Wewe usilete mambo ya ndoa kwenye uongozi wa nchi.
Wanawachuoni ni warithi wa mitume na wamezisherehesha hadith na kuzi backup na aya za quran kama una ushahidi kinyume na hapo unaotokana na vyanzo hivyo viwili (quran na sahihi hadith) unaweza pia kuviweka hapa utuelimishe navyo .
kwanza unatakiwa kujua hadith aliyoitoa huyo shaikh ni sahihi na mtume muhammad (amani iwe juu yake) aliitoa pindi alipoletewa habari na abubakar(radhi ziwe juu yake ) kwamba ufalme wa irani ( kwa muda ule sassanid empire) uliwachagua watoto wa kike wa mfalme khosrow II (aliyekuwa amekufa) .kwa majina azarmidokhti khosrow na borandukhti(boran) khosrow kuwa viongozi wa juu ( yaani queens) .
Hivyo kama aligusia kuhusu uongozi wa kiserikali unadhani ndani ndo kuna mabadiliko? Jibu ni hakuna , halafu hakuna ikhtlafu baina ya ma'ulama kuhusiana na na hii ishu mbona.
na kingine mtume muhammad huwa hatamki ispokuwa ni wahyi kutoka kwa Allah (subhanna huwataal) kama Allah (the almighty) alivyotuambia kwenye surat najm.
An-Najm 53:3
وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلْهَوَىٰٓ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Wala hatamki kwa matamanio.
An-Najm 53:4
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْىٌ يُوحَىٰ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa;
.