Mashabiki wa Simba SC tunahitaji kujitafakari

Mashabiki wa Simba SC tunahitaji kujitafakari

CARIFONIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
616
Reaction score
1,453
Sisi mashabiki wa simba tunaitaji kujitafakari, ifike muda tukubali kuwa wenzetu upande wa pili wamejipanga kutuzidi sisi kwenye huu msimu, kitu ambacho tulikua tunajidai nacho ni ushiriki wetu kwenye michuano ya kimataifa lakini baada ya kutupwa nje kwenye michuano hiyo kwa sasa tumeanza kuisoma namba

Sasa hivi tunapocheza na Yanga hatuna jeuri ya kuwafunga zaidi tunakaza Mayele asitufunge ndio ushindi wetu huo, msimu huu tumekutana mara tatu, mechi ya kwanza ni ngao ya jamii tukapigwa kimoja cha mkwezi then kwenye ligi ya NBC tumekutana mara mbili na games zote tumetoa sare, jambo la kushangaza sisi mashabiki wa simba hua tunafuraia haya mtokeo utadhani sisi ndio tumeshinda ndio maana mashabiki wa yanga wanatudharau sana sasa hivi.

Timu yetu ya Simba imesahau lengo la timu yoyote ile inapokutana na timu nyingene ni kuakikisha inaibuka na ushindi na sio kutafuta sare au kumzuia mchezaji flani asifunge halafu tuanze kujisifu eti flani mbona hakutetema leo.

Ndio mahana tunaonekana wote ni makolo tu ifike muda viongozi, wachezaji na mashabiki tujitafakari lengo la kuanzisha timu ni kupata ushindi na kubeba makombe na sio bla bla za sijui tumefika robo fainali club bingwa Africa au shirikisho. jamani tuache ukolo, kwanza wakiambiwa makipa ambao hawajafungwa na bwana fistone kalala mayele katika timu za hapa bongo je Manula hatajitokeza?
 
Kudrop msimu mmoja tu maneno!Misimu yote minne simba iliyokuwa bingwa imeifunga yanga mara ngapi!Mkuu kipaumbele cha simba kwa sasa si kushindana na yanga
una ubavu wa kushindana na nani?,vi robo robo hivyo ndio vinawapa jeuri.
 
Ukitaka kugombana na mashabiki wa simba, basi wewe waambie tu ukweli.
Ifike mahali tuelewe mpira haswa ni nini?
Inabid mmoja akosee au awe dhaifu ili mwingine awe winner, vipi mngejisikiaje kila msimu Simba wawe wababe wa yanga tu je unadhan kungekua na Radha ya hii ligi?
Kupokezana kunaleta burudani Zaid kuliko mmoja tu ndio atawale ,Simba kateleza huu msimu ambapo kampa faida yanga na yanga atateleza huku Simba akiwa na hasira atakuja kwa kishindo au Simba na yanga zitateleza alafu timu nyingine itaibuka mbabe.

Sasa ni Waz kwa mawazo yenu mnataman Simba aendelee kuwa bingwa kila msimu huku wengine mkiwa wasindikizaji ,haya epl hakuna kitu km hicho
 
Sisi mashabiki wa simba tunaitaji kujitafakari, ifike mda tukubali kua wenzetu upande wa pili wamejipanga kutuzidi sisi kwenye huu msimu, kitu ambacho tulikua tunajidai nacho ni ushiriki wetu kwenye michuano ya kimataifa lakini baada ya kutupwa nje kwenye michuano hiyo kwa sasa tumeanza kuisoma namba

Sasa hivi tunapocheza na yanga hatuna jeuri ya kuwafunga zaidi tunakaza Mayele asitufunge ndio ushindi wetu huo, msimu huu tumekutana mara tatu, mechi ya kwanza ni ngao ya jamii tukapigwa kimoja cha mkwezi then kwenye ligi ya NBC tumekutana mara mbili na games zote tumetoa sare, jambo la kushangaza sisi mashabiki wa simba hua tunafuraia haya mtokeo utadhani sisi ndio tumeshinda ndio maana mashabiki wa yanga wanatudharau sana sasa hivi.

Timu yetu ya simba imesahau lengo la timu yoyote ile inapokutana na timu nyingene ni kuakikisha inaibuka na ushindi na sio kutafuta sare au kumzuia mchezaji flani asifunge halafu tuanze kujisifu eti flani mbona hakutetema leo.

Ndio mahana tunaonekana wote ni makolo tu ifike mda viongozi, wachezaji na mashabiki tujitafakari lengo la kuanzisha timu ni kupata ushindi na kubeba makombe na sio bla bla za sijui tumefika robo fainali club bingwa Africa au shirikisho. jamani tuache ukolo, kwanza wakiambiwa makipa ambao hawajafungwa na bwana fistone kalala mayele katika timu za hapa bongo je Manula hatajitokeza?
Yaani hebu fafanua ni kwa namna gani mashabiki tunatakiwa kujipanga? Au sasa tuingie uwanjani kufanya vurugu?

Screenshot 2022-05-01 at 12.06.05.png
 
Iwapo Mtoa Mada Anaitwa aidha New York Au California Au Washington Naomba Mumpuuze. Hiyo Sio Miji Ya kitanzania.... Miji Yetu Sisi ni Bunju, Buza na Mchambawima Zanzibaaaar .
Huyo Naomba Apuuzwee kbs kbs..!
 
Simba haina mashabiki kama wewe, na hata hivyo raha ya ligi ni kupokezana ndio inakuwa na msisimko. Nakumbuka mwaka jana Simba ilichukua ligi lakin mashabiki waliona kawaida tuu kwasababu walishalizoea.
 
Simba haina mashabiki kama wewe, na hata hivyo raha ya ligi ni kupokezana ndio inakuwa na msisimko. Nakumbuka mwaka jana Simba ilichukua ligi lakin mashabiki waliona kawaida tuu kwasababu walishalizoea.
kweli, inatakiwa Yanga nae achukue ubingwa mara nne mfululizo, sioni timu ya kupambana nae hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom