Sang'udi
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 9,138
- 22,236
- Thread starter
- #21
Zitto ni laana kwa hii nchi.Naona kuna mchezo unaendelea wa kuwazubaisha watu ili wasahau madai ya msingi ya taifa letu kwa sasa, Katiba Mpya.
Unapoona mtu hata kama ni mnafiki, kila siku anakuja na malalamiko kuhusu makosa aliyofanya marehemu, lakini akiambiwa aungane na wengine kutafuta solution ili makosa kama hayo yasijirudie, yeye anakimbilia kutaka Tume Huru kwanza, ujue huyo mtu hajielewi, ametumwa, na ni mbinafsi.
Hata kama akija na kisingizio cha haki yake kutoa maoni, hayo maoni ya kulalamika kila siku bila kuja na solution ni kelele tu kwa wanaojielewa, namshauri aache utapeli wa kuchezea akili za wajinga, aweke maslahi ya taifa letu mbele bila kujali nani yupo madarakani.
Lakini mkuu, ni kwa namna gani Katiba Mpya itakuwa mwarobaini wa haya maovu katika jamii zetu?
Wakenya wana Katiba bora kabisa karibu kuliko nchi zote Afrika, yet ndio taifa linaloongoza kwa rushwa na ukabila.
Hebu tueleze, ni vipi Katiba Mpya itakuwa mwarobaini bila kuwa na watu imara kama Magufuli?