Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Kwahiyo ukimuabudu Mungu hiyo ndio tiba?
Ndio, ukiona jini lililoasi limekuingia jiangalie ibada zako zitakuwa haziposawa kwahiyo kuondoa hiyo shida rudi kwa Mola wako na ufanye ibada kwa usahihi
 
Mimi nimeweka ushahidi siongei maneno matupu kama wewe, nimekuwekea ushahidi wa jinsi biblia inavyotumika kwenye ushirikina sasa mimi sipo hapa kukushawishi wala kukulazimisha kukubali hilo halinihusu wewe amini utakavyo ni uhuru wako.

Kama unaona biblia haiwezi kutumika kwenye kuagua sawa ila inatumika kwenye ushirikina na ushahidi nimeweka.

Maombi ya novena hayapo kwenye biblia ni utaratibu tu ambao watu wameuunda wa maombi hakuna tofauti na albadri.
 
Uislamu na uganga/uchawi ni kama shingo na kichwa.
 
Ndio, ukiona jini lililoasi limekuingia jiangalie ibada zako zitakuwa haziposawa kwahiyo kuondoa hiyo shida rudi kwa Mola wako na ufanye ibada kwa usahihi
Hicho unachoeleza kipo kimaandiko au ni mtazamo binafsi?
 
Sasa mbona mleta mada anasema hakuna uchawi na anakataa hadi matumizi ya kutumia Qur'an kama tiba?
 
Sasa mbona mleta mada anasema hakuna uchawi na anakataa hadi matumizi ya kutumia Qur'an kama tiba?
Sijaona sehemu kakataa uchawi, Quran siyo tiba ya busha wala uchawi, Quran ni muongozo wa namna Gani binadam wahusiane wao kwa wao na wao na mungu
 
Wewe una andiko linaloonesha tofauti na nilichokisema? Hebu nifunze kwalo nipate ufahamu
Mimi najua tiba sahihi ya kisheria kwenye uislamu ni Ruqya kwa matatizo kama hayo ya majini, ila wewe unasema tiba ni kuswali tu.
 
Sijaona sehemu kakataa uchawi, Quran siyo tiba ya busha wala uchawi, Quran ni muongozo wa namna Gani binadam wahusiane wao kwa wao na wao na mungu
Amesema kabisa haamini uchawi, yeye anachukulia uchawi ni imani hewa tu ila kwenye imani za uchawi watu humshirikisha Mungu ndio maana kautaja uchawi kwenye mada yake ila yeye haamini kuwepo kwa uchawi.

Kwahiyo tiba ya uchawi ni ipi? Maana kama uchawi upo basi pia ipo tiba ya kuondoa madhara yenye kusababishwa na uchawi.
 
Mimi najua tiba sahihi ya kisheria kwenye uislamu ni Ruqya kwa matatizo kama hayo ya majini, ila wewe unasema tiba ni kuswali tu.
Lete andiko, mimi lakwangu hili hapa

Allah anasema(Suratul-taghaabun)
64:11 - Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Kwahiyo misiba na matatizo mengine yote hayampati mja isipokuwa kwa idhini yake Mwenyezi Mungu na suluhisho la hayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu lete lakwako
 
Hivi uchawi ni ugonjwa? Maana nijuavyo mimi imesuniwa kuwa Mwenyezi Mungu hakuleta ugonjwa isipokuwa na tiba yake

Sasa je uchawi ni ugonjwa? Au ni imani tu za kishirikina
 
Hivi uchawi ni ugonjwa? Maana nijuavyo mimi imesuniwa kuwa Mwenyezi Mungu hakuleta ugonjwa isipokuwa na tiba yake

Sasa je uchawi ni ugonjwa? Au ni imani tu
Uchawi unaweza kutumika kumsababisha mtu ugonjwa, hata uwepo wa majini ni imani mkuu ndio maana nilikwambia kuna waislamu wengine hawaamini uwepo wa majini kama ambavyo wewe hauamini uchawi.
 
Hii mada haikuhusu kaa pembeni hatupo hapa kukejeli tupo hapa kufundishana kwa tusiyoyajua wewe na kejeli zako anzisha uzi wako

After all wewe sio miongoni mwa masheikh niliyowazungumzia hapa
We maamuma,Nikikuambia kwamba msingi wa elimu ya usihiri upo kwenye juzuu moja wapo katika msururu wa juzuu zenu je utanibishia?,sidhqn kama kuna shehe anakosa kitabu kama Abu maashar al falak kabir na vinginevyo ambavyo ni vitabu vya usihiri,
 
Uchawi unaweza kutumika kumsababisha mtu ugonjwa, hata uwepo wa majini ni imani mkuu ndio maana nilikwambia kuna waislamu wengine hawaamini uwepo wa majini kama ambavyo wewe hauamini uchawi.
Hebu tupe mfano wa hayo magonjwa pia ungejibu na hiyo hoja hapo juu nipate kuunganisha na hii
 
Mimi nimeweka ushahidi siongei maneno matupu kama wewe,
ushahidi sio hizo picha na story za kusadikika ni field ya waganga wakiagua kwa kutumia biblia.
nimekuwekea ushahidi wa jinsi biblia inavyotumika kwenye ushirikina sasa mimi sipo hapa kukushawishi wala kukulazimisha kukubali hilo halinihusu wewe amini utakavyo ni uhuru wako.
sio swala la kuamini ni swala la kujua,nawewe unatakiwa ujue kuanzia leo,mganga anayetumia bible anakuona wewe kiazi.
Kama unaona biblia haiwezi kutumika kwenye kuagua sawa ila inatumika kwenye ushirikina na ushahidi nimeweka.
hakuna hiyo kitu.
Maombi ya novena hayapo kwenye biblia ni utaratibu tu ambao watu wameuunda wa maombi hakuna tofauti na albadri.
Usifananishe novena na uchawi wa kiislam ndugu,sio haki.
 
We maamuma,Nikikuambia kwamba msingi wa elimu ya usihiri upo kwenye juzuu moja wapo katika msururu wa juzuu zenu je utanibishia?,sidhqn kama kuna shehe anakosa kitabu kama Abu maashar al falak kabir na vinginevyo ambavyo ni vitabu vya usihiri,
Hizo zote ulizotaja ni shirki hivyo wanayofanya hayo wana ya kujibu mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya kiyama

Albadir ni shirki

Falaki ni ushirikina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…