Hakuna mtu mbaya kama mchina linapokuja suala la mahusiano ya kiuchumi.
Wazungu waneikopesha Afrika miaka na miaka. Nchi nyingi za Afrika (Tanzania mojawapo) zikashindwa kulipa. Lakini haijawahi kutokea mataifa hayo ya wazungu kuchukua bandari au viwanja vya ndege kama wanavyofanya Wachina ukichelewa/kushindwa kulipa deni.
Mataifa ya wazungu yamekwishazifutia nchi nyingi za Afrika madeni lakini China haijawahi kuisamehe deni nchi yoyote Duniani.
Watawala wa Afrika wanawachukia wazungu kwa sababu sharti kubwa la kupata mkopo au msaada ni kuheshimu haki za binadamu na misingi ya demokrasia. Watawala wa Afrika, wengi wao ni madikteta wanaotaka kuwagandamiza raia wao, na wanaotaka kuendelea kutawala hata bila ya kuchaguliwa. Wanampenda mchina kwa sababu na yeye utawala wake ni wa kidikteta, na jamii ya Wachina kwa kiasi kikubwa ni primitive na inayokumbatia utawala primitive sawa na tawala nyingi za Afrika.
Wachina wamejaa Zimbabwe, kwa sababu dikteta Mugabe baada ya kupewa kisogo na mataifa ya Ulaya, aliona aheri amkumbatie dikteta mwenzake, mchina, akitarajia atamsaidia, lakini akaishia kwenye aibu kubwa ya kiuchumi. Hakuna nchi duniani iliyoachana na Dunia, ikamkumbatia mchina, halafu ikapata maendeleo.
Wachina walimdanganya Magufuli kuwa wataigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda, wakawa wanajenga tu uwigo wa mabati, halafu wanamwita Magufuli akaweje jiwe la msingi. Maeneo mengi mbao zilizoshikilia hayo mabati zinazidi kuoza na mabatai kulala chini. Ikamlazimu Magufuli aache kabisa kuongelea tena Tanzania ya viwanda. Hana hamu nao.
Sent using
Jamii Forums mobile app