Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Akienda kukabidhi silaha sijui atatoa justification gani kwa bosi wake juu ya matumizi ya hizo risasi!
 
Hao Majembe, Yono and the like ni wasumbufu sana, wanasumbua sana wananchi, wanadai dau kubwa kama Mtu hana gari inapelekwa wanakojua mwananchi akisharekebisha Tra anapofata Gari Yake hapewi badala Yake anaambiwa alipe pesa chungu nzima eti kwaajili ya ulinzi, nakwambia iwe ni Kwa Masaa au Siku moja au mbili nakwambia atadaiwa hela nyingi kuzidi ule Mshahara anao lipwa mlinzi aliyeajiriwa kwenye kampuni ya ulinzi Kama vile ktk, night support, etc! Kwa hili la leo wamegusa pabaya huenda inaweza ku draw attention kubwa itakayopelekea wananchi kuondokana na kadhia ya hao jamaa! Komaa nao kaka Adam watie akili!
Akomae na nani wakati mwenzako yupo ndani muda huu? Amefunguliwa mashtaka kwa kosa la kumzuia askari asitimize wajibu wake (RB yake ipo).

Hata ikitokea akitoka huko rumande lakini atakuwa tayari amesumbuliwa bila hata sababu ya msingi.

Muda mwingine hekima ni bora kuliko jeuri. Tutambue nyakati zimebadilika kwa sasa.
 
Hata wanachi wanazo silaha, tusipo angalia itakuwa ni kuwahiana sasa! Polisi hapewi silaha ili atishie namna hiyo. Kuna situation ambapo hubidi kutumia. What I can see kuna hali ya mtafaruku kati ya raia na polisi.
Na kwa taarifa yako maaskari wanajua kabisa kuwa kuna raia wana silaha na ndio maana hizo SMG zao wanaziweka tayari muda wote.

Hata kwenye tukio hilo la Malima, huyo askari alijua kabisa kutakuwa na kuwaiana na ndio maana akafyatua za kwake ili kujihami na lolote.
 
Kwahiyo mtu akikuuliza mkuu wa masafara yuko wapi ni dharau? Hivi nyie ni nani aliewashikia akili zenu? Au ndio jinsi mlivyozaliwa?
Polisi anapiga risasi hewani halafu unasema eti alidharauliwa.
Mambo ya mkuu wa msafara yuko wapi, sio kwa mazingira Yale, maana yake wahuni wao is ha wazunguka askari, who knows nani rafiki nani adui! Wangeendeleza debate wakati huo wa hatari watu wabaya wangeweza kuwadhuru askari, ye Malima angetii amri kwanza, then angeenda hapo Oysterbay police kuwaulizia hao wakuu wa msafara, lakini sio kwa ufinyu ule wa busara aliouonyesha pale, je askari angepanic zaidi akamshoot nani angepata faida?
 
Kwahiyo mtu akikuuliza mkuu wa masafara yuko wapi ni dharau? Hivi nyie ni nani aliewashikia akili zenu? Au ndio jinsi mlivyozaliwa?
Polisi anapiga risasi hewani halafu unasema eti alidharauliwa.
Kile kitendo cha kupiga risasi hewani ndo cha hatari sana jaman.ingeweza kumdhuru mtu pale tungekua tunaongea mengine.sawa yawezekana adam malima ana makosa lkn polisi kaaminiwa ndo maana kapewa silaha.hata ongea yake tu huyo polisi inaonekana hakuwa vizuri na ni mtu wa jazba,hafai kua askari naomba kama kuna kitengo cha kulima mbogamboga huko polisi apewe huyo askari manake ni hatari kumpa silaha.upuuzi kabisa ule
 
Hata kama angetemewa mate usini huwezi piga risasi kijinga tena zihesabiwe hizo risasi akatwe kwenye mshahara wake kodi yangu haiwezi kutumika kupiga wananchi biti
Yaan kabisa zihesabiwe zile risasi alizopiga hewani alipie
 
Mkuu nimecheka na pia hii comment imenifikirisha....naona polisi wanapoelekea watawavunja miguu hadi JK na Ben Mkapa.

Ngoja tuone.
Kwa haya mambo ya kipuuzi yanayotokea nchini Ni lazima sasa tutambue adui ya watanzania ni Nani? Mwalimu ningekuwa na uwezo ningeomba ufufuke ujionee nchi uliyoijenga mawaziri wastaafu wanavyotishiwa kwa risasi. Pole Malim. Pole Nape.
 
Kavaa mkanda tu wenye bendera ya taifa kabwatuka kiasi kile, Siku akivaa ngao ya bibi na Bwana begani unafikiri itakuwaje?
Akamuulize Zombe maisha anayaonaje kwa sasa?
Kama mpaka tunappandika hapa huyo askari hajavuliwa uaskari ntashangaa sana.unapiga risasi hewani kutishia raia?wakati unalipwa mshahara kwa kodi zetu kulinda raia na mali zao.tunaomba fagio la vyeti feki lipite polisi na jeshini.na kuanzia sasa hivi polisi waajiriwe wenye diploma na degree
 


Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.

Yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.

Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.

Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.

Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.

Adam Kighoma Malima alikuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, enzi za Kikwete. Anatokea katika chama cha CCM.


Huyo askari lazima apandishwe cheo na Magufuli.
Ana haki kabisa ya kutodharaulika
 
Na kwa taarifa yako maaskari wanajua kabisa kuwa kuna raia wana silaha na ndio maana hizo SMG zao wanaziweka tayari muda wote.

Hata kwenye tukio hilo la Malima, huyo askari alijua kabisa kutakuwa na kuwaiana na ndio maana akafyatua za kwake ili kujihami na lolote.
Na wale wa kibiti silaha zao zilikuwa full magazine na zilikuwa zipo on... teh teh

Endeleeni kutengeneza matabaka kati yenu na raia mtavuna ya kibiti
 
Kuna kosa lilitokea bare linalohusiana na matumizi mabaya ya barabara.Askari walijaribu kumchulia harua dereva ambaye alikuwa kwenye gari wananchi nao waliona na wakasogea karibu na kuanza kulalamika kwa maneno.Huyu Malima akiwa miongoni mwa RAIA nae kasogelea tukio mstari wa mbele kabisa huku wakionekana kuvuruga kazi ya askari

Mtazamo wangu n kuwa askari walikuwa sawa kwasababu kilichotokea kwa wingi ule wa watu na kilichokuwa kinazidi kuendelea ilikuwa n dharau kwa jeshi la polisi.
Umeiona video mkuu?
 
Askari anapotakiwa kuonyesha kitambulisho ni wajibu wake aonyeshe. Mavazi na virungu sio vielelezo kamili. Wanatakiwa wavivae kama wanafunzi wa jangwani au zanaki.
Mawazo ya kipuuuzi nimeanza kufahamu kwa nini raisi anasema sipangiwi ,maana akiwasikiliza ninyi roho zenu zimejaaa chuki na ushabiki usio kua na maana.Unafahamu ni sheria gani inampa mamlaka askari kutumia risasi za moto?? Au unabwabwaja tu.
 
Majembe ni Kampuni iliyosajiliwa kisheria na inafanya kazi kwa kufata taratibu na wanalipa kaodi yetu ivo siowahuni km alichukua Pesa bank kwa kuweka dhamana ya gari na sasa kavunja mkataba acha gari lichukuliwe akalipe Pesa au gali lipigwe mnada lifidie deni sana sana anachokifanya nikulifanya deni kuwa kubwa.Iyondokukopa harusi kulipa matanga.
 
Mawazo ya kipuuuzi nimeanza kufahamu kwa nini raisi anasema sipangiwi ,maana akiwasikiliza ninyi roho zenu zimejaaa chuki na ushabiki usio kua na maana.Unafahamu ni sheria gani inampa mamlaka askari kutumia risasi za moto?? Au unabwabwaja tu.
Askari anatakiwa aonyeshe kitambulisho instant anapotakiwa kufanya hivyo. Wapo wahalifu hutumia mwanya huyo.

Hata Nape naye alipodai kitambulisho alikuwa mpuuzi? We kama uliamua kuwa askari kivae kitambulisho haraka kama mwanafunzi tena kionyeshe f namba zako, kituo unachotoka, majina yako kamili na cheo chako. Usiweke namba za vyeti kujua kwako kusoma na kuandika kunatosha
 
Back
Top Bottom