Masharti nafuu tunayopewa na China

Masharti nafuu tunayopewa na China

China ni marafiki zetu wa enzi na enzi na kwa sasa wanajitanua zaidi duniani na wanaoushawishi mkubwa kuliko USA. Hawanaga kazi mbovu
Lakini USA ambao sio marafiki wenu ndio wanawapa condoms, wanawajengea vyoo, ARV, vyandarua bila kisahau ujenzi wa barabara!!

Na zaidi ya yote ndiye aliye tengeneza simu anayotumia magufuli.
 
Ungetuambia huyo aliyesema amepata masharti nafuu, pengine tungeangalia hayo masharti. Kumbuka JPM wakati wa awamu ya 5 alichukua mkopo kutoka India kwa masharti nafuu. India wana reserve kubwa ya forex na walikubali kuweka riba ya chini kidogo. Sina details lakini kumbuka Waziri mkuu wa India alitembelea Tanzania wakati ule.

Hivi Mordi si aliahidi kuwa watanunua tani kwa tani za choroko, dengu, korosho n.k?.....sijui ni kiasi gani imefikiwa.
 
Kenya ameingia mkenge, hakujua janja ya China. Hata mradi wa kujenga Bagamoyo port kama tungeukubali bila marekebisho ndio ungekuwa mbaya sana kama utumwa mamboleo. Na sisi tukiendekeza misifa ya kujenga miradi mikubwa bila uchambuzi yakinifu na baadae kukwama kifedha na kuja kutegemea China, kuna uwezekano wa kushindwa kulipa.

China ya sasa siyo China ya Mao na rafiki yake Nyerere. Kumbuka siku hizo China ilikuwa imetengwa na dunia, ikatumia urafiki wake na Tanzania ya Nyerere kujitangaza kwa kutupa misaada mikubwa ya Mawasiliano, Uchukuzi, Kijeshi, viwanda, Afya, Utamaduni, Elimu, Kilimo n.k

China ya sasa ipo kileleni kiuchumi kwa kutumia njia hizo hizo za mabeberu tena kwa ujanja zaidi. Labda Raisi Magufuli ana jibu kama alivyogundua udhahifu kwenye mradi wa Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uliokuwa ukisifiwa na kupigiwa upatu na Spika Ndugai.
Bagamoyo port haikuwa loan ilikuwa ni FDI
 
China ni marafiki zetu wa enzi na enzi na kwa sasa wanajitanua zaidi duniani na wanaoushawishi mkubwa kuliko USA. Hawanaga kazi mbovu
Kabisa aisee kama yutong zilivyo bora kuliko scania au foton zilivyo imara kuliko hilux vigo!!!
 
Kati ya mtu wa kuwa waangalifu naye duniani ni Mchina!!

Mchina bwana hakatai dili...na hamshindwani bei..hata ukitaka daraja ajenge kwa buku atalijenga tu. 😀😀😀
 
Masharti yake ni kama vile Wachina wanavyodaiwa kuchukua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka kutokana na nchi hiyo kushindwa kulipa madeni. Pia China imechukua Shirika la Umeme Zambia (ZESCO) na Shirika la Habari Zambia (ZNBC).
Hayo ndio masharti?
 
Kenya ameingia mkenge, hakujua janja ya China. Hata mradi wa kujenga Bagamoyo port kama tungeukubali bila marekebisho ndio ungekuwa mbaya sana kama utumwa mamboleo. Na sisi tukiendekeza misifa ya kujenga miradi mikubwa bila uchambuzi yakinifu na baadae kukwama kifedha na kuja kutegemea China, kuna uwezekano wa kushindwa kulipa.

China ya sasa siyo China ya Mao na rafiki yake Nyerere. Kumbuka siku hizo China ilikuwa imetengwa na dunia, ikatumia urafiki wake na Tanzania ya Nyerere kujitangaza kwa kutupa misaada mikubwa ya Mawasiliano, Uchukuzi, Kijeshi, viwanda, Afya, Utamaduni, Elimu, Kilimo n.k

China ya sasa ipo kileleni kiuchumi kwa kutumia njia hizo hizo za mabeberu tena kwa ujanja zaidi. Labda Raisi Magufuli ana jibu kama alivyogundua udhahifu kwenye mradi wa Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo uliokuwa ukisifiwa na kupigiwa upatu na Spika Ndugai.
Sawa je mashrti nafuu toka China ni yapi?
 
Mkuu 'Falcon'

Baadhi ya masharti nafuu wanayoyapenda watawala wetu ni baadhi ya haya:

1. Wasiambiwe kwamba wanawanyima haki watu wao.

2. Wakiua kiasi kadhaa ya watu wao, wasihojiwe na yeyote kwa kisingizio cha kuingiliwa mambo yao ya ndani

3. Mkubwa akiamua kuharibu mazingira kwa kuweka mradi wake anaoupenda, asibughudhiwe na mtu, kwa vile uamzi wake ndio wa mwisho

4. Mambo ya riba na masharti mengine ya muda wa kulipa, wao hayo huwa sio masharti wanayoona kuwa na ugumu kama hayo matatu ya mwanzo

Lakini, ili nisionekane kuwa nina upendeleo wa upande mmoja:
Hata hao watoa mikopo nao kweli huwa wanayo matatizo yao. IMF au WB wanakupa mkopo wenye riba ya 0.5%, kwa muda wa miaka 30 kurudisha mkopo, lakini wanakurundikia masharti ambayo wakati mwingine huwa magumu kuyakubali, kama alivyoshindwa kuyakubali Mwalimu Nyerere wakati wake.

China wao wanakwambia hawataingilia mambo yako; kama unataka kuwachinja watu wako kwa kitoweo, hilo ni shauri lako, mradi pesa yao na faida irudi.
Sasa bora lipi mkuu
 
Hakuna mtu mbaya kama mchina linapokuja suala la mahusiano ya kiuchumi.

Wazungu waneikopesha Afrika miaka na miaka. Nchi nyingi za Afrika (Tanzania mojawapo) zikashindwa kulipa. Lakini haijawahi kutokea mataifa hayo ya wazungu kuchukua bandari au viwanja vya ndege kama wanavyofanya Wachina ukichelewa/kushindwa kulipa deni.

Mataifa ya wazungu yamekwishazifutia nchi nyingi za Afrika madeni lakini China haijawahi kuisamehe deni nchi yoyote Duniani.

Watawala wa Afrika wanawachukia wazungu kwa sababu sharti kubwa la kupata mkopo au msaada ni kuheshimu haki za binadamu na misingi ya demokrasia. Watawala wa Afrika, wengi wao ni madikteta wanaotaka kuwagandamiza raia wao, na wanaotaka kuendelea kutawala hata bila ya kuchaguliwa. Wanampenda mchina kwa sababu na yeye utawala wake ni wa kidikteta, na jamii ya Wachina kwa kiasi kikubwa ni primitive na inayokumbatia utawala primitive sawa na tawala nyingi za Afrika.

Wachina wamejaa Zimbabwe, kwa sababu dikteta Mugabe baada ya kupewa kisogo na mataifa ya Ulaya, aliona aheri amkumbatie dikteta mwenzake, mchina, akitarajia atamsaidia, lakini akaishia kwenye aibu kubwa ya kiuchumi. Hakuna nchi duniani iliyoachana na Dunia, ikamkumbatia mchina, halafu ikapata maendeleo.

Wachina walimdanganya Magufuli kuwa wataigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda, wakawa wanajenga tu uwigo wa mabati, halafu wanamwita Magufuli akaweje jiwe la msingi. Maeneo mengi mbao zilizoshikilia hayo mabati zinazidi kuoza na mabatai kulala chini. Ikamlazimu Magufuli aache kabisa kuongelea tena Tanzania ya viwanda. Hana hamu nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee mbona umegusa kila angle?
 
china ina mahesabu makali kwenye huo mkopo wa masharti nafuu
anyway wacha tuone vile tutaambiwa
 
Hivi Mordi si aliahidi kuwa watanunua tani kwa tani za choroko, dengu, korosho n.k?.....sijui ni kiasi gani imefikiwa.
Sifahamu wananunua kiasi gani, lakini ni rahisi sana kuangalia/check na Wizara, watakuwa na figures za mauzo ya mwaka jana na huu unaoisha.
 
Hakuna mtu mbaya kama mchina linapokuja suala la mahusiano ya kiuchumi.

Wazungu waneikopesha Afrika miaka na miaka. Nchi nyingi za Afrika (Tanzania mojawapo) zikashindwa kulipa. Lakini haijawahi kutokea mataifa hayo ya wazungu kuchukua bandari au viwanja vya ndege kama wanavyofanya Wachina ukichelewa/kushindwa kulipa deni.

Mataifa ya wazungu yamekwishazifutia nchi nyingi za Afrika madeni lakini China haijawahi kuisamehe deni nchi yoyote Duniani.

Watawala wa Afrika wanawachukia wazungu kwa sababu sharti kubwa la kupata mkopo au msaada ni kuheshimu haki za binadamu na misingi ya demokrasia. Watawala wa Afrika, wengi wao ni madikteta wanaotaka kuwagandamiza raia wao, na wanaotaka kuendelea kutawala hata bila ya kuchaguliwa. Wanampenda mchina kwa sababu na yeye utawala wake ni wa kidikteta, na jamii ya Wachina kwa kiasi kikubwa ni primitive na inayokumbatia utawala primitive sawa na tawala nyingi za Afrika.

Wachina wamejaa Zimbabwe, kwa sababu dikteta Mugabe baada ya kupewa kisogo na mataifa ya Ulaya, aliona aheri amkumbatie dikteta mwenzake, mchina, akitarajia atamsaidia, lakini akaishia kwenye aibu kubwa ya kiuchumi. Hakuna nchi duniani iliyoachana na Dunia, ikamkumbatia mchina, halafu ikapata maendeleo.

Wachina walimdanganya Magufuli kuwa wataigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda, wakawa wanajenga tu uwigo wa mabati, halafu wanamwita Magufuli akaweje jiwe la msingi. Maeneo mengi mbao zilizoshikilia hayo mabati zinazidi kuoza na mabatai kulala chini. Ikamlazimu Magufuli aache kabisa kuongelea tena Tanzania ya viwanda. Hana hamu nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unafaidika vipi na kutujazia uongo mrefu namna hii hapa?
 
Stori yako haiendani na uhalisia
Screenshot_20201230-073054.png
 
Sawa je mashrti nafuu toka China ni yapi?
Masharti nafuu kwa China ni kwamba utapata mkopo bila vizingiti, faster faster.na kwa riba ndogo.
Lakini kwa undani ukishindwa kulipa atakupa mbadala wake.Na huo mbadala atataka kitu kinachokuigizia faida amilikishwe yeye.
Kukopa harusi kulipa matanga
 
Back
Top Bottom