Pre GE2025 Masheikh 12, waliokaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi waachiwa huru

Pre GE2025 Masheikh 12, waliokaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi waachiwa huru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watu wanawatetea tu ila hao jamaa walistahiki kupotelea hukohuko na ole wao wajifanye kama wanajikuna
Watu wanashindwa kufatilia nini kilitokea Hadi wamefika hapo, Tena walikamatwa na Serikali ,Rais akiwa muislamu

Intelligence ipo makini , kuwashikilia miaka yote hiyo lazima Kuna jambo

Watu wa kivule wangekuja hapa kutupa mkasa zaidi
 
..kauli sahihi ni wameonewa na serikali ya Ccm.

..kuna Mashekhe walikamatwa wakati Raisi, na Igp, wakiwa Waislamu.

..wakati wa kampeni, mwanasiasa pekee aliyepanda jukwaani na kuwatetea Mashekhe wa Ansar Sunna alikuwa Tundu Lissu.

..pia Mheshimiwa Bwege alipokuwa mbunge aliwahi kuwasemea Waislamu waliopotezwa mikoa ya kusini.

..Tuiondoe CCM ili haki itawale ktk nchi yetu.
ishu sio CCM, ishu ni ugaidi
 
Shura ya Maimamu Tanzania

KUTOKA MAHAKAMA KUU LEO TAREHE 4/3/2025

MASHEIKH 12, WATOKA GEREZANI. WATANO NI FAMILIA MOJA YA ULATULE.

MASHEIKH 12, walio kaa gerezani miaka 10, (2015-2025), kwa tuhuma za Ugaidi wameachiwa huru leo. Uamuzi huo umetolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Kirekiano.

Kabla ya hukumu hiyo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP, aliambia Mahakama upande wa Jamhuri hauna haja ya kuendelea tena na shauri hilo.

Akitoa uamuzi huo mheshimiwa jaji amesema amekubali ombi hilo la Mwendesha Mashtaka wa serikali.

Kwa muda mrefu Shura ya Maimamu Tanzania imekua ikimuomba Mkurugenzi wa Mashtaka DPP kulifuta shauri hilo kwa sababu za upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi ya Masheikh hao.

Walioachiwa huru ni:

1. Ali Mohammed Ulatule (70).
2. Khamisi Mohammed Ulatule (61).
3. Nassoro Suleiman Ulatule (41),
4. Rajab Ali Mohammed Ulatule (34).
5. Na Ramadhani Khamisi Mohammed Ulatule (29).

Wengine ni:

6. Saidi Abdallah Chambeta.
7. Fadhili Shaabani Lukwembe.
8. Mnemo Qassim Mwatumbo.
9. Abdallah Bushiri kalukula.
10. Khamisi Ally Masamba.
11. Omari Abdallah Makota.
12. Na Mohammed Hassan Ungando.

Katika kundi la Masheikh walioachiwa leo, 5, ni wa familia moja ya Ulatule. Wao walikamatwa familia moja watu 16, na baada ya masiku kadhaa (ya kutofahamika walipo), hatimaye 7, walikutwa katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam baada ya kufikishwa Mahakamani na kusomewa shtaka la ugaidi.

Aidha wenzao 9, hawajulikani walipo mpaka leo. Kati ya 7, waliokua gerezani 2, Sheikh Suleima Mohammed Ulatule (99), na Sheikh Saidi Mohammed Ulatule (79), wamefariki dunia wakiwa gerezani.

Kufuatia kuachiwa kwa masheikh hao 12, idadi ya mahabusu wenzao waliobaki katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam ni 39.

Shura ya Maimamu Tanzania inawashukuru wale wote wanaoshiriki ipasavyo harakati za kutetea haki za binadamu.

=======================​

JamiiForums imewasiliana na Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda kuhusu maamuzi hayo ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar, amesema

“Tunaendelea kuwasiliana na DPP kuhusu wale 39 waliosalia ndani, tumefanya hivyo kwa njia ya maandishi na hata Watuhumiwa wamekuwa wakiwasilisha maombi yao ya kutaka kesi ifutwe pia,

Ni mashauri ya muda mrefu n ahata hoja zinazotolewa hazina mashiko, zinakuwa nyepesi sana, mfano unakuta inaweza kupangwa mashahidi 70 watoe Ushahidi ndani ya wiki mbili lakini wanaotoa ushahidi unakuta ni wawili tu, hivyo inafanya kesi kwenda mwaka mzima bila kuwa na mwendelezo unaoeleweka.”
Yaani hakuna nchi inayo endeshwa kihuni kama Tanzania chini ya ccm. Mtu unapotezea miaka 12 ya maisha yake halafu baada ya miaka 12 ya mateso unamwambia nenda nyumbani? Bila hata mjadala ! Hii sio sawa siku watanzania watakapo choke huu uhuni Tanzania itakuwa kama Samalia.
 
Yaani hakuna nchi inayo endeshwa kihuni kama Tanzania chini ya ccm. Mtu unapotezea miaka 12 ya maisha yake halafu baada ya miaka 12 ya mateso unamwambia nenda nyumbani? Bila hata mjadala ! Hii sio sawa siku watanzania watakapo choke huu uhuni Tanzania itakuwa kama Samalia.
akili za kigaidi hizi
 
je kama walishiriki kwa namna moja au nyingine ku facilitate hayo magaidi wataachwaje kukamatwa?
Halafu wakishakamatwa kinachofuata nini, kufungwa bila mashtaka na kuuliwa?

16 walikatwa kwenye famulia moja, 7 wakaletwa mahakamani, 9 hawakuletwa.

Unadhani hawa 9 walifanywaje ?

Kwa hiyo Kikwete ali sign death warrant tisa. On paper wanasema wa mwisho kunyonga ni Mwinyi. Na hawa 9 je, walisamehewa na Kikwete wakapaa mbinguni ?
 
Needless to say, the global problem of terror will be finished by the moslems themselves, if they decide to end it today they'll do so devoid of any hindrance because they are the architects.
 
Halafu wakishakamatwa kinachofuata nini, kufungwa bila mashtaka na kuuliwa?

16 walikatwa kwenye famulia moja, 7 wakaletwa mahakamani, 9 hawakuletwa.

Unadhani hawa 9 walifanywaje ?

Kwa hiyo Kikwete ali sign death warrant tisa. On paper wanasema wa mwisho kunyonga ni Mwinyi. Na hawa 9 je, walisamehewa na Kikwete wakapaa mbinguni ?
sababu ya kukamatwa kwao ni ugaidi. Swali hili jibu lake ni mukhtadha wa kukamatwa kwao
 
Sheria ya DDP hana nia ya kuendelea na kesi ni ya hovyo sana ni kama watu wapo kwenye ukoloni bado kwa nini anakuja na jia wakati alikua hana ushahidi wa kutosha kwenye sheria pana mapungufu sana ndio maana yale makampuni yakitudaka lazima tuwalipe na wanafungua kesi zao nje ya Nchi huko DPP anabaki kusoma kama sisi tu..
 
Or else watuhumiwa wanaotumia kama Hawa kwa kukaa rumande muda mrefu, ilihali wanaathirika kisaikolojia na kiuchumi, Walipwe fidia na dola.
Ukigombana na DPP tu anakutia ndani wewe gaidi unapigwa mvua baada ya miaka 10 anakuja mwingine anakuachia
 
Back
Top Bottom