'Mashangingi' ya Viongozi wa Taifa: Hili ni jini la kunyonya pesa za Wananchi

'Mashangingi' ya Viongozi wa Taifa: Hili ni jini la kunyonya pesa za Wananchi

Tukiendele kujipambanua kuwa tunabana matumizi tujue kama nchi hatuna vipaumbele kama mpaka sasa Viongozi wetu wanafanya matumizi ya anasa.

Fikiria gari moja la Mkuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Wakuu, Mawaziri, Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi za UMMA wanaendela kutumia magari aina ya V8 GXR yenye gharama ya Sh. Milioni 300.

Hii pesa ina uwezo wa kutengeneza madawati 3,500, Inaweza chimba visima vya maji 6-8 with solar, Kujenga zahanati 3 mpaka 4. Inaweza kujenga vyumba vya madarasa zaidi 10-11.

Tuige nchi kama Malaysia, Rwanda etc katika kubana matumizi na kutumia magari ya kawaida yenye unafuu.
Hivo v8 ziko kama 300 hivi tunabana matumizi. Hakuna mwafrika anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzake
 
Lakini mkuu hizo gari si zimeshanunuliwa toka enzi za jakaya?? Tufanyeje sasa tuziuze au?
Au unataka magufuli aingie madarakan anunue Vitz wakati mkuu wake wa mkoa ana VxV8??
Auze wapande daladala kubana matumizi kwani si wanalipwa mishahara?
 
Ukitengeneza hayo madawati, itakuwa ni hitimisho la uhitaji wa madawati? Acha roho ya kwanini kijana acha wapate magari mazuri ili kila kijana ajitahidi kusoma ili naye akifanikiwa ayapande.

hawaa minduku hawajasoma mbona ? usije danganya watoto wako, matumiz mabovu ya pesa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa kuwa hutegemei kuteuliwa ndo maana umeliona hili. Kweli tuna matatizo mengi. Hivi tupo +55m watu ndo utokee weye tu ulione hilo?? Weka maoni yako kwenye visanduku vya maoni.

Mkuu wa wilaya sio mtu wa chini ka hivyo, ni mkuu wa ailaya, ni nambari 1 wa wilaya nzima. Mwenye kustahili hishima mpe hishima yake. Huyo mtoto naye siku moja atajakuwa mkuu wa wilaya naye atapewa limshangingi lake.

sema kuwa tubuni mbinu mpya ya kupata hayo madarasa na mahospitali unayo yatamani ila sio kuwaminya wengine wenye nafasi yao.
Nadhani wewe Ni Jerry Muro na sidhani Kama nimekosea maana huu Ni mwandiko wake halisi kabisa bila kupepesa macho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ndio research ambazo tunatakiwa kufanya na kuwaambia hawa wanasiasa wajinga.
 
Ofisi ya RC au mkoani kunapaswa kuwa na V8 moja tu itakayotumika na RAS, DAS na DC incase wanasafari za mapolini kwenye barabara mbovu.

Kama RAS, DAS, DC na RC wanaenda msafara mmoja basi wote wataingia kwenye hilo V8.

RAS, DAS, DC na RC wakiwa mjini watumie usafiri wao wenyewe private, RAS,DAS,DC na RC wakopeshwe magari watalipia kupitia mishahara yao baada ya kuisha muda wa kuhudumu waondoke na hayo magari.

Tanzania ni nchi masikini inayohitaji kubana matumizi yasiyo ya lazima ili mambo mengine ya muhimu yatumike kwanza.
 
Kuna haja ya hivi vyeo vya kisiasa vitumike kama mfano wa uzalendo kwenye utendaji na kuisaidia hii nchi ili mwisho wa siku tufike kule tunakotaka, Tunavyowalea lea hawa wanasiasa na watendaji wengine ndipo tunapokaribisha wajinga wengi kuvifakamia hivi vyeo kwa maslahi binafsi.

Kuna haja ya kazi za kisiasa kama Uwaziri, RC, DC, Ubunge nk ziwe za kujitolea na sehemu za kuonyesha uzalendo kwa Taifa letu na kama mtu anahitaji mshahara mkubwa, marupurupu mazuri, nk aende kuajiriwa kwenye kazi za kitaalamu ili kweli aonyeshe utalaamu wake alipwe hizo stahiki azitakazo.
 
Lakini mkuu hizo gari si zimeshanunuliwa toka enzi za jakaya?? Tufanyeje sasa tuziuze au?
Au unataka magufuli aingie madarakan anunue Vitz wakati mkuu wake wa mkoa ana VxV8??
wapi katajwa magufuli? jitahidi kusoma post yote kabla hujachangia
 
Lakini mkuu hizo gari si zimeshanunuliwa toka enzi za jakaya?? Tufanyeje sasa tuziuze au?
Au unataka magufuli aingie madarakan anunue Vitz wakati mkuu wake wa mkoa ana VxV8??
Ukisema yalinunuliwa tangu enzi za JK ni upumbavu kiwango cha Flyover......hayo magari yananunuliwa mapya kila siku
 
HATUJIULIZI KWANINI KWENYE KUNUNUA MASHINE ZA MRI SJUI CT SCAN NK, INAKUWAGA UTATA
LAKINI KWENYE KUNUNUA MAGARI HAYO NI FASTER.....

OVA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti unakuta DC anatumia V8, DAS anatumia V8, RAS nae V8 halafu wote wanahudumu Mtwara mjini.
Mkuu wa mkoa wa DSM anatumia V8 la nini pale DSM.
Zipo gari nyingi 4x4 zinaweza kumudu hizi barabara zetu na bei yake haiwezi kufika hata 100milioni na consumption ya mafuta ni nzuri kabisa..
Tuwe wazalendo wakweli sasa na tuanze kutumia Defender 110 na viongozi wetu sasa ifikie mahala kama wanaziara isiyozidi 300KM basi wajiendeshe wenyewe.

Huu uzalendo sasa uwe kwa vitendo na uhusishe watu wote..
 
.
Screenshot_20200224-201111.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom