupiga risasi juu baada ya kuona anazongwa.
 
Nimpongeze aliyewezesha hizi clips zisambae,ni mtu mzalendo na ni muungwana ngoja hao wanaohusika na maswala ya nidhamu,utumiaji sahihi wa silaha na crowd control.
 
Hivi bangi imeruhusiwa kwa hawa "walinda usalama"? Sidhani kama haya ni matumizi mazuri ya silaha. Eti ana mkanda wa bendera.... So what? Nawalaumu wale jamaa ambao hawakuhakiki vyeti vya hawa vijana......!!!!! Si bure!!!! Eti ameapa.... Kama umeapa nenda Kibiti ukafanye doria!!!
 
Kila mtu humlaumu askari wakati wa amani.
Kukichafuka ndio askari anaonekana muhimu na kuheshimika, kimsingi askari hapendeki kwa sababu anazuia mambo mengi yanayogusa maisha ya watu ya kila siku

Nimefundishwa Jeshi ni kwamba askari ni kioo cha jamii na sababu ya nidhamu.Sasa kama.Askari huna nidhamu,huwezi kuheshimu RAIA,uko busy kunyanyasa RAIA,ndiyo sababu ya rushwa duh!ukiwa hivyo unastahili red carpet tu.
 
Angalia vyote hivyo vipo,cha kwanza kinachoonekana ni jinsi raia walivyokuwa wakali wakitukana matusi huku wamewaelekezea polisi camera usoni,angalia response ya polisi!

Mkuu huyo ni tabaka la juu au tawi la juu subiri lidondoke ndiyo wanajua akama.akina Nape.
 
Binafs me nafurahi sana kuona viongozi na makada wa CCM nao wanashikiwa bunduki ngoja nao waonje joto ya jiwe safi sana
 
Ningesikitika sana kama wale askari wangemuacha Adam huru katika mazingira yale.Nimependa wote walivyoungana na kumuweka chini ya ulinzi. Lazima tutii vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Tuiheshimu serikali.
 
Naunga mkono kitendo cha self defence cha yule askari...Malima ni mmiliki wa bunduki ya kivita (SMG), angeweza kumzidi ujanja.
 
Malima ana bahati sana ningekuwa mimi ndo polisi jina lake lingekuwa limeshabadilika na pengine tungekiwa tumeshagawana majengo ya serikali, yeye muhimbili mimi ukonga
Wewe endelea na kazi ya kulinda Lumumba na kusafisha viatu vya Makonda, hauna nafasi kwenye jeshi letu la polisi tunalijengea weledi
 
Video clip inatoa mwanga zaidi kuhusu hilo tukio.
Video clip inatoa mwanga zaidi kuhusu hilo tukio.
Inaweza kuwa hivyo au la kutokana na haya yafuatayo, maelezo ya mleta thread yanatofautiana na Hiyo video Kama nilivyo muuliza huko nyuma, pili video haikuchukua taarifa za awali , hivyo unaweza kuwa na picha inayo onyesha kitu fulani na kuacha vitu fulani hivyo kutoa taswira isiyo ya kweli. Au iliyoelemea upande moja. Na si nia yangu kupigia upatu upande wowote . Kwa sababu haitatujenga
 
Nimefundishwa Jeshi ni kwamba askari ni kioo cha jamii na sababu ya nidhamu.Sasa kama.Askari huna nidhamu,huwezi kuheshimu RAIA,uko busy kunyanyasa RAIA,ndiyo sababu ya rushwa duh!ukiwa hivyo unastahili red carpet tu.
Hujafundishwa raia kuheshimu askari?
 
Ni kweli mkuu yaani kila mtu analaumu polisi lakini wakumbuke Malima lazima amejibu jeuri(dharau), mbona polisi walikua wameanza kuondoka iweje wakarudi?
Dharau jambo baya sana kwa kila mtu ukionesha dharau tegemea kukutana na feedback mbaya.
Wewe utakuwa unawakilisha maoni ya kwenye uelewa mdogo.kwa hiyo dharau kiboko yake ni risasi
 
Malima amechanganyikiwa kukosa ubunge.
Askari akikupa amri lazima utii tu hata kama una haki zote.
Ingekuwa mie ni yule askari nisingepiga juu kuharibu kuharibu mazingira tu,ningempa Malima risasi kama tano za kwenye vidole vya miguu akajifunze utii bila ya shuruti

Ndio maana hujawa yule askari!!
 
Niliwahi kuhoji humu, ni namna gani tunawaajiri askari siku hizi? Wakati wa mkoloni askari lazima alikuwa mrefu mwenye kilo za kutosha, akikunasa kibao lazima uone nyota japo ni mchana, akikushika tanganyika jeck anakunyanyua kwa mkono mmoja, sasa hivi jamii ya hamorapa sijui vinaingiaje huko umwerani?

Hapa huyu jamaa alikuwa wa kukamata tanganyika jeck na kutupa ndani ya tenga, sasa makelele meengi dalili ya woga tu, kwanza kapiga blast inamaana risasi ashamaliza, yangetokea majibizano hakuwa na risasi hata ya kujihami, mambo ya hovyo tu.

hivi risasi moja inauzwa shs ngapi? Hawawezi chezea silaha hovyo namna ile, lazima wakatwe kwenye mshahara.
 
Back
Top Bottom