Kuhusu kiingereza mleta mada hapa umepotosha kwa 100%.
Mimi binafsi nimesikiliza Clouds Fm, na mtangazaji hakusema hilo. Amesema wanyarwanda wanazungumza kinyarwanda tu, na alipojaribu kufafanua akasema wanazungumza Kifaransa.
USAHIHI.
Rwanda kijamii ni nchi inayozungumza Kinyarwanda (mchanganyiko wa lugha ya Kitutsi, Kihutu, Kitwa), na miaka yote lugha ya kiofisi ni mbili (Kinyarwanda na Kifaransa). Kama wewe ni mnyarwanda hujakwenda shule vizuri na kuishi mjini, basi hata Kifaransa huwezi kuongea, utabakia kwenye kilugha tu (kinyarwanda).
Kuhusu Kiingereza, Rwanda wako nyuma zaidi, ndio sasa wanaanza kujifunza sasa baada ya Kagame kuridhia kiingereza kuwa lugha rasmi ya tatu kitaifa. Hata wasomi wa kinyarwanda wa kisomo cha juu walioishi na kujifunza kwenye nchi na vyuo vyenye kuongea kiingereza, bado kiingereza chao ni duni mnoo (kwenye matamshi (pronunciation), Usanifu (grammar) na mtitiriko (flow) kuliko hata kijana wa kitanzania aliyesoma na kumaliza shule za kata.
Kwenye kiingereza, mtu pekee anayeweza kumbambaisha mtanzania ni mzungu tu, wengine wote tunabanana fresh.