Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Masheikh mliosoma dini na kupata nyadhifa katika jamii acheni tabia ya kuchanganya dini na uganga/uchawi

Sikupinga ila nilitaka ulete andiko na nikasema kitu kama hakina uthibitisho maana yake sio sahihi hatimae umeleta
Hiyo hadithi sio kuwa nilikuwa siijui ila nilihitaji uilete na umeileta haya na tuijadili ili tuone kinachofanyika katika Rukya za masheikh ni shirki au sio shirki?

Hivyo basi nipe na Hadith au andiko la masharti ya rukya ili tuendelee
Ulivyosema hakuna ithibati ya Ruqya ulikuwa umekusudia nini?
 
Dumu nazo hizo zote ongezea na DHIKRI, dua, sadaka, kumtendea wema ndugu au jirani yako, kuondoa mwiba ulio barabarani na kuuweka kando n.k n.k, pia jiepushe na shirki na riya mwili wako utakuwa na ulinzi madhubuti hakuna kiumbe atakae kugusa na kapu la yote hayo ni SWALAA,
Allah anasema (Ankabut)
29:45 - SOMA uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini KUMDHUKURU Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda.
Kwahiyo unachosema inatakiwa muislamu afanye ibada zote kwa ujumla wake hadi kuondoa jiwe njiani hapo ndio atapata ulinzi?
 
Kuna hii tabia ambayo imeshakuwa mazoea kwa wengi wa masheikh wa kitanzania na Afrika kwa ujumla kuchanganya dini na uganga au uchawi.

Utakuta mtu kasoma dini vizuri na ana elimu kubwa lakini badala ya kuitumia elimu hiyo katika kufanya mema na kuitafuta pepo ya Allah (S. W) huitumia kama kigezo cha kuaminika katika masuala ya kiuganga na kichawi jambo ambalo haliruhusiwi katika dini na ni shirki

Katika Surat mubayyina, Allah anasema baada ya Bismillah Arahman rahiim

98:1 - Hawakuwa walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina waache walio nayo mpaka iwajie bayana,

98:2 - Yaani Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasika,

98:3 - Ndani yake mna maandiko yaliyo nyooka

98:5 - Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.

Katika aya hizo M/Mungu anasema waumini wote na masheikh hatujaamrishwa ila tuwe wema, tutoe zaka na kusali hayo ya uganga na ushirikina mmeyatoa wapi nyie masheikh nawauliza?

Mmeiharibu dini kiasi kuwa uislamu unaonekana ni dini ya wachawi na mila zingine potofu mlizokuwa nazo kabla hata hamkuujua huo uislamu wala elimu ya dini.

Kupitia andiko hili kama wewe ni Sheikh na una tabia hiyo iache mara moja na tubia kwa Mwenyezi Mungu haraka kabla kifo hakija kufika itakuwa ni khasara kwako siku ya kiyama

NB, tujadili kistaarabu
Nionavyo mimi, Uislam uko karibu sana na ushirikina, uchawi na uganga.
 
Kwahiyo nisingeleta ingebaki kauli yako kwamba Ruqya haina ithibati kwamba ushahidi wa Ruqya.
Unaongea bila uthibitisho yani unatoa kichwani na yenyewe umeleta hadithi moja ya kuokoteza hadi sasa

Kuleta nyingine au andiko kuhusu masharti ya Rukya hutaki maana unajua itakavyokuwa kwa uganga unaofanywa na masheikh unaangukia kwenye shirki haukidhi vigezo vya Rukya unayopigia gitaa hapo
 
Hoja sio kuwa kumsomea mtu ni shirki,

Hoja imetokana na wewe kusema kwakuwa wewe msomaji unaitakidi kwa Allah na sio Adhana hivyo hata huyo unaemsomea asipoitakidi kwa Allah na akiitakidi katika Adhana au msomaji wewe msomaji haikuhusu kwa maana yeye ndio anakuwa mshirikina ila sio wewe, yani umtumbukize mwenzio katika shirki na wewe uwe salama?

Na hapo ndio utajua kuiepuka shirki kwa kuganga na Adhana ni kitu ambacho uwezekano wake ni mdogo sana kwa kuzingatia masharti na nature ya waaguliwa na muaguaji
Lakini mwanzoni ulisema ni shirki.
sasa hivi unasema tena kutokana na mimi nilivyosema, Mimi nimeeleza kidogo tu kuhusu shirki ilivyokuwa pana, Unafikiri hata wewe unavyodai mtu afundishwe ajisomee mwenyewe hawezi kufanya shirki ?.
Wewe unaweza kumfundisha vizuri kabisa kuwa ajisomee qur an na awe na itakidi kuwa anayeponya ni ALLAH apo wewe umemaliza kwa upande wako suala linabaki kwake je yeye atafanya hivyo au ataitakidi tofauti.
 
Lakini mwanzoni ulisema ni shirki.
Na hata andiko langu limejikita hapo ila wewe ndio ukaelezea na kusema shirki ni pana ila ukweli kumsomea mtu ni shirki hasa kwa waganga hawa wa kiafrika ila tukizungumza hayo mnakuja na utetezi wa kuwa shirki ni jambo kubwa kwahiyo tusiwaseme kuwa wanafanya shirki
Wewe unaweza kumfundisha vizuri kabisa kuwa ajisomee qur an na awe na itakidi kuwa anayeponya ni ALLAH apo wewe umemaliza kwa upande wako suala linabaki kwake je yeye atafanya hivyo au ataitakidi tofauti.
Ni bora umfundishe asome mwenyewe na ajue jinsi ya kujikinga na madhara yatokayo na majini kuliko kufanya kitengo cha uganga na kuwasomea wenye majini tena kwa Adhana eti wanaagua majini. Na siku hizi hadi matangazo wanatoa kabisa halafu tukisema ni shirki tunaambiwa tunahukumu yani tusizungumze kabisa kuhusu shirki maana tukizungumza tunahukumu
 
Unaongea bila uthibitisho yani unatoa kichwani na yenyewe umeleta hadithi moja ya kuokoteza hadi sasa

Kuleta nyingine au andiko kuhusu masharti ya Rukya hutaki maana unajua itakavyokuwa kwa uganga unaofanywa na masheikh unaangukia kwenye shirki haukidhi vigezo vya Rukya unayopigia gitaa hapo
Haya lete wewe basi hadithi sahihi yenye kueleza masharti na vigezo vya Ruqya unayoisema wewe.
 
Back
Top Bottom