Sang'udi
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 9,138
- 22,236
- Thread starter
- #61
Uzalendo ni kuipenda nchi yako na kuwa tayari kujitoa bila kujibakisha, hata uhai wako ikilazimika.Kusema za ukweli alikuwa anapenda kuendeleza hii nchi ila shida ni kuwa aliifanya Tanzania kama familia yake. Akatumia nguvu nyingi na ukiipinga Tanzania ni sawa na kumpinga yeye binafsi. Hilo lilikuwa ni kosa lake kubwa. Huu upepo wa kumkandia kama afanyavyo Zitto, utaisha kama upepo wa kisurisuri na mwisho miaka kama 10 ijayo, watu wawili watakuwa ni heros hapa TZ (Nyerere na Magufuli).
Uzalendo unahusisha kuchukulia attacks zozote zinazoelekezwa kwa nchi yako, ama ambazo zina lengo la kuihujumu nchi yako, kama zako binafsi.
Na hiki ndicho alichokifanya Magufuli. Alikuwa mzalendo kwelikweli.