Ni hivi ukisema Hayati JPM alikuwa fisadi ,mwananchi wa kawaida atakwambia heri fisadi aliyejenga SGR,heri fisadi aliyenunua ndege,heri fisadi aliyejenga vituo vya afya,Heri fisadi aliyepambana na wauza madawa ya kurevya,heri fisadi aliyebana mafisadi tukaheshimika tuingiapo ofisi za umma,heri fisadi aliyejenga viwanja vya ndege,heri fisadi JPM aliyejenga Madaraja makubwa,heri fisadi JPM aliyetuacha Lita ya petrol ikiwa inauzwa shillinga 2300,heri fisadi JPM aliyesaidia tukienda mahospitali tunapata madawa kuwa urahisi,heri fisadi JPM aliyesomesha watoto wetu bure ,heri fisadi JPM aliyetuhimiza kumuomba Mungi kipindi cha shida.
Mh zitto,unajisahaurisha ufisadi wa nyuma kwa kumpaka matope hayati JPM.? Mbona hukubwajabwaja akiwa hai? Au utasingizingia kuwa ungepotezwa .Nikwambie tu wanaokuelewa niwatanzania wa mitandaoni ambao siyo wapiga kura.Huku mitaani wanamwelewa sana JPM tena wanamkumbuka sana.
Yani wamemumisi kinoma.kama unafikiri ndiyo njia ya kuikuza ACT yako kwa kumsema marehemu ambaye hawezi kujitetea umelaniwa na chama chako na ukoo wako na wengine wenye tabia kama ya kwako nawashauri niwashauri tu muache Mara moja tabia yenu ya hivyo.
Vinginevyo tutajiuliza mengi juu ya usiri wa kifo chake.Kwa nini tulifichwa taarifa za kuumwa kwake?