Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,600
- 35,158
Lakini USA ambao sio marafiki wenu ndio wanawapa condoms, wanawajengea vyoo, ARV, vyandarua bila kisahau ujenzi wa barabara!!China ni marafiki zetu wa enzi na enzi na kwa sasa wanajitanua zaidi duniani na wanaoushawishi mkubwa kuliko USA. Hawanaga kazi mbovu
Hivi Mordi si aliahidi kuwa watanunua tani kwa tani za choroko, dengu, korosho n.k?.....sijui ni kiasi gani imefikiwa.
Ungetuambia huyo aliyesema amepata masharti nafuu, pengine tungeangalia hayo masharti. Kumbuka JPM wakati wa awamu ya 5 alichukua mkopo kutoka India kwa masharti nafuu. India wana reserve kubwa ya forex na walikubali kuweka riba ya chini kidogo. Sina details lakini kumbuka Waziri mkuu wa India alitembelea Tanzania wakati ule.
Bagamoyo port haikuwa loan ilikuwa ni FDIKenya ameingia mkenge, hakujua janja ya China. Hata mradi wa kujenga Bagamoyo port kama tungeukubali bila marekebisho ndio ungekuwa mbaya sana kama utumwa mamboleo. Na sisi tukiendekeza misifa ya kujenga miradi mikubwa bila uchambuzi yakinifu na baadae kukwama kifedha na kuja kutegemea China, kuna uwezekano wa kushindwa kulipa.
China ya sasa siyo China ya Mao na rafiki yake Nyerere. Kumbuka siku hizo China ilikuwa imetengwa na dunia, ikatumia urafiki wake na Tanzania ya Nyerere kujitangaza kwa kutupa misaada mikubwa ya Mawasiliano, Uchukuzi, Kijeshi, viwanda, Afya, Utamaduni, Elimu, Kilimo n.k
China ya sasa ipo kileleni kiuchumi kwa kutumia njia hizo hizo za mabeberu tena kwa ujanja zaidi. Labda Raisi Magufuli ana jibu kama alivyogundua udhahifu kwenye mradi wa Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uliokuwa ukisifiwa na kupigiwa upatu na Spika Ndugai.
Kabisa aisee kama yutong zilivyo bora kuliko scania au foton zilivyo imara kuliko hilux vigo!!!China ni marafiki zetu wa enzi na enzi na kwa sasa wanajitanua zaidi duniani na wanaoushawishi mkubwa kuliko USA. Hawanaga kazi mbovu
Hayo ndio masharti?Masharti yake ni kama vile Wachina wanavyodaiwa kuchukua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka kutokana na nchi hiyo kushindwa kulipa madeni. Pia China imechukua Shirika la Umeme Zambia (ZESCO) na Shirika la Habari Zambia (ZNBC).
Sawa je mashrti nafuu toka China ni yapi?Kenya ameingia mkenge, hakujua janja ya China. Hata mradi wa kujenga Bagamoyo port kama tungeukubali bila marekebisho ndio ungekuwa mbaya sana kama utumwa mamboleo. Na sisi tukiendekeza misifa ya kujenga miradi mikubwa bila uchambuzi yakinifu na baadae kukwama kifedha na kuja kutegemea China, kuna uwezekano wa kushindwa kulipa.
China ya sasa siyo China ya Mao na rafiki yake Nyerere. Kumbuka siku hizo China ilikuwa imetengwa na dunia, ikatumia urafiki wake na Tanzania ya Nyerere kujitangaza kwa kutupa misaada mikubwa ya Mawasiliano, Uchukuzi, Kijeshi, viwanda, Afya, Utamaduni, Elimu, Kilimo n.k
China ya sasa ipo kileleni kiuchumi kwa kutumia njia hizo hizo za mabeberu tena kwa ujanja zaidi. Labda Raisi Magufuli ana jibu kama alivyogundua udhahifu kwenye mradi wa Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uliokuwa ukisifiwa na kupigiwa upatu na Spika Ndugai.
Kwahivo kwanini China inataka tusihoji mambo hayo?Masharti nafuu ni kutokuhoji demokrasia na Utawala bora. Masharti magumu ni kuhoji mambo ya demokrasia na Utawala bora.
Lipi Bora sasaUsharti nafuu wa Kichina ninaoujua na ambao nimejaribu Kuufuatilia ni Kukujengea haraka nchi yako, ila Wao Kuchukua Rasilimali zako Miaka 100.
Sasa bora lipi mkuuMkuu 'Falcon'
Baadhi ya masharti nafuu wanayoyapenda watawala wetu ni baadhi ya haya:
1. Wasiambiwe kwamba wanawanyima haki watu wao.
2. Wakiua kiasi kadhaa ya watu wao, wasihojiwe na yeyote kwa kisingizio cha kuingiliwa mambo yao ya ndani
3. Mkubwa akiamua kuharibu mazingira kwa kuweka mradi wake anaoupenda, asibughudhiwe na mtu, kwa vile uamzi wake ndio wa mwisho
4. Mambo ya riba na masharti mengine ya muda wa kulipa, wao hayo huwa sio masharti wanayoona kuwa na ugumu kama hayo matatu ya mwanzo
Lakini, ili nisionekane kuwa nina upendeleo wa upande mmoja:
Hata hao watoa mikopo nao kweli huwa wanayo matatizo yao. IMF au WB wanakupa mkopo wenye riba ya 0.5%, kwa muda wa miaka 30 kurudisha mkopo, lakini wanakurundikia masharti ambayo wakati mwingine huwa magumu kuyakubali, kama alivyoshindwa kuyakubali Mwalimu Nyerere wakati wake.
China wao wanakwambia hawataingilia mambo yako; kama unataka kuwachinja watu wako kwa kitoweo, hilo ni shauri lako, mradi pesa yao na faida irudi.
Umenifurahisha sana.Natamani kila awamu ingekuwa inalipa madeni ya mikopo yake waliyokopa kabla muda wao wa kuondoka madarakani haujafika, tungeheshimiana vizuri sana.
Aisee mbona umegusa kila angle?Hakuna mtu mbaya kama mchina linapokuja suala la mahusiano ya kiuchumi.
Wazungu waneikopesha Afrika miaka na miaka. Nchi nyingi za Afrika (Tanzania mojawapo) zikashindwa kulipa. Lakini haijawahi kutokea mataifa hayo ya wazungu kuchukua bandari au viwanja vya ndege kama wanavyofanya Wachina ukichelewa/kushindwa kulipa deni.
Mataifa ya wazungu yamekwishazifutia nchi nyingi za Afrika madeni lakini China haijawahi kuisamehe deni nchi yoyote Duniani.
Watawala wa Afrika wanawachukia wazungu kwa sababu sharti kubwa la kupata mkopo au msaada ni kuheshimu haki za binadamu na misingi ya demokrasia. Watawala wa Afrika, wengi wao ni madikteta wanaotaka kuwagandamiza raia wao, na wanaotaka kuendelea kutawala hata bila ya kuchaguliwa. Wanampenda mchina kwa sababu na yeye utawala wake ni wa kidikteta, na jamii ya Wachina kwa kiasi kikubwa ni primitive na inayokumbatia utawala primitive sawa na tawala nyingi za Afrika.
Wachina wamejaa Zimbabwe, kwa sababu dikteta Mugabe baada ya kupewa kisogo na mataifa ya Ulaya, aliona aheri amkumbatie dikteta mwenzake, mchina, akitarajia atamsaidia, lakini akaishia kwenye aibu kubwa ya kiuchumi. Hakuna nchi duniani iliyoachana na Dunia, ikamkumbatia mchina, halafu ikapata maendeleo.
Wachina walimdanganya Magufuli kuwa wataigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda, wakawa wanajenga tu uwigo wa mabati, halafu wanamwita Magufuli akaweje jiwe la msingi. Maeneo mengi mbao zilizoshikilia hayo mabati zinazidi kuoza na mabatai kulala chini. Ikamlazimu Magufuli aache kabisa kuongelea tena Tanzania ya viwanda. Hana hamu nao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimecheka sanaNina uhakika hata ukiwahoji hao Viongozi hawana jibu lolote kusema ni China ina unafuu gani.
Sifahamu wananunua kiasi gani, lakini ni rahisi sana kuangalia/check na Wizara, watakuwa na figures za mauzo ya mwaka jana na huu unaoisha.Hivi Mordi si aliahidi kuwa watanunua tani kwa tani za choroko, dengu, korosho n.k?.....sijui ni kiasi gani imefikiwa.
China hajihusishi na siasa zenu za maji taka!! Yeye anausongo na maliasili zenu tu; akizipata hizo basi!!Mchina sio poa, hafanyi biashara kwa hasara.
Mkuu unafaidika vipi na kutujazia uongo mrefu namna hii hapa?Hakuna mtu mbaya kama mchina linapokuja suala la mahusiano ya kiuchumi.
Wazungu waneikopesha Afrika miaka na miaka. Nchi nyingi za Afrika (Tanzania mojawapo) zikashindwa kulipa. Lakini haijawahi kutokea mataifa hayo ya wazungu kuchukua bandari au viwanja vya ndege kama wanavyofanya Wachina ukichelewa/kushindwa kulipa deni.
Mataifa ya wazungu yamekwishazifutia nchi nyingi za Afrika madeni lakini China haijawahi kuisamehe deni nchi yoyote Duniani.
Watawala wa Afrika wanawachukia wazungu kwa sababu sharti kubwa la kupata mkopo au msaada ni kuheshimu haki za binadamu na misingi ya demokrasia. Watawala wa Afrika, wengi wao ni madikteta wanaotaka kuwagandamiza raia wao, na wanaotaka kuendelea kutawala hata bila ya kuchaguliwa. Wanampenda mchina kwa sababu na yeye utawala wake ni wa kidikteta, na jamii ya Wachina kwa kiasi kikubwa ni primitive na inayokumbatia utawala primitive sawa na tawala nyingi za Afrika.
Wachina wamejaa Zimbabwe, kwa sababu dikteta Mugabe baada ya kupewa kisogo na mataifa ya Ulaya, aliona aheri amkumbatie dikteta mwenzake, mchina, akitarajia atamsaidia, lakini akaishia kwenye aibu kubwa ya kiuchumi. Hakuna nchi duniani iliyoachana na Dunia, ikamkumbatia mchina, halafu ikapata maendeleo.
Wachina walimdanganya Magufuli kuwa wataigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda, wakawa wanajenga tu uwigo wa mabati, halafu wanamwita Magufuli akaweje jiwe la msingi. Maeneo mengi mbao zilizoshikilia hayo mabati zinazidi kuoza na mabatai kulala chini. Ikamlazimu Magufuli aache kabisa kuongelea tena Tanzania ya viwanda. Hana hamu nao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Stori yako haiendani na uhalisiaHakuna mtu mbaya kama mchina linapokuja suala la mahusiano ya kiuchumi.

Ukiniambia nichague kati ya unafuu wa masharti ya "kuuliwa" na kupewa masharti hayo mengine..., hebu nisaidie kuchagua lililo "bora" hapo!Sasa bora lipi mkuu
Masharti nafuu kwa China ni kwamba utapata mkopo bila vizingiti, faster faster.na kwa riba ndogo.Sawa je mashrti nafuu toka China ni yapi?