Tetesi: Masharti ya mikopo yameikumba Tanzania, kupata mkopo sharti Makamu wa Rais atokee upinzani

Kisamv,

Upinzani una hype kubwa maeneo ya mijini, ambapo pia CCM wanawafuasi wao na sio kidogo. Hivyo mjini ndio sehemu pekee wapinzani wanaweza kumenyana na CCM kwenye sanduku la kura. Ukitoka maeneo ya nje ya mji kidogo tu, watu huwaambii kitu kuhusu CCM. Wapinzani hawana wagombea wa kutosha wenye uwezo wa kuleta ushindani maeneo yote, isipokua tu wanajitahidi sana kuleta vurugu maaeneo ya majini maana ndio sehemu wamechagua kujenga taswira ya vyama vyao. Nikiangalia chama kikuu cha upinzani kwa karibu huwa najiuliza kwanini mwenyekiti habadiliki?, ni kwamba chama hakina imani na wanachama wengine? au ndio tuseme chama hakina mwenye ushawishi kama yeye? au labda yeye ndiye mwenye akili na nguvu kuliko mtu mwingine kwenye chama.

Huwezi kukiamini chama ambacho hakiamini katika misingi ya kidemokrasia, chama ambacho kinategemea mtu mmoja tu, ni hatari kwa maendeleo ya nchi. Upinzani bado sana Tanzania, inabidi wajipange.
 
Blessings in the disguise!

Ila kama Katiba ni hii hii utabadilisha chama na watu mambo yatabaki vile vile...Uzuri ni kuwa tutaondoa baadhi ya watu wnaaodhani wao ni royal families
 
Blessings in the disguise!

Ila kama Katiba ni hii hii utabadilisha chama na watu mambo yatabaki vile vile...Uzuri ni kuwa tutaondoa baadhi ya watu wnaaodhani wao ni royal families
Nafuu ya maisha inaonekana. Niliwahi kusafiri wakati wa mvua kwa roli na maiti ya mfanyakazi mwenzetu kutoka Dodoma Jumapili jioni tukafika Musoma Jumatano asubuhi wakati tulikuwa tunasafiri usiku na mchana. Sasa hivi Dodoma Musoma hata saa 10 hazifiki
 
Hatuwezi kuongozwa na chadema ng'o sisi sio wendawazimu..

Haitokuja tokea labda waunde chama kipya .
 
Hii itakuwa shida kwa upande mmoja, na sio shida kwa upande mwingine.

Shida itakuwa ni kukubali kuingiliwa na mabeberu. Hilo ni jambo baya zaidi linalofanana na lile la Rais kukubali kuchanjwa ili apate mikopo ya mabeberu.

Haitakuwa shida kwa kuwa vyama vya upinzani vipo vingi, na CCM haitashindwa kutengeneza pandikizi la kuliteua.

Lakini ajenda kuu ya jambo kama hili itakuwa ni kwa mabeberu kuendelea kutudhalilisha. Na pia watafanya mpango wa kumuua Rais wa CCM siku moja ili mpinzani achukuwe nchi.

Wameshatusoma kuwa tunaheshimu katiba ndo maana sasa hivi tunaongozwa na mwanamke. Katika hali ya kawaida mwanamke asingeweza kuwa Rais wa Tanzania hata ipite miak 100.

Sasa wanataka kutuingilia zaidi na kutuvuruga kabisa.

Demokrasia wanayopigia kelele wazungu haina maana sana kwetu sisi, zaidi ya kwao wao. Kwao itawasaidia sana kutuvuruga wakati wowote wakitaka kwa kumpa hela mtu wanayemtaka awe kiongozi wetu.
 
Reactions: Ame
Hao mabeberu si wanatumia akili? Kwanini na sisi tusitumie akili ili siku za usoni watuheshimu?
Tatizo wao wanatumia akili, sisi tunatumia matumbo yetu kulinganisha matakwa yao na yetu...Hapo ndipo tunapoingia chaka
 
Tanzania haijawahi kuongozwa kwa amri kutoka Bretton woods institutions, 10 downing street, Washington au Brussels. Ni msingi ulijengwa na Mwalimu Nyerere na Mzee Karume. Tanzania inaheshimu mataifa yote duniani lakini msingi wa Uhuru wetu hatuingiliwi katika siasa zetu za ndani. #Tujadili mambo yetu kama Watanzania tusilete vitisho vya kuingiza wazungu.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kwa nguvu zipi ulizonazo za kuwapinga mabeberu mkuu!
 
We kisamvu ha kopo kweli yaani maisha yako yote unategemea serikali ndiyo ikuletee nafuu ya maisha waache kupeleka nafuu ya maisha kwao
 
Tatizo kuna mashimo yameshatobolewa ambamo panya wanaingia na kutoka
 
Kwa nguvu zipi ulizonazo za kuwapinga mabeberu mkuu!
Hatuwezi kuwapinga na wao hawawezi kutulazimisha au kutuamrisha. Diplomasia ni kuheshimiana. πŸ™πŸ™πŸ™
 
Mikopo ni initiative ya beberu mwenyewe kuzikamata masikio nchi maskini, kwa hiyo hakuna jipya hapo....
 
Haiwezi kusaidia chochote. Zenj makamu wa Rais ni uponzani imewasaidiaje hadi sasa?
 
Ni habari njema Sana hii kama itakuwa ya kweli
inategemea huyo mpinzani kuwa makamu wa raisi personal integrity yake ipo gado kiasi niga. kama alikuwa hana makochi kwao usitegemee atakujua wewe bila kutafuta makochi kwanza! wewe pigania katiba ya israel imtingishayo mtawala kama netanyahu mahakamani itutawale utaona uhondo !hao watoa mikopo wasisitishe mikopo mpaka nchi zote za africa ziwe na katiba imshitakiwayo raisi. hapo watatuokoa waafrica! wapulika iwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…