Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
- Thread starter
- #121
Labda ukweli unaoukataa ni kwamba nchi yako mwenyewe ilikuwa ikitumia sheria hii. Wakati mimi ninazaliwa utaratibu ulikuwa hivyo, sema leo hii wanadamu wamebadili mfumo wa ndoa, ndio maana kuna thread nyingi humu za kulia lia tu kuhusu ndoa hata isieleweke chanzo ni nini.Huyu Shehe na wenzake wakaombe uraia kwenye nchi zinazofuata sharia za dini ya Kiislamu kwa Tanzania haiwezekani na haitatokea, kikatiba ni nchi isiyofungamana na dini yoyote ile na analijua hilo tumuombe Mwenyezi Mungu na Serikali yetu tukufu kwa kulitambua jambo hili muhimu tangu mwanzo kwa ustawi wa taifa letu, mwisho (amani yetu bado tunaipenda).
Hawa mashehe wala hawahitaji kuhama nchi kama unavyotamani iwe, wametumia uhuru wao wa kikatiba kutoa maoni yaombele ya tume halali kabisa iliyoundwa kukusanya maoni kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.
Pia huo mustakabali unaousema ni upi? Labda unieleweshe hilo kwanza, mustakabali wa taifa letu ni upi? Kumbuka baada ya kufungwa sheria ya elimundipo na masomo ya afya ya uzazi yakaanza kwa sababu vibinti vinabalehe vikiwa mashuleni halafu vinajiingiza kwenye mapenzi. Tena leo hii ukimpa mimba mwanafunzi adhabu yake ni miaka 30 jela, unadhani hawa mabinti wanabakwa? Halafu baada ya sheria hii kufeli kutatua tatizo tumegeukia kudai binti akishajifungua arudI shuleni kuendelea na masomo, kwa nini apate mimba wakati ni MTOTO?
Huku wanauana kwa KUTETEA HAKI ZA MTOTO halafu wanaandaa mazingira ya WATOTO HAO kuzalia mashuleni!! Huoni huu nao ni mkanganyiko mkubwa? Kuna haja ya kufafanua sheria ya kumlinda mtoto wa kike inakusudia kumlinda dhidi ya nini? Kama na kujamiiana hilo halipo na limekubalika kwenye jamii. Kitu pekee inachosimamia sheria hii ni HAKI YA KUPATA ELIMU basi. Kwamba binti ana hak8 ya kupata elimu na kuwa na maisha yake mwenyewe, sio vinginevyo.
Huku kuna wadau wanadai waache mabinti wafanywe na watoto wenzao, hebu tazama fikra hizo!! Kwa nini mtoto wa kike alihitaji usimamizi? Sababu kuu ni kwamba thamani ya mwanamke inashuka kwa 1. Umri 2. Vitendo vya ngono. Mwanamume thamani yake inapanda kadri siku zinavyokwenda akiwa anajijengea mazingira mazuri. Leo hii binti anafundishwa kupandisga thamani yake kwa njia ya elimu pamoja na mambo mengine yatakayomfanya atambulike kwenye jamii (kuwa staa). Sasa mifumo hii yote IMEFELI PAKUBWA lijapo suala la ndoa, asilimia kubwa ya wanawake wa namna hii hawafit kwenye mfumo wa ndoa, ndio sababu vilio vya ndoa hivi sasa vimetamalaki!!
Najua ni ngumu sana kueleza haya ukaeleweka, lakini Mungu alipomuumba mwwnamke alimpangia majukumu yake kama ilivyokuwa kwa mwanamke.