Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 14,677
- 18,561
Wewe sio Mwislamu:Kwahiyo nifuate maneno yako sio maandiko?
Hiyo Aya uliyoleta Mungu anasema ukifa ukiwa kafiri(hujasilimu) akhera utakuwa ni mwenye hasara na sio duniani
Lete andiko linalosema mtu ambae sio muislam auawe na alipe kodi kutoka kwenye Qur'an
Sio wakristo wote wenye kuikubali hiyo novena na ni utaratibu ambao haupo kwenye biblia, kwahiyo kuhusishwa Mungu sio shida hata manabii feki wanamuhusisha Mungu tena katika nyumba ya Mungu ila wanatumia nguvu za giza huku wakimtaja Yesu.Ushahidi ni picha hizo ulizoleta!!!
sasa kosa la mganga kama sule kwenye field hii ni lipi??nimetaja wasomi wabobevu wa Quran na wao kuwa waganga,hiyo ni neema moja wapo ya Quran.
ukweli hauwezi kuwa ukweli kwa sababu wewe umedai ni ukweli,mpaka uwe ukweli wenyewe,ukweli wenyewe ni kwamba hakuna mganga anaagua na bible.
Kitendo tu cha Quran kukubali kutumika kwenye mabaya na mazuri ni neema pia.urogee au utibie ni saafi.
novena Mungu anahusishwa kabisa,hakuna tunguli wala kuchoma ubani na kunenea maneno ya ajabu ajabu.
Mada inazungumzia shirki na uchawi ni sehemu ya shirki, kwahiyo nachokiuliza ni ndani ya mada.Mada ya uchawi siku ile uliikimbia Leo tuachane nayo tuongelee shirki kama shirki yani kumshirikisha Mwenyezi Mungu na viumbe alivyoviumba
Lete hoja kiongozi
Majini walikuwepo kabla ya uislamu na binaadamu hili tunakubaliana wote, sasa kabla ya uislamu majini walikuwa dini gani?Kwa mujibu wa waislam allah ameumba majini na wanadamu ili wamuabudu kwa pamoja. Yani majini ni waislam na wamesilimu na kumuabudu allah
Ngoja nitarudi inshaalah,nina mengi hapo 👆👆Kuna hii tabia ambayo imeshakuwa mazoea kwa wengi wa masheikh wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kuchanganya dini na uganga au uchawi.
Utakuta mtu kasoma dini vizuri na ana elimu kubwa lakini badala ya kuitumia elimu hiyo katika kufanya mema na kuitafuta pepo ya Allah (S. W) huitumia kama kigezo cha kuaminika katika masuala ya kiuganga na kichawi jambo ambalo haliruhusiwi katika dini na ni shirki
Katika Surat mubayyina, Allah anasema baada ya Bismillah Arahman rahiim
98:1 - Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,
98:2 - Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika,
98:3 - Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka
98:5 - Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.
Katika aya hizo M/Mungu anasema waumini wote na masheikh hatujaamrishwa ila tuwe wema, tutoe zaka na kusali hayo ya uganga na ushirikina mmeyatoa wapi nyie masheikh nawauliza?
Mmeiharibu dini kiasi kuwa uislamu unaonekana ni dini ya wachawi na mila zingine potofu mlizokuwa nazo kabla hata hamkuujua huo uislamu wala elimu ya dini.
Kupitia andiko hili kama wewe ni Sheikh na una tabia hiyo iache mara moja na tubia kwa Mwenyezi Mungu haraka kabla kifo hakija kufika itakuwa ni khasara kwako siku ya kiyama
NB, tujadili kistaarabu
👍Hii mada haikuhusu kaa pembeni hatupo hapa kukejeli tupo hapa kufundishana kwa tusiyoyajua wewe na kejeli zako anzisha uzi wako
After all wewe sio miongoni mwa masheikh niliyowazungumzia hapa
uislam ni shrik tupu.Hivi ushirikina ni nini?
Kisa nimeomba andiko wanitoa hadi kwenye dini!Wewe sio Mwislamu:
Kwani Alshababu huwa wanafikia mikoa gani?
Kama sio Tanga Zanzibar Mtwara na Rufiji
Kama huijui Jazya tutaongea nini mimi na wewe ?Kisa nimeomba andiko wanitoa hadi kwenye dini!
Kama huna ushahidi usiwe mrahisi kuropoka ni busara ukakaa kimya kwa kitu ambacho hukijui au huna ushahidi nacho
Uchawi ni shirki hilo halina mjadala kwanzia waumini wake na watekelezaji wote ni washirikinaMada inazungumzia shirki na uchawi ni sehemu ya shirki, kwahiyo nachokiuliza ni ndani ya mada.
Wewe kama hauamini uchawi wala sio shida ni hiari yako ila umekubali kwamba kwenye imani ya uchawi kuna kumshirikisha Mungu, sasa mie nakuuliza sheikh wangu je kuna uchawi ambao haumshirikishi Mungu?
Maswali mazuri sana🤝je huyu Allah mwenye majina 99 anatofauti gani na Mungu wa kweli JEHOVA.???JE??huyu Allah ni NANI?
JE?ni kweli kuwa kuna MAJINI MAZURI/WEMA?
JE? ni kweli majini nayo yana muabudu MUNGU wa kweli?? au MAJINI yanamubudu mungu wao allah??
Je ni kweli MUNGU wa kweli ana ushirika na MAJINI?yani anasikiliza sala za majini na anazijibu?yani ana urafiki na majini???
Kwahiyo tunakubaliana kwamba kupiga picha na bible au kudai unatumia bible sio issue,issue ni bible kukubaliana na wewe mganga.Sio wakristo wote wenye kuikubali hiyo novena na ni utaratibu ambao haupo kwenye biblia, kwahiyo kuhusishwa Mungu sio shida hata manabii feki wanamuhusisha Mungu tena katika nyumba ya Mungu ila wanatumia nguvu za giza huku wakimtaja Yesu.
Hakuna popote bible imeandika inawezatumika kutibu watu ndio maana naweza kwambia tu,aliyeandika hivi kavimbiwa mihogo tu,tofauti na neema za Quran kwamba inawezatumika kutibia watu.Haya tizama huu uchawi wa biblia halafu niambie nani karuhusu biblia kutumika hivi.
Hiyo Aya imeamrishwa baada ya makafiri kuanza kuupiga vita uislam huku waislam wakiuliwa wakiwa wanasubiri hukumu ya Mwenyezi Mungu anawaambiaje kuhusu visa na mauaji wanayo fanyiwa na makafiri ndio ikashuka surah nzima ya Al taubah kuwapa muongozo waumini nini cha kufanya ukisoma yote ndio utaelewa huko mwanzo kabisa Mwenyezi Mungu anasemaKama huijui Jazya tutaongea nini mimi na wewe ?
Hata Ku google hutaki
AT-TAWBA - 29)
Piganeni na wasio muamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, wala hawashiki Dini ya Haki, miongoni mwa walio pewa Kitabu,
mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii.
Hiyo Kodi ndio Jazya
"Wala msiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuuliwa isipo kuwa kwa haki..."
Hiyo Aya imeamrishwa baada ya makafiri kuanza kuupiga vita uislam huku waislam wakiuliwa wakiwa wanasubiri hukumu ya Mwenyezi Mungu anawaambiaje kuhusu visa na mauaji wanayo fanyiwa na makafiri ndio ikashuka surah nzima ya Al taubah kuwapa muongozo waumini nini cha kufanya ukisoma yote ndio utaelewa huko mwanzo kabisa Mwenyezi Mungu anasema
9:13 - Je, hamtapigana na watu walio vunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumfukuza Mtume, nao ndio walio kuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.
Kwa maana hapo inaonesha wazi kuwa makafiri ndio walioanza kuwapiga na kuwaua waislam hivyo nao wakaamuliwa wapigane wasiwe legelege kuangalia wanakufa tu kama kuku
Uislamu unakataza kuua nafsi bila sababu yoyote
Surah Al-Isra (17:33):
Hii hoja nimeijibu katika comment #197AT-TAWBA - 29)
Piganeni na
1. wasio muamini Mwenyezi Mungu (Allah)
2. wala Siku ya Mwisho,
(Kiyama)
3. wala hawaharimishi alivyo harimisha Mwenyezi Mungu na Mtume, ( Nguruwe)
4. wala hawashiki Dini ya Haki,
(Uislamu)
miongoni mwa walio pewa Kitabu, (Wayahudi na Wakristo)
5. mpaka watoe kodi kwa khiari yao, hali wamet'ii. (Jazya)
Vipi kama hiyo kodi hawana ?
Ni kipigo hadi ufe au usilimu
Kuna dini hapo ?
Hakuna kulazimisha dini ni danganya toto
(AL I'MRAN - 85)
Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.
Usiombe kuishi kwenye Islamic State:Hii hoja nimeijibu katika comment #197