Pre GE2025 Masheikh 12, waliokaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi waachiwa huru

Pre GE2025 Masheikh 12, waliokaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi waachiwa huru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndicho nachokueleza Kila mtu yanamkuta kwa aina yake, kipindi unasema hayo, wapo waliozingishiwa kuua wakakaa miaka 5 kama yule dogo wa Iringa, wapo wakina Mzee Kibao waliuouwawa wapo wakina Azory/Kaguye wote hao Kuna sababu wengine wakisema walishirikiana na Magaidi wa ikwilili. Kwahio Kila mtu asali kwa dini yake yasije yakamkuta.

Mimi nilitegemea Hawa Magaidi wahukumiwe kabisa miaka kibao, sasa kama wanakaa miaka 10 wanaachiwa kwa DPP kutokua na nia yakuendelea na kesi maana yake nini?. Hawa walitaka Zanzibar iwe nchi kamili ndio wakakutana na mkono wa chuma wote tunajua nini kilitokea. Hayo mengine unayoyasema ilikua watawala wenyewe Ili kwenye macho ya watu wapate sababu.

Masoko kibao yameungua lkn mpaka Leo hakuna aliyekamatwa, lakini wengi tunajua ni nn sababu yakuunguzwa masoko hayo. Kwahio kama ukiangushiwa mzigo huo raia wataamini hasa kama wajishughulisha na siasa. Mimi nachosema omba tu yasikukute au kumkuta ndugu yako.
Hiyo ndiyo kazi ya Serikali na vyombo vya dola. Huwezi kuita chombo cha dola halafu ukataka kiwe na reasoning kama ya madrassa. Hakuna kitu kama hicho duniani.
 
Cream ile yenyewe ilishapotezwa
Hii iloachiwa ni second layer
Suala la usalama wa taifa letu halifai kuchukuliwa kwa mahaba
Tuilinde Motherland kwa gharama yoyote ile
Ukiona mtu anashikwa kuna kitu sio bure
Makosa yapo ila hujulikana mapema tu kuna salafi walimfanansha wakamchukua baada ya week mbili ndevu zote sasa hataki
Tufunge saum tupate afya
 
Mimi nauliza wakuu kwa anayejua kwani waligaidi nini?? Haiwezekan mtu kukaa mahbusu hivi na hawakuwa na interest za kisiasa. Ugaidi wao walikua wanahusika vipi
 
Mimi nauliza wakuu kwa anayejua kwani waligaidi nini?? Haiwezekan mtu kukaa mahbusu hivi na hawakuwa na interest za kisiasa. Ugaidi wao walikua wanahusika vipi
Ndio swali wengi twajiuliza,hakuna aliyeweza kulijibu hadi sasa,ni bla bla tu,!!!,, kwanini isisemwe walifanya 1,2,3
 
Shura ya Maimamu Tanzania

KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 4/3/2025

MASHEIKH 12, WATOKA GEREZANI. WATANO NI FAMILIA MOJA YA ULATULE.

MASHEIKH 12, walio kaa gerezani miaka 10, (2015-2025), kwa tuhuma za Ugaidi wameachiwa huru leo. Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Kirekiano.

Kabla ya hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP, aliambia Mahakama upande wa Jamhuri hauna haja ya kuendelea tena na shauri hilo.

Akitoa uamuzi huo mheshimiwa jaji amesema amekubali ombi hilo la Mwendesha Mashtaka wa serikali.

Kwa muda mrefu Shura ya Maimamu Tanzania imekua ikimuomba Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kulifuta shauri hilo kwa sababu za upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi ya Masheikh hao.

Walioachiwa huru ni:

1. Ali Mohammed Ulatule (70).
2. Khamisi Mohammed Ulatule (61).
3. Nassoro Suleiman Ulatule (41),
4. Rajab Ali Mohammed Ulatule (34).
5. Na Ramadhani Khamisi Mohammed Ulatule (29).

Wengine ni:

6. Saidi Abdallah Chambeta.
7. Fadhili Shaabani Lukwembe.
8. Mnemo Qassim Mwatumbo.
9. Abdallah Bushiri kalukula.
10. Khamisi Ally Masamba.
11. Omari Abdallah Makota.
12. Na Mohammed Hassan Ungando.

Katika kundi la Masheikh walioachiwa leo, 5, ni wa familia moja ya Ulatule. Wao walikamatwa familia moja watu 16, na baada ya masiku kadhaa (ya kutofahamika walipo), hatimaye 7, walikutwa katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam baada ya kufikishwa Mahakamani na kusomewa shtaka la ugaidi.

Aidha wenzao 9, hawajulikani walipo mpaka leo. Kati ya 7, waliokua gerezani 2, Sheikh Suleima Mohammed Ulatule (99), na Sheikh Saidi Mohammed Ulatule (79), wamefariki dunia wakiwa gerezani.

Kufuatia kuachiwa kwa masheikh hao 12, idadi ya mahabusu wenzao waliobaki katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam ni 39.

Shura ya Maimamu Tanzania inawashukuru wale wote wanaoshiriki ipasavyo harakati za kutetea haki za binadamu.

=======================​

JamiiForums imewasiliana na Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kuhusu maamuzi hayo ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar, amesema

“Tunaendelea kuwasiliana na DPP kuhusu wale 39 waliosalia ndani, tumefanya hivyo kwa njia ya maandishi na hata Watuhumiwa wamekuwa wakiwasilisha maombi yao ya kutaka kesi ifutwe pia,

Ni mashauri ya muda mrefu n ahata hoja zinazotolewa hazina mashiko, zinakuwa nyepesi sana, mfano unakuta inaweza kupangwa mashahidi 70 watoe Ushahidi ndani ya wiki mbili lakini wanaotoa ushahidi unakuta ni wawili tu, hivyo inafanya kesi kwenda mwaka mzima bila kuwa na mwendelezo unaoeleweka.”
Inasemekana wamerudishwa tena ndani kwa kupewa kesi nyengine hili likovipi?
 
Soma nilichoandika, hoja yangu ni kutoelewa kama una ufahamu ulipaswa kunielewesha sio mabishano.
Hakuna fidia.
Wameshitakiwa kwa ugaidi, serikali imesema haina nia ya kuendelea na kesi, hivyo kesi haijasikilizwa, haimaanishi hao si magaidi ila tu hawana nia, so hawawezi kushitaki maana so far ni watuhumiwa na wanaweza rudishwa ndani kesi ikaanza upya.
Samahani lugha ya awali ilikuwa kali kidogo.
 
Shura ya Maimamu Tanzania

KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 4/3/2025

MASHEIKH 12, WATOKA GEREZANI. WATANO NI FAMILIA MOJA YA ULATULE.

MASHEIKH 12, walio kaa gerezani miaka 10, (2015-2025), kwa tuhuma za Ugaidi wameachiwa huru leo. Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Kirekiano.

Kabla ya hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP, aliambia Mahakama upande wa Jamhuri hauna haja ya kuendelea tena na shauri hilo.

Akitoa uamuzi huo mheshimiwa jaji amesema amekubali ombi hilo la Mwendesha Mashtaka wa serikali.

Kwa muda mrefu Shura ya Maimamu Tanzania imekua ikimuomba Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kulifuta shauri hilo kwa sababu za upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi ya Masheikh hao.

Walioachiwa huru ni:

1. Ali Mohammed Ulatule (70).
2. Khamisi Mohammed Ulatule (61).
3. Nassoro Suleiman Ulatule (41),
4. Rajab Ali Mohammed Ulatule (34).
5. Na Ramadhani Khamisi Mohammed Ulatule (29).

Wengine ni:

6. Saidi Abdallah Chambeta.
7. Fadhili Shaabani Lukwembe.
8. Mnemo Qassim Mwatumbo.
9. Abdallah Bushiri kalukula.
10. Khamisi Ally Masamba.
11. Omari Abdallah Makota.
12. Na Mohammed Hassan Ungando.

Katika kundi la Masheikh walioachiwa leo, 5, ni wa familia moja ya Ulatule. Wao walikamatwa familia moja watu 16, na baada ya masiku kadhaa (ya kutofahamika walipo), hatimaye 7, walikutwa katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam baada ya kufikishwa Mahakamani na kusomewa shtaka la ugaidi.

Aidha wenzao 9, hawajulikani walipo mpaka leo. Kati ya 7, waliokua gerezani 2, Sheikh Suleima Mohammed Ulatule (99), na Sheikh Saidi Mohammed Ulatule (79), wamefariki dunia wakiwa gerezani.

Kufuatia kuachiwa kwa masheikh hao 12, idadi ya mahabusu wenzao waliobaki katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam ni 39.

Shura ya Maimamu Tanzania inawashukuru wale wote wanaoshiriki ipasavyo harakati za kutetea haki za binadamu.

=======================​

JamiiForums imewasiliana na Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kuhusu maamuzi hayo ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar, amesema

“Tunaendelea kuwasiliana na DPP kuhusu wale 39 waliosalia ndani, tumefanya hivyo kwa njia ya maandishi na hata Watuhumiwa wamekuwa wakiwasilisha maombi yao ya kutaka kesi ifutwe pia,

Ni mashauri ya muda mrefu n ahata hoja zinazotolewa hazina mashiko, zinakuwa nyepesi sana, mfano unakuta inaweza kupangwa mashahidi 70 watoe Ushahidi ndani ya wiki mbili lakini wanaotoa ushahidi unakuta ni wawili tu, hivyo inafanya kesi kwenda mwaka mzima bila kuwa na mwendelezo unaoeleweka.”
warudi wakafanye ugaidi tena!nchi ya ovyo sana hii!watu wanafanya ugaidi, wanaua watu wasio na hatia halafu mnawaachia huru kweli!!?????
 
Back
Top Bottom