#COVID19 Mashabiki walimponza Mwl. Kashasha, aliambukizwa COVID-19

#COVID19 Mashabiki walimponza Mwl. Kashasha, aliambukizwa COVID-19

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
KIFO ni fumbo. Hutamsoma tena Mwalimu Alex Kashasha kwenye kolamu yake aliyokuwa akiandika kwenye ukurasa wa 12 wa Mwanaspoti kila Jumamosi. Kifo kimemchukua, atazikwa Dar es Salaam Jumatatu.

SOMA ZAIDI: Kilichomuua Mwalimu Kashasha hiki hapa

Hutasikia tena ile misemo, mbwembwe zake akitangaza mpira kwenye TBC au akifafanua jambo kwenye Mwananchi Digital.

Kaka wa Marehemu, Deus Alexander alisema alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Uviko-19 ambao aliupata akitoka kwenye mechi ya Simba na Yanga mjini Kigoma baada ya kupiga picha na kila aliyekuwa akimuomba kwenye vituo mbalimbali akiwa kwenye basi kurejea Dar.

Alisema watamzika Jumatatu ya Agosti 23 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mchana.

“Kwa kuwa mdogo wangu alikuwa mtu wa watu hatutaki kuwanyima mashabiki na wanasoka wenzake uhuru, hivyo tunatafuta eneo la wazi ambalo litakuwa rahisi kumuaga na tutawaambia mapema,kumuaga itakuwa Jumapili, kiukweli tuna maumivu kumpoteza mtu mwenye upendo sana kwenye familia,” alisema na kuongeza Kashasha alianza kuumwa tangu alipotoka kwenye fainali za Kombe la ASFC mjini Kigoma Julai 25.

“Alikuwa anasumbuliwa na figo ndani ya miaka miwili ambayo alikuwa anahudhuria kliniki, tatizo lilipoanzia alitoka na basi kutoka kwenye fainali ya Simba na Yanga, kitendo cha kupiga picha na watu kila kituo kulimfanya apate ugonjwa wa Uviko 19 kwani alifika nyumbani akiwa amechoka sana,” alisema kaka yake na kuongeza ilimletea shida, alifika amechoka sana.”

“Hospitali wakamtibia ugonjwa wa mapafu lakini baada ya kuona hali bado haipo vizuri wakamfanyia upasuaji wa kusafisha figo, baadaye Mungu akamchukua,” alisema.

Kashasha ameacha mkewe Elizabeth Sawe na watoto wawili Theopster Kashasha (25) na Theonester Kashasha (16).

Alisema ndugu zao wote wako Dar es Salaam wakiwemo shangazi zake ambao walikuja kwenye harusi ya mtoto wa mdogo wa marehemu ambaye harusi yake ilitarajiwa kufanyika leo Dar es Salaam.

“Sisi tulishafanya sendoff wiki mbili zilizopita na kesho (leo) ndiyo harusi hivyo ndugu wote wako hapa mjini ndio maana tumeamua kumzika hapa hapa mjini Kwa kuwa hata wazazi wetu walishatangulia mbele za haki,” alisema.

Soma zaidi kuhusu Kashasha kwenye ukurasa wa tisa wa Gazeti hili na endelea kufuatilia kinachoendelea msibani kwenye mitandao yetu ya kijamii kila dakika.

Mhariri Mkuu wa Michezo wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Enock Bwigane aliliambia Mwanaspoti jana kwamba; “Kwa namna ambavyo alikuwa anazungumza sikutarajia leo hii kutokuwa naye, maana alitaka kujua usajili unavyoendelea, ligi ijayo kama haitakuwa na viporo, kiukweli alitarajia kufanya mengi msimu ujao.
 
cc brazaj , nakumbuka zile aina ya vifo ulikuwa ukizisisitiza sana !

Inasikitisha sana. Hiyo ni roho nyingine inayopotea bila sababu na bila ya yeyote kuwajibishwa. Yamesemwa sana ila hakuna katika mamlaka anayejali wala kutilia manani:

Nadharia iliyoshiba kuhusu vifo na wendazao

Tuko kama tumerogwa. Hakuna kujali, hakuna kuchukua hatua eti tulitolewa hofu:

IMG_20210718_063455_991.jpg


Tunaendelea kudondoka mmoja mmoja na kumsingizia Mungu hadi kila mtu yatakavyomkuta kivyake vyake.
 
TBC wakampandisha basi mzee wa miaka 64 kutoka Dar hadi Kigoma, Kigoma Dar zaidi ya km 2800 kwa pamoja.

TBC ndio wamechangia kumuua mzee kashasha.

Mzee Kashasaha ni wale senior bachelors, amepata mtoto wa kwanza akiwa na miaka 39 halafu mimi nina 32 bado mtu ananiambia nimechelewa kuoa< nawaangalia nasema hiiii, nisile good time nikae nahangaika na kuoa? Bado sana angalau 36 hivi ndio naweza kuanza kufikiria kuoa.
 
TBC wakampandisha basi mzee wa miaka 64 kutoka Dar hadi Kigoma, Kigoma Dar zaidi ya km 2800 kwa pamoja.

TBC ndio wamechangia kumuua mzee kashasha.

Mzee Kashasaha ni wale senior bachelors, amepata mtoto wa kwanza akiwa na miaka 39 halafu mimi nina 32 bado mtu ananiambia nimechelewa kuoa< nawaangalia nasema hiiii, nisile good time nikae nahangaika na kuoa? Bado sana angalau 36 hivi ndio naweza kuanza kufikiria kuoa.
Hayo ndio maneno.
Mzee Kashasha alikuwa na ugonjwa wa figo bado ndugu wanashadidia amekufa kwa Covid 19 na ameipata wakati wa safari ya kutoka Dar Kig na kurudi. Hakika familia zingine zinatia huruma.
 
Back
Top Bottom