1. Hoja nikuwa anakanusha kuwa haji Tanzania kwa mbeleko ya ulinzi wa watu ng'ambo bali atalindwa na Katiba na sheria za Tanzania. Ninahoji hoja hiyo ya Lissu, iweje leo aone umuhimu wa kulindwa na katiba na sheria za nchi yetu wakati akiwa na akili timamu aliutaka ulimwengu uutemee mate Tanzania!
2. Hashambuliwi mtu hapa. Ukirejea dokezo namba moja, kwa mtu mwenye uelewa wa kawaida kabisa lazima ajiulize, mtu aliyeitakia mabaya Tanzania akiwa na akili timamu tena mchana kweupe anawezaje kufikiria Tanzania hiyo hiyo impe ulinzi bila hata kujutia kitendo chake hicho cha kuitaka Tanzania itengwe na Dunia!? Ndiyo maana nikaandika yawezekana hajapona.
3. Sina hakika kama wewe ndiye Lissu ama la. Maana kwa mujibu wa sheria za JF, siwezi kuingia kwenye mtego wa 'name calling'. Maelezo ya awali yalikuwa yanajibu nukuu iliyokuwa kwenye post hiyo.
====
Nadhani ufafanuzi huu unatosha kuelewa maudhui ya post yangu ya awali.
Tuendelee na mjadala.