vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Aisee nimeshangaa kundi kubwa la watu walioshangilia timu yao kutolewa na Wydad kwa mbinde na kusema hawadai, wamekufa kiume cha ajabu zile kauli hazihakisi nyuso zao zilizovyo kwasasa. Admin wa Simba anajitahidi sana kupost taarifa, matukio, kumbukumbu, n.k kwenye page rasmi ya Simba lakini cha kushangaa hali imebadilika, wanao re tweet, comment na kulike ni idadi ndogo sana hata robo ya ile nyomi haifikii. Na kwa bahati mbaya wale wanao comment ndio wamechafukwa kabisa, wanaonesha wana hasira mno juu ya timu yao. Kumbe mlijifanya mmeridhika na ugali na mlenda, mkijua jirani yako atakula huo huo ugali na mlenda ama pengine atakuwa na hali ngumu zaidi kwa kula ugali na chumvi. Leo umeona jirani yako anukisha pilau, umeamisha hasira kwa mzazi wako kwanini hapiki vitu vizuri kama fulani. Nyie hamudai kitu hivyo endeleeni kuwa kama awali vimbeni kwa mlipofikia.