Happy Holidays.
Tarehe 21 mwezi huu kuna dege moja kubwa sana (pichani) lilitua pale KIA na taarifa tulizopata tukaambiwa ilikuja ikashusha mizigo baadaye ikaondoka.
View attachment 2459076
Ndege hii ni maalumu kwa kubeba mizigo mbalimbali yoyote ile, inasemekana kuwa sinmara ya kwanza kuja hapa nchini ila kutokana na taarifa zinazosemwa za uongo ndiyo imepelekea kuleta mshtuko kwa raia wengi.
Kuna kampuni pale KIA inaitwa KADCO ambayo inaonekana ndiyo ilitoa huduma za kutoa huduma zote kuhusiana na ndege hiyo, mkurugenzi wake kaandika barua kujinasua kwa lolote japo kutokana na (barua hii chini) kachemka kwa kusahau dunia ipo kiganjani.
View attachment 2459087
Aliposema "...ndege iliendelea na safari yake kwenda nchi nyingine..."
Wananchi tofauti wamefanya research na kuifuatilia hiyo ndege na kupata data sahihi kuwa, ndege ilipokuja ilipakia mizigo kama si kushusha kisha iliondoka direct to Abu Dhabi, angalia hapo [emoji1484]
View attachment 2459092View attachment 2459093
Kinachoumiza akili na kuwachefua raia ni baadhi ya watendaji kutumia lugha ulagai kwa wenye nchi (japo hawawezi kufanya lolote)
WHY Inatumika nguvu kubwa kupotosha ukweli ambao upo uwani mwa kila mtu?.
Je kama kuna upolaji wa mali za wananchi nani anaweza kutumia nafasi, nguvu nk kuokoa hilo?.
View attachment 2459096
Karibuni kwa mjadara.