Mashaka makubwa kuhusu ujio wa ndege kubwa duniani Antonov 124 iliyotua na kuondoka KIA Desemba 22

Hii ni post ya mtu mwenye akili timamu asiyejaa mihemko
 
Happy Holidays.
Tarehe 21 mwezi huu kuna dege moja kubwa sana (pichani) lilitua pale KIA na taarifa tulizopata tukaambiwa ilikuja ikashusha mizigo baadaye ikaondoka.


Ndege hii ni maalumu kwa kubeba mizigo mbalimbali yoyote ile, inasemekana kuwa sinmara ya kwanza kuja hapa nchini ila kutokana na taarifa zinazosemwa za uongo ndiyo imepelekea kuleta mshtuko kwa raia wengi.

Kuna kampuni pale KIA inaitwa KADCO ambayo inaonekana ndiyo ilitoa huduma za kutoa huduma zote kuhusiana na ndege hiyo, mkurugenzi wake kaandika barua kujinasua kwa lolote japo kutokana na (barua hii chini) kachemka kwa kusahau dunia ipo kiganjani.


Aliposema "...ndege iliendelea na safari yake kwenda nchi nyingine..."

Wananchi tofauti wamefanya research na kuifuatilia hiyo ndege na kupata data sahihi kuwa, ndege ilipokuja ilipakia mizigo kama si kushusha kisha iliondoka direct to Abu Dhabi, angalia hapo πŸ‘‡πŸΎ


Kinachoumiza akili na kuwachefua raia ni baadhi ya watendaji kutumia lugha ulagai kwa wenye nchi (japo hawawezi kufanya lolote)

WHY Inatumika nguvu kubwa kupotosha ukweli ambao upo uwani mwa kila mtu?.

Je kama kuna upolaji wa mali za wananchi nani anaweza kutumia nafasi, nguvu nk kuokoa hilo?.



Karibuni kwa mjadara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…