Masanja awachana 'live' wambea wa ndoa yake

Masanja awachana 'live' wambea wa ndoa yake

SN.BARRY

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
4,038
Reaction score
8,929
Video hiyo hapo

"Yaani namuachaje huyu msichana, nimuache huyu dada halafu? Yaani hata ndoa ziishe leo zote halafu kesho tuanze upya namrukia huyu huyu! Nataka niwaambie kwa lugha rahisi, ninamshukuru Mungu kwasababu Mungu yupo kazini."

"Yote ambayo wanangu mnasikia, msiende na mikumbo watu wanachoongea, endelea kuamini katika ukweli ya kwamba tunachokwambia mke wangu mimi ni mke ambaye mnaishi naye hapa kanisani mnaelewa. Ni mke ambaye anajichanganya na ninyi, hatengenezi umbali kati yenu na sisi, na hili ni darasa nililifanya kwakwe."

"Anaongea na watu wote, anacheka na watu wote, hivyo ndivyo huyu mwanamke alivyo. Haiwezi kutokea tutengeneza mazingira ya kumfanya asiongee na watu."

"Natamani dunia ielewe leo kwa jinsi ninavyomuelewa huyu msichana, tuweke uchungaji na kanisa pembeni, nimkute uso kwa uso anapiga "gemu" na mtu, namkamata kwanza wife halafu nampima yule jamaa nammudu au simmudu? Nikiona hii ngoma siiwezi kuzipanga atanipasua, nitarusha maneno tu lakini wife naondoka naye."

"Sisi tumeoana hadi kitutenganishe kifo. Hakuna stori hapa kati kati, mchawi, pepo, jini cha kusambaratisha. Nataka nikukwambie mabaya yote yanayokuja mbele yetu hatushindi kwa akili, uweza na nguvu zetu, tunaye anayetupa kushinda, ndiyo maana nina uhakika wa kubaki na mke wangu mpaka siku ya unyakuo."
 
Back
Top Bottom