Mimi sisemi kwamba hao ma secretary hawana hizo tabia ila kwa upande wangu sijawahi ingia ofisi secretary akaniletea nyodo au kiburi kwanza hakikisha na ww huna muonekano wa kua na kiburi au dharau imagine unaingia ofisi ya watu husalimii unauliza nimemkuta fulani unatarajia huyo secretary atakupokeaje mwingine anapeleka barua za maombi ya kazi inakua kama vita kafika kaacha barua kasepa na secretary nae anazikalia imeisha hiyo.
Niliendaga ofisi moja town mmiliki wa ofisi yupo ghorofa ya mwisho nikafika nikamkuta dada mmoja mziri yuko safi sana nikamsalimia mwanzo alitaka kuleta nyodo ila kwakua nilifika kwenye dawati lake na kumsalimia na kumuuliza hali ndipo nikaomba kumuona boss basi alikua ananiangalia as if nimekosea njia boss aliporuhusu niingie akawa anaskia tunavyopiga stor na kicheka nilipotoka nikamuaga vizuri siku nyingine naenda pale nikamsalimia tena na kumjulia hali alichangamka sana akijua fika sina nyodo na boss ni mshkaji wangu mpka leo yule dada ananiheshimu sana.
Hatujui kuishi na watu tumejawa viburi lawama alafu tuliletewa nyodo tunakua wakwanza kulalama kama tumeonewa.
Haikupunguzii kitu kusalimiana vizuri na secretary au mlinzi kwenye eneo fulani na kuna siri kubwa sana ya mafanikio ukijua kuishi vizuri na walinzi na ma secretary hawa watu wanaweza kupa picha halisi ya kampuni au ofisi unayotaka kuingia na wanaweza push jambo lako likafika sehemu sahihi